Eleza sifa tano za semi.

      

Eleza sifa tano za semi.

  

Answers


KELVIN
a) Semi hufumba ujumbe wake kwa mfano maana ya ndani ya nahau “piga kalamu’ ni‘futa kazi’ ilhali maana ya juu ni ‘kuchapa au kugonga kalamu methali pia huwa na maana iliyofumbwa aidha vitendawili hufumba jibu.
b) Hutumia picha (taswira) na ishara kupitisha ujumbe wake, mtu anaposema ‘kwetu ni jehanamu; ile picha ya jehanamu inajichora akilini mwa msikilizaji, jehanamu hapa inamanisha mahali pabaya penye mateso mengi
c) Maana ya semi hupatikana katika jamii iliyozibuni, methali “mgaaga na upwa hali wali mkavu” kwa mfano itaeleweka na jamii za pwani.Vile vile katika tashbihi weupe au weusi, hulinganishwa na vitu mbalimbali kutegemea jamii na mazingira yake.mathalani, watasema –eupe kama maziwa au theluji-eusi kama mpingo, lami au makaa kutegemea vifaa vinavyopatikana katika jamii husika.
d) Huwasilisha ujumbe mrefu kwa maneno machache mfano ni methali ‘juhudi si pato’ambayo imefupisha ujumbe mrefu kuwa mtu huweza kufanya bidii sana na akakosa kufanikiwa, Semi huwasilisha ujumbe kwa njia ya mkato tofauti na hadithi ambazo ni masimulizi marefu.
e) Semi ni tanzu tegemezi, hii ina maana kwamba semi hutokea kuambatana au kutegemea tanzu nyingine kwa mfano methali hutolewa katika muktadha wa mazungumzo ya kutoa mawaidha au mwishoni mwa hadithi kama funzo la hadhi lakabu, misimu, misemo na nahau pia hupatikana katika utanzu wa mazungumzo.
kalvinspartan answered the question on October 24, 2017 at 14:13


Next: Taja mambo tano yanayofaa kuzingatiwa katika uchambuzi wa ngano.
Previous: Semi zina umuhimu gani kufunzwa katika shule za upili.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions