Taja na ueleze aina za wahusika katika Fasihi Simulizi.

      

Taja na ueleze aina za wahusika katika Fasihi Simulizi.

  

Answers


KELVIN
Wahusika katika Fasihi Simulizi

Wahusika ni viumbe wa sanaa ambao hutumiwa katika kazi ya fasihi kuwasilisha maswala mbalimbali.wafuatao ni wahusika katika fasihi simulizi.

1.Fanani-anayetunga na kuwasilisha fasihi simulizi.

2.Hadhira-wale wa kusikiliza, kutazama, kushiriki wa kuimba, kuuliza maswali, kutegua vitendawili, kupiga makofi, n.k. kuna aina mbili za hadhira: (i) hadhira tendi/hai na (ii) hadhira tuli.

3.Wanyama-wanaofanya kama binadamu na kuwakilisha sifa kama vile ujanja, ulaghai, tamaa na ujinga na wanaobakia wanyama tu.

4.Binadamu katika uhalisia wake

5.Mazimwi na majitu-viumbe vyenye matendo na maumbile ya kutisha kama vile jicho moja, vichwa viwili au zaidi, nusu mtu na nusu myama, wenye tamaa iliyokithiri ya kuweza kumeza kila kitu.

6.Wahusika vitu (visivyo na uhai) mawe, miti, vijaluba, vibuyu-hutumiwa kuibua imani za kidini.

7.Mizimu-roho za waliokufa-hutembea, hula na huathiri binadamu.

8.Miungu-viumbe vyenye uwezo mkubwa dhidi ya binadamu k.m. katika ngano za usuli, mighani na visasili.
kalvinspartan answered the question on October 20, 2017 at 16:34


Next: Taja sababu zinazochangia katika kubadilika kwa Fasihi Simulizi
Previous: Taja sababu nne za kutotumia kuchunza kama njia ya kukusanya fasihi simulizi.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions