Fasili ya sintaksia imejaribu kuelezwa na wataalam mbalimbali.kwa mujibu wa masamba na wenzake(1999)sintaksia ni utanzu wa sarufi inayojihusisha na uchunguzi wa mpangilio wa maneno katika sentesi na uhusiano wa vipashio vyake.wanaendelea kusema kuwa utanzu huu uchunguza sheria au kanuni zinazofuatwa katika kuyapanga maneno ili yalete maana yanayokubalika na kueleweka katika lugha husika.pia habwe na karanja (2004)wanasema sintaksia ni utanzu wa isimu unaoshugulikia muundo wa sentesi kama vile kategoria za maneno ,vikundi na vishazi.kutokana na wataalam hawa,twaweza kusema kuwa sintaksia ni utanzu unaojihusisha na uchunguzi wa mpangilio wa maneno katika sentesi na uhusiano wa vipashio vyake,kwa kuzingatia sheria na kanuni za lugha husika ili kuleta mawasiliano.
“kitengo”kwa mujibu wa TOKI(2004) ni mahali pateule panapotengwa kwa shuguli maalum.tunaporejea katika muktadha wa lugha tunaweza kusema kuwa vitengo vya lugha ni vipengele muhimu vinavyounda maarifa ya lugha kwa ujumla.kwa fasili hii,vipengele vinavyounda maarifa ya lugha ni fonolojia,mofolojia,sintaksia na semantiki,kwa hivyo kutokana na kwamba sintaksia pia ni kitengo mojawapo kinachounda maarifa ya lugha ,tunakubali kuwa sintaksia kutenganishwa na vitengo vingine vya lugha kutokana na uhusino mkubwa uliopo baina ya vitengo hivi.vitengo hivi hutegemeana na kuathiriana.hivyo basi tunaweza kuonyesha jinsi sintaksia inavyoweza kutenganishwa na vitengo vingine vya lugha yaani,fonolojia,mofoloji na semantiki kama ifuatavyo.
Uhusiano baina ya fonolojia na sintaksia
Masamba na wenzake wanafasili fonolojia kuwa ni uchambuzi wa mfumo wa sautikatika lugha mahususi.wanaendelea kusema ni jinsi ambavyo vitamkwa au sauti za lugha zinavyoungana ili kujenga maneno yanayokubalika katika lugha,kwa hivyo tunaweza kusema kuwa kuungana kwa vitamkwa ili kujenga maneno yanayokubalika katika lugha Fulani hutegemea mpangilio sahihi wa vitamkwa .na kwa kuwa neon ni kiwango cha msingi cha uchambuzi katika sintaksia basi fonolojia ina uhusiano wa moja kwa moja na sintaksia.mifano ifutayo huthibitisha hoja hii.
1.”anapika”
Hili ni neno lakini pia ni sentensi,hivyo basi huweza kuchanganuliwa kifonolojia kama ifuatavyo;a/n/a/p/i/k/a.mpangilio wa sauti umeunda neno ”anapika”
2(a).baba-limeundwa na (KIKI)
(b)abab-limeundwa na(IKIK)
Katika mfano 2(a) tunaona neno ‘baba’ lina maana na limefuata kanuni na mpangilio unaokubalika wakati mfano 2(b) neno ‘abab’halina maana katika lugha ya Kiswahili kwa sababu halina mpangilio mzuri wa fonimu.
Kwa mifano hii tunaona kuwa hatuwezi kuwa na miundo mikubwa katika sentesi billa kuwa na mpangilio sahihi wa sauti katika lugha.kwa hivyo sintaksia haiwezi kukamilika bila fonolojia.
Uhusiano baina ya sintaksia na mofolojia:
Mofolojia ni kitengo kingine cha lugha ambacho kwa mujibu wa rubanza (1996)ni taaluma inayoshugulikia vipashio vya lugha katika kuunda maneno.kutokana na fasili hii,kipashio cha msingi katika uchambuzi wa kimofolojia ni neno ambalo ndilo hutumika kuunda daraja ya sintaksia.
Vilevile maumbo ya kimofolojia huathiri vipengele vingine vya kisintaksia,kwa mfanmo sentesi zifutazo hufafanua zaidi;
1.mtoto anacheza
2.watoto wanacheza
Katika mifano hii,tunaona kwamba mofimu m- na wa- katika upande wa kiima zimeathiri utokeaji wa mofimu a- na wa- katika upande wa kiarifu.pia kanuni za mfuatano na mpangilio wa mofimu au viambishi zikifuatwa huunda maneno katika miundo kisintaksia.mfano.
Alicheza =a-li-chez-a
Anaimba=a-na-imb-a
Kwa ujumla kipengele cha umoja na wingi katika maumbo ya kimofolojia ndicho kinachoathiri umbo linalofuata jina na kuathiri muundo wa sentensi nzima.mfano,
1.Mwalimu alikuwa anafundisha
2.Walimu walikuwa wanafundisha
Tunaona katika mifano hii maumbo ya umoja na wingi ya maneno,mnwalimu na walimu yameathiri mpangilio mzima wa sentensi.
Uhusiano baina ya semantiki na sintaksia
Habwe na karanja wakimnukuu Richard na wenzake(1985) wanaseam semantiki ni stadi ya maana.semantiki ni utanzu unaochunguza maana katika lugha ya mwanadamu.wanaendelea kusema semantiki hutafiti maana za mofimu ,mofimu,maneno na tungo kwa hivyo kutokana na fasili hii maana hushugulikiwa katika vitengo au viwango vyote vya lugha ambavyo ni fonolojia,mofolojia na sintaksia.
Mifano a) paka mweusi amepotea
b) mweusi paka amepotea
c) amepotea mweusi paka
katika mifano hii tunaona kwamba sentesi a)ina maana kutokana na kwamba imefuata mpangilio sahihi wa maneno katika tungo na sentensi zilizobaki hazina maana.
Kutokana na sababu kwambva hazijafuata mpangilio ulio sahihi,kwa mantiki hii kwa kuwa semantiki hushugulikie viwango vyote vya lugha,basi hushugulikia pia kiwango cha sintaksia ambapo huangazia maana za tungo.Tungo yoyote ni lazima ilete maana inayokubalika wa wazungumzaji au watumiaji wa lugha husika,kama itakua kinyume basi haitakuwa tungo bali ni orodha ya maneno tuu mfano:
1) Mtoto anacheza mpira uwanjani
2) Mtoto uwanjani mpira anacheza
Tukiangalia kwa mifano hiitunagundua kwamba katika sentensi ya pili haina maana kutokana kuwa na mpangilio mbaya wa maneno.
Kwa hivyo tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa sintaksia haiwezi kutenganizhwa na vitengo vingine vya lugha kwa vile kuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya vipengele hivi vya lugha na kwa hivyo hutegemeana kati ya kipengele kimoja na kingine,kwa mfano,
Huwezi kupata mofolojia (neno) bila bila kupitia ngazi ya sintaksia(sentesi/tungo)bila ya kupitia ngazi ya fonolojia na mofolojialakini vitengo vyote hivi hutawaliwa na kitengo cha semantiki ili kuleta mawasiliano miongoni mwa wazungumzaji.
MAREJEO
1. Habwe J na P.Karanja(2007),Misingi Sarufi ya Kiswahili, Nairobi:phoenix publishers
2. Massamba D.P.B na wenzake(1999)Sarufi miundo ya Kiswahili sanifu,sekondary na vyuo. Dar es salaam:TUKI
3. Rubanza,Y,I1996).Mofolojia Ya Kiswah Dare es salaam;Chuo kikuu Huri Cha Tanzania,
4. Tuki(2004)Kamusi Ya Kiswahili Sanifu: Dare es salaam:TUKI
ELVIS123 answered the question on December 2, 2017 at 08:48
- Mikakati inayotumiwa kukabiliana Na vikwazo vya mawasiliano katika lugha ya pili(Solved)
Mikakati inayotumiwa kukabiliana Na vikwazo vya mawasiliano katika lugha ya pili
Date posted: November 30, 2017. Answers (1)
- Unda nomino mbilimbili kutokana na vitenzi hivi.(Solved)
Unda nomino mbilimbili kutokana na vitenzi hivi.
a)jaribu.
b)chuma
Date posted: November 25, 2017. Answers (1)
- Taja aina mbili za viwakilishi nafsi(Solved)
Taja aina mbili za viwakilishi nafsi
Date posted: November 25, 2017. Answers (1)
- Unda vitenzi kutokana na nomino hizi.
i) Hotuba
ii) Tiba(Solved)
Unda vitenzi kutokana na nomino hizi.
i) Hotuba
ii) Tiba
Date posted: November 25, 2017. Answers (1)
- Bainisha kielezi katika sentensi hii. Wageni hao waliwasili Julai mwaka jana. (Solved)
Bainisha kielezi katika sentensi hii. Wageni hao waliwasili Julai mwaka jana.
Date posted: November 25, 2017. Answers (1)
- Toa mifano miwili miwili kwa sauti zifuatazo: (i) Sauti ghuna ambazo ni vipasuo (ii) Si ghuna ambazo ni vikwamizo.(Solved)
Toa mifano miwili miwili kwa sauti zifuatazo:
i) Sauti ghuna ambazo ni vipasuo.
ii) Si ghuna ambazo ni vikwamizo.
Date posted: November 25, 2017. Answers (1)
- Bainisha matumizi ya’ku’ katika sentensi hii.
Kufaulu kwako kutakuletea heshima ikiwa hukudanganya katika mtihani huo.(Solved)
Bainisha matumizi ya’ku’ katika sentensi hii.
Kufaulu kwako kutakuletea heshima ikiwa hukudanganya katika mtihani huo.
Date posted: November 25, 2017. Answers (1)
- Eleza mtindo unaotumiwa kuainisha ngeli kisha utoe mifano miwili(Solved)
Eleza mtindo unaotumiwa kuainisha ngeli kisha utoe mifano miwili.
Date posted: November 24, 2017. Answers (1)
- Ziandike sayari zote kwa Kiswahili(Solved)
Ziandike sayari zote kwa Kiswahili.
Date posted: November 23, 2017. Answers (1)
- Eleza hatua muhimu zinazofuatwa katika uandishi na usahihishaji wa Insha.(Solved)
Eleza hatua muhimu zinazofuatwa katika uandishi na usahihishaji wa Insha.
Date posted: November 23, 2017. Answers (1)
- Eleza mtindo wa uainishaji wa ngeli.(Solved)
Eleza mtindo wa uainishaji wa ngeli.
Date posted: November 22, 2017. Answers (1)
- Andika tarakimu hii kwa maneno: 10,001.(Solved)
Andika tarakimu hii kwa maneno: 10,001.
Date posted: November 21, 2017. Answers (1)
- Ni kiungo kipi hutoa nyongo katika mwili wa binadamu? Andika wingi wa kiungo hicho(Solved)
Ni kiungo kipi hutoa nyongo katika mwili wa binadamu? Andika wingi wa kiungo hicho.
Date posted: November 21, 2017. Answers (1)
- ISIMUJAMII .Taja na ueleze njia tano zinazochangia maenezi ya lugha ya Kiswahili nchini.(Solved)
ISIMUJAMII
Taja na ueleze njia tano zinazochangia maenezi ya lugha ya Kiswahili nchini.
Date posted: November 20, 2017. Answers (1)
- Eleza matumizi ya vile katika sentensi hii. Vile vile seremala alitengeneza meza.(Solved)
Eleza matumizi ya vile katika sentensi hii.
Vile vile seremala alitengeneza meza.
Date posted: November 20, 2017. Answers (1)
- Akifishe sentensi ifuatayo:Io amekimbia (Solved)
Akifishe sentensi ifuatayo:
Lo amekimbia
Date posted: November 20, 2017. Answers (1)
- Bainisha virai nomino, virai vivumishi, na virai vielezi katika sentensi ifuatayo: Yule mwalimu mwenye ndevu amewasili ukumbini sasa hivi.(Solved)
Bainisha virai nomino, virai vivumishi, na virai vielezi katika sentensi ifuatayo:
Yule mwalimu mwenye ndevu amewasili ukumbini sasa hivi.
Date posted: November 20, 2017. Answers (1)
- Sahihisha sentensi : Mama mwenye alikufa amezikwa katika kaburini.(Solved)
Sahihisha sentensi :
Mama mwenye alikufa amezikwa katika kaburini.
Date posted: November 20, 2017. Answers (1)
- Tofautisha maana ya sentensi zifuatazo: Chakula chote kitaharibika. Chakula chochote kitaharibika.(Solved)
Tofautisha maana ya sentensi zifuatazo:
Chakula chote kitaharibika. Chakula chochote kitaharibika.
Date posted: November 20, 2017. Answers (1)
- Eleza sababu tano za kuchanganya na kubadili ndimi/msimbo.(Solved)
Eleza sababu tano za kuchanganya na kubadili ndimi/msimbo.
Date posted: November 20, 2017. Answers (1)