Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Jadili mikondo hewa yoyote mitatu inayotumika katika utamkaji wa sauti za binadamu

      

Jadili mikondo hewa yoyote mitatu inayotumika katika utamkaji wa sauti za binadamu

  

Answers


ELVIS
Mikondo hewa ni njia ambayo hewa husafiria wakati wa matamshi. Binadamu hutumia sauti za lugha mbalimbali katika mawasiliano zinazotokana na lala za matamshi amabayo huwezeshwa na mfumo wamkondo wa hewa.

Kuna namna tatu kuu za mfumo wa mkondo hewa. Nazo ni:
Mfumo mkondo hewa wa mapafuni
Mfumo mkondo kinywani.
Mfumo mkondo hewa puani

Upatikanaji wa sauti za lugha za binadamu hufananua jinsi sauti za lugha husika zinavyotamkwa katika bomba la sauti la mwanadamu.

Chemba ya mapafuni
Hewa itokayo kwenye chemba ya mapafu ambayo mwanadamu hutumia kwa kupumua ili aishi ndiyo hiyo hiyo inayotumika katika utamkwaji wa sauti za lugha zake. Hewa hiyo hupitishwa kwenye chemba zilizomo katika bomba la sauti kwa kupitia chemba ya midomo au chemba ya pua.
Mtu anapotaka kutoa sauti yoyote ile, ni lazima hewa itoke mapafuni kuja nje kupitia pua au midomo. Hivyo matamshi ya sauti mbalimbali hutegemea ni wapi hewa hukatizwa/ huzuiliwa kupita. Sauti hazitamkwi mapafuni bali kwenye ala za matamshi mbalimbali kinywani, ni hewa tu ndiyo inayotoka mapafuni.

Chemba ya puani
Hewa ile kutoka mapafuni ikipitia chemba ya pua basi hisia za sauti inayotamkwa zitakuwa za sauti ng’ong’o.
Wakati huu ala za matamshi – ala sogezi ya kidakatonge hujisusha kutoka kwenye ukuta wa marakaraka ilihewa hiyo ipate kupitia puani; kitendo hiki huachilia hewa nafasi ya kupitia kwenye pua bila kuzuiliwa kutoka nje la bomba la sauti kwa kupitia chemba yam domo lakini wakati huo ala sogezi ya kidakatonge hujibandua kutoka kwenye alapahala ya ukuta wa marakaraka na kuacha nafasi wazi kwa mkondo wa hewa utokao kwenye chemba ya koromeo kupenyeza mpaka kwenye chemba cha pua.

Chemba ya kinywani/midomoni
Hewa hutoka mapafuni isipopitia chemba ya pua itapitia midomo. Hewa ikipitia chemba ya midomoni hadi nje basi hisia za sauti itakayotamkwa zitakuwa za sauti si ng’ong’o.
Katika hali hii, lala sogezi ya kidakatonge huwa imejikweza na kujibandika kwenye ukuta wa marakara kitendo amabacho hakiruhusu hewa kutoka mapafuni kupenya hadi kwenye chemba ya pua bali hupenya kupitia chemba ya midomo.
Midomo ni ala sogezi ya matamshi. Mfano sauti za konsonanti /b/ na /p/ hutamkwa midomoni sauti hizi zinapotamkwa ala sogezi ya midomo chini hujikweza na kujibandika kwenye ala – pahala yam domo juu kiasi kwamba mkondo hewa utokao mapafuni haupati nafasi ya kupenya kuelekea nje ya bomba la sauti kwa kupitia chemba ya midomo.
ELVIS123 answered the question on November 13, 2017 at 03:46


Next: State two role of hydrochloric acid in the digestion food
Previous: Under which principle does the speed governor work?

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions