Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
- Wakati wa kutamka irabu,hewa hauzuiliwi katika ala za kutamka lakini katika kutamka
lonsonanti,hewa huzuiliwa/hubanwa
monica20 answered the question on October 12, 2017 at 15:48
- Kamilisha kwa vielezi viigizi vifuatavyo: (i) Funga mlango (ii) Yule mtu ananuka(Solved)
Kamilisha kwa vielezi viigizi vifuatavyo:
i) Funga mlango
ii) Yule mtu ananuka
Date posted: October 12, 2017. Answers (1)
- Weka nomino zifuatazo katika ngeli zake. (i) Kipepeo (ii) Maziwa(Solved)
Weka nomino zifuatazo katika ngeli zake.
i) Kipepeo
ii) Maziwa
Date posted: October 12, 2017. Answers (1)
- Tunga sentensi katika kauli ya kutendewa ukitumia vitenzi vifuatavyo (i) Wa (ii) Chwa(Solved)
Tunga sentensi katika kauli ya kutendewa ukitumia vitenzi vifuatavyo
i) Wa
ii) Chwa
Date posted: October 12, 2017. Answers (1)
- Andika katika usemi halisi
Juma alisema kwamba hangependa kumwona mwanawe akiteseka.(Solved)
Andika katika usemi halisi
Juma alisema kwamba hangependa kumwona mwanawe akiteseka.
Date posted: October 12, 2017. Answers (1)
- Andika sentensi ifuatayo katika umoja;
Hao wenyewe hawakuzingatia mafunzo ya lishe bora.(Solved)
Andika sentensi ifuatayo katika umoja;
Hao wenyewe hawakuzingatia mafunzo ya lishe bora.
Date posted: October 12, 2017. Answers (1)
- Tumia kirejeshi - O – tamati katika sentensi ifuatayo:
Kijana ambaye anapendeza ni yule ambaye hutia bidii.(Solved)
Tumia kirejeshi - O – tamati katika sentensi ifuatayo:
Kijana ambaye anapendeza ni yule ambaye hutia bidii.
Date posted: October 12, 2017. Answers (1)
- Andika kwa ukubwa;
Kiti kilichokuwa kimekaliwa na mwanamke kilivunjika.(Solved)
Andika kwa ukubwa;
Kiti kilichokuwa kimekaliwa na mwanamke kilivunjika.
Date posted: October 12, 2017. Answers (1)
- Bainisha aina za shamirisho katika sentensi:
Shule nzuri ilijengewa wanafunzi kwa matofali(Solved)
Bainisha aina za shamirisho katika sentensi:
Shule nzuri ilijengewa wanafunzi kwa matofali
Date posted: October 12, 2017. Answers (1)
- Tumia neno “kimya” katika sentensi kama:
(i) Kielezi
(ii) Kihisishi(Solved)
Tumia neno “kimya” katika sentensi kama:
(i) Kielezi
(ii) Kihisishi
Date posted: October 12, 2017. Answers (1)
- Onyesha (i) Kielezi (ii) Kitenzi katika sentensi: Mvua ilinyesha mfululizo(Solved)
Onyesha (i) Kielezi (ii) Kitenzi katika sentensi: Mvua ilinyesha mfululizo
Date posted: October 12, 2017. Answers (1)
- Bainisha vishazi katika sentensi ifuatayo:
Katiba ambayo ilipingwa na wengi haitetei maslahi ya wananchi.(Solved)
Bainisha vishazi katika sentensi ifuatayo:
Katiba ambayo ilipingwa na wengi haitetei maslahi ya wananchi.
Date posted: October 12, 2017. Answers (1)
- Akifisha sentensi hii kwa njia tatu tofauti ili kuleta dhana tatu tofauti.
Babu alimchapa nyanya(Solved)
Akifisha sentensi hii kwa njia tatu tofauti ili kuleta dhana tatu tofauti.
Babu alimchapa nyanya
Date posted: October 12, 2017. Answers (1)
- Tunga sentensi moja kudhihirisha maana tofauti ya maneno yafuatayo:(Solved)
Tunga sentensi moja kudhihirisha maana tofauti ya maneno yafuatayo:
Date posted: October 12, 2017. Answers (1)
- Onyesha shadda katika neno lifuatalo: mlima(Solved)
Onyesha shadda katika neno lifuatalo: mlima
Date posted: October 12, 2017. Answers (1)
- Ainisha mofimu zinazopatikana katika neno lifuatalo: Angemlia(Solved)
Ainisha mofimu zinazopatikana katika neno lifuatalo: Angemlia
Date posted: October 12, 2017. Answers (1)
- Tunga sentensi ukitumia kielezi cha;
Wakati(Solved)
Tunga sentensi ukitumia kielezi cha;
Wakati
Date posted: October 12, 2017. Answers (1)
- Tunga sentensi ukitumia kielezi cha;
i) Mahali(Solved)
Tunga sentensi ukitumia kielezi cha;
i) Mahali
Date posted: October 12, 2017. Answers (1)
- Andika sauti mwambatano inayotamkiwa kwenye ufizi.(Solved)
Andika sauti mwambatano inayotamkiwa kwenye ufizi.
Date posted: October 12, 2017. Answers (1)
- Huku ukitoa mfano mmoja mmoja taja makundi mawili ya sauti.(Solved)
Huku ukitoa mfano mmoja mmoja taja makundi mawili ya sauti.
Date posted: October 12, 2017. Answers (1)
- Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Jambazi wa kimataifa ni tatizo lililowasumbua walimwengu kwa muda mrefu sana. Serikali nyingi
zimetumia mapesa mengi kwa miaka...(Solved)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Jambazi wa kimataifa ni tatizo lililowasumbua walimwengu kwa muda mrefu sana. Serikali nyingi
zimetumia mapesa mengi kwa miaka mingi sana zikijitahidi kupambana na janga hili. Hata hivyo,
fanaka haijapatikana, wala haielekei kamwe itapatikana leo au karne nyingi baadaye.
Yamkini tatizo kubwa lililopo ni kuhusu jelezi la dhana ya “ujambazi” tena “tena “wa kimataifa”.
Hili ni tatizo mojawapo na yapo mengi sana. Tatizo la pili ni kiburi. Kuna wale watu binafsi na hasa
viongozi wa nchi kubwakubwa na serikali zao zilizojiaminisha kuwa ujambazi ni balaa kweli, tena
belua, lakini huo ni wa huko, wala hauwezi kuwagusa licha ya muwashtua wao.
Kulingana na maoni ya watakaburi hao,ujambazi ni wa watu ‘washenzi’ wasiostaarabika,
wapatikanao katika nchi zisizoendelea bado. Ujambazi pekee wanaouona unafaa kukabiliwa ni
dhidi ya mbubujiko wa madawa ya kulevya uliosababishwa na vinyangarika kutoka nchi hizo
maalum za ‘’ ulimwengu wa tatu” . Kulingana na wastaarabu wa nchi zilizoendelea, vinyangarika
hivi ndivyo hasa adui mkubwa wa ustaarabu ulimwenguni na ni sharti vifagiliwe mbali bila huruma.
Baada ya kusagwa sagwa, ulimwengu mstaarabu utazidi kutononoka na ahadi ya mbingu hapa
ardhini itakamilika.
Imani ya watu ya kuwa ujambazi wa kimataifa, hata iwapo upo, hauwezi kuwashtua wala
kuwatingisha wao ilikuwa kamili na timamu. Ilikuwa kamili na timamu hadi hapo mwezi Septemba
tarehe 11 mwaka wa 2001, ndege tatu za abiria zilipoelekezwa katika majumba mawili ya fahari,
yenye urefu wa zaidi ya ghorofa mia moja na kuyatwangilia mbali. Mshtuko na kimako! Kimako
kwa kuwa, kabla ya siku hiyo, wamarekani hawangeweza kudhani kwamba ingewezekana taifa
lolote au mtu yeyote kuthubutu kuishambulia nchi yao. Taifa wasifa lililojihami barabara dhidi ya
aina yoyote ile ya uchokozi kutoka pembe lolote la dunia.
Hakuna ulimwenguni mzima, aliyeamini kuwa Marekani ingeweza kushambuliwa. Kwa ajili hiyo,
mshtuko uliitingisha ardhi yote na huzuni ilitanda kote, kama kwamba sayari nzima
imeshambuliwa, wala sio Marekani pekee.
Mintarafu hiyo, Marekani ilipolipiza kisasi kwa kuwaunguza waliokuwemo na wasiokuwemo kwa
mabomu hatari huko Afghanistan, idadi kubwa ya watu duniani ilishangilia na kusheherekea. Kwa
bahati mbaya, tafsiri ya shambulizi la minara – picha ya Newyork na lile la Pentagon, uti wa uwezo
wa kivita wa Marekani, ilizorota. Kuna wengi waliodhani huo ni mwanzo wa vita vya Waislamu dhidi
ya Wakristo na kwa muda, Waislamu wote wakashukiwa kimakosa kuwa ni majambazi wa
kimataifa.
Ukizingatia aya tatu za mwisho, fafanua fikira za watu na mambo yote yaliyotokea baaada ya
Septemba tarehe 11, 2001 (Maneno 65 -75)
Date posted: October 12, 2017. Answers (1)