Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Ni matatizo yapi yanayomkabili mkusanyaji wa Fasihi Simulizi.

      

Ni matatizo yapi yanayomkabili mkusanyaji wa Fasihi Simulizi.

  

Answers


KELVIN
a) Gharama ya utafiti, huenda ikawa kubwa kiasi cha mtafiti kutoimudu huenda akakosa pesa za kusafiri au kununua vifaa.
b) Mtazamo hasi wa wanajamii kuhusu ujazaji wa hojaji huenda ukawafanya wengi wao kutojaza hojaji hizo.
c) Wanajamii wengine huweza kushuku kwamba mtafiti anawapeleleza na wakakatoa kutoa habari.
d) Baadhi ya mafanani au wahojiwa huenda wakadai walipwe kabla ya kutoa habari zozote.
e) Mbinu nyingine k.m hojaji huhitaji watu wanaojua kusoma na kuandika ikiwa watu wanaohojiwa hawajui kusoma na kuandika matokeo ya utafiti huenda yasiwe ya kutegemewa.
f) Vizingiti vya kidini .hutokea pale ambapo wahojiwa wanaamini kuwa matendo ya fasihi simulizi k.m matambika ni kinyume cha dini hivyo kukataa kuhojiwa.
g) Kupotea au kufisidiwa kwa vifaa vya kuhifadhia data, yote yaliyohifadhiwa kwayo pia hupotea.
h) Uchache wa wazee au wataalamu wa fasihi simulizi, fasihi simulizi ilikwa maarufu miongoni mwa wazee na hivyo kukosekana kwao hutatiza ukusanyaji
i) Vikwazo kutoka kwa watawala, huenda watawala wakakataa kutoa idhini ya kufanya utafiti baadhi ya taasisi fadhili pia huenda zikakataa kudhamini utafiti.
j) Wadhamini mara nyingi ndio huamua mambo yanayochunguza, mahali pa kuchunguziwa na mawanda au upeo wa uchunguzi la sivyo, mapendekezo hufutiliwa mbali.
k) Huenda mtafiti asiwe na muda wa kutosha kuwahoji watu wengi, basi hatapata habari za kutosha kuhusu mada husika.
l) Matatizo ya mawasiliano na uchukuzi k.m katika kuenda katika sehemu zilizo kama, bila uchukuzi au vyombo vya usafiri.
m) Matatizo ya kibinafsi, mtafiti anaweza kushindwa kuidhibiti hadhira badala ya kuwauliza maswali, mhojiwa ndio huweza kumuuliza mtafiti maswali pia kutojua lugha husika huwa tatizo
n) Ukosefu wa usalama huenda mtafiti akavamiwa aidha baadhi ya watu si karimu na huenda wakamshuku mtafiti ua kumvamia.
o) Tafsiri za data pia ni tatizo fasihi simulizi huendelezwa kwa lugha za kijamii kupata msamiati unaofaa kufasiri lugha chanzi hadi lugha pokezi ni tatizo.
kalvinspartan answered the question on October 20, 2017 at 16:41


Next: Taja umuhimu wa kuhifadhi Fasihi Simulizi
Previous: Taja njia zinazotumiwa na jamii ya sasa kuhifadhi Fasihi Simulizi

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions