Eleza aina tofauti za vitendawili.

      

Eleza aina tofauti za vitendawili.

  

Answers


KELVIN
a)Sahili
Vina muundo rahisi/maneno machache k.m Akiona mwangaza wa jua hufa-samaki.
b)Tata
Vyenye majibu tofauti
c)Kisimulizi
Masimulizi k.m. Kulikuwa na baba ng’ambo moja ya mto na binti zake wawili ng’ambo ya pili. Alikuwa na maembe mawili aliyopaswa kuyavukisha pamoja apelekee binti zake. Angefanya nini?
d)Vya tanakali k.m. Parrrr! Mpaka Makka-utelezi.
e)Mkufu
Vyenye sehemu zinazochangizana kimaana k.m. Nikitembea yuko lakini nikiingia nyumbani hupotea-kivuli.

kalvinspartan answered the question on October 24, 2017 at 14:19


Next: Taja sifa tano za vitendawili
Previous: Tambua mbinu za lugha ambazo zinatumika katika vitendawili

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions