Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Eleza tofauti kati ya hadhira ya fasihi andishi na fasihi simulizi.

      

Eleza tofauti kati ya hadhira ya fasihi andishi na fasihi simulizi.

  

Answers


KELVIN
a)Hadhira ya fasihi simulizi huweza kuwasiliana moja kwa moja na mwasilishaji ilhali ile ya fasihi simulizi sio lazima iwasiliane na mwandishi.
b)Hadhira huchangia katika uwasilishaji wa fasihi simulizi k.v kwa kuimba, kupiga makofi n.k (hadhira tendi/hai) ilhali hadhira ya fasihi andishi haichangii katika uandishi.
c)Hadhira ya fasihi simulizi huonana na mwasilishaji ilhali ile ya fasihi andishi si lazima ionane na mwandishi.
d)Hadhira ya fasihi simulizi ni kubwa kuliko ile ya fasihi andishi kwani huhusisha hata wasiojua kusoma na kuandika.
e)Hadhira ya fasihi simulizi ni hai yaani inajulikana na fanani ilhali ile ya fasihi simulizi si hai yaani haijulikani na mwandishi.
f)Hadhira ya fasihi simulizi hainunui kazi ilhali ile ya fasihi andishi hununua kazi.
g)Hadhira ya fasihi simulizi yaweza kumiliki kazi ya fanani lakini ile ya fasihi andishi haiwezi kumiliki kazi ya mwandishi.
h)Hadhira ya fasihi simulizi huchagua kwa kulenga watu wa rika fulani lakini ile ya fasihi andishi hailengi watu wa rika yoyote.

kalvinspartan answered the question on October 20, 2017 at 16:29


Next: Taja sifa zinazozofananisha fasihi andishi na fasihi simulizi.
Previous: Kuna umuhimu gani kufunza fasihi simulizi katika chuo za upili?

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions