Eleza maana ya vitanza ndimi huku ukitoa umuhimu wake

      

Eleza maana ya vitanza ndimi huku ukitoa umuhimu wake

  

Answers


KELVIN
Sentensi zenye mfuatano wa sauti zinazotatanisha kimatamshi zinapotamkwa kwa haraka.
Sifa
a)Ni kauli fupi.
b)Huwa na mchezo wa maneno.
c)Huundwa kwa sauti zinazokaribiana kimatamshi.
d)Hutumia maneno yenye maana zaidi ya moja au yenye sauti sawa.
e)Hutanza/hutatiza ndimi za wengi wakalemewa kutamka.
f)Hukanganya kimatamshi.

AMA

a) Kimsingi, vitanza ndimi ni mchezo wa maneno na sauti.
b) Huundwa kwa maneno ambayo yana sauti zinazokaribiana kimatamshi maneno haya huweza kuwa na maana nyingi au yenye kukabiriana kimaana.
c) Ukinzani wa maneno kisauti na kimaana huyafanya matamshi ya maneno kuutatiza ulimi.

kalvinspartan answered the question on October 24, 2017 at 14:27


Next: Ni sifa zipi zinazotambulisha chemshabongo.
Previous: Taja asili nne za lakabu.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions