Taja sifa zinazofanya utanzu uwe wa fasihi simulizi

      

Taja sifa zinazofanya utanzu uwe wa fasihi simulizi

  

Answers


KELVIN
i.Fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya mdomo ilhali fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi.
ii.Fasihi simulizi huhifadhiwa akilini ilhali fasihi aandishi huhifadhiwa kwa maandishi.
iii.Fasihi simulizi ni mali ya jamii ilhali fasihi andishi ni mali ya mtu binafsi/mwandishi.
iv.Fasihi simulizi ina wahusika wa kila aina k.v binadamu, wanyama na ndege, mazimwi na majitu, miungu, mizimu, mashetani na vitu visivyo na uhai k.v. mawe na miti ilhali fasihi andishi ina wahusika binadamu kwa kiasi kikubwa.
v.Fasihi simulizi ina tanzu nyingi kuliko fasihi andishi.
vi.Uwasilishaji wa fasihi simulizi huweza kuandamana na utendaji k.v matumizi ya ishara, nyimbo, makofi, kuimba, kubeba zana katika majigambo n.k ilhali ule wa fasihi andishi hauandamani na utendaji isipokuwa inapowasilishwa mbele ya hadhira.
vii.Fasihi simulizi huwasilishwa mbele ya hadhira ilhali fasihi andishi si lazima iwasilishwe mbele ya hadhira.
viii.Fasihi simulizi huwasilishwa mahali maalum k.v jandoni, matangani, arusini, n.k ilhali fasihi andishi haina mahali maalum.

kalvinspartan answered the question on October 20, 2017 at 16:23


Next: Taja sifa tano za visasili.
Previous: Taja sifa zinazozofananisha fasihi andishi na fasihi simulizi.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions