Mtambaji bora anafaa kuwa na sifa zipi?

      

Mtambaji bora anafaa kuwa na sifa zipi?

  

Answers


KELVIN
a)Asiwe mwoga ili kuweza kuzungumza hadharani.
b)Asiwe na haya ili kuweza kuzungumzia mambo ya aibu inapobidi.
c)Awe na uelewa wa mazingira na masuala ibuka katika jamii ili kuweza kuwasilisha dhana zisizopatikana katika mazingira yake k.m. kutumia rais kuelezea dhana ya mfalme.
d)Awe na ufahamu mpana wa lugha ili aweze kuitumia kwa uhodari na kuwasilisha kwa wepesi.
e)Awe mchanganfu na mcheshi ili kunasa makini ya hadhira na kuzuia isikinai.
f)Awe na ufahamu mpana wa utamaduni husika ili kuzuia kutumia maneno na ishara zinazoweza kuwaudhi au kupingana na imani za hadhira.
g)Awe na uwezo wa kushirikisha hadhira k.v. kuimba, maswali ya balagha ili isikinai, n.k.

kalvinspartan answered the question on October 21, 2017 at 10:01


Next: Eleza majukumu ya hadithi katika jamii.
Previous: Taja mifano minne ya mianzo katika hadithi.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions