Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali 1. Huku ulimwengu unapoingia katika teknologia ya tarakilishi na sera ya utandaridhi, ukweli wa mambo ni kuwa akina mama wamezinduka. Suala...

      

Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali
1.
Huku ulimwengu unapoingia katika teknologia ya tarakilishi na sera ya utandaridhi, ukweli wa mambo ni kuwa akina mama wamezinduka. Suala la usawa wa kijinsia limeanza kushamiri kote duniani na ole wake mwanamume yeyote ambaye hajawa tayari kutembea na majira. Lakini hebu tuchunguze jambo hili kwa makini zaidi. Usawa wa jinsia ni nini?

Usawa wa kijinsia ni usawa wa binadamu wote; wawe wake au waume. Usawa huu unapaswa kudhihirika katika kugawa nafasi za kazi, utoaji wa elimu, nafasi za uongozi na nyanja nyinginezo zozote za maisha.

Ubaguzi wa aina yoyote ile hasa dhidi ya mwanamke ni jambo linalokabiliwa na vita vikali sana ulimwenguni kote.

Dahari na dahari, hasa katika jamii za kiafrika, kumekuwa na imani isiyotingisika kuwa mwanamke ni kiumbe duni akilinganishwa na mwanaume. Kwa hivyo mwanamke amekuwa akifanyiwa kila aina ya dhuluma ikiwepo kupigwa, kutukanwa, kudharauliwa, kunyimwa haki zake, kunyimwa heshima na mambo kama hayo. Lakini je, ni kweli kuwa mwanamke ni kiumbe duni asiyefaa kutendewa haki?

Tukichunguza jamii kwa makini tunaweza kuona mara moja kuwa hivyo ni imani potofu isiyo na mashiko yoyote. Ukiimulika familia yoyote ile iliyopiga hatua kimaendeleo, uwezekano mkubwa ni kuwa mume na mke wa familia inayohusika wana ushirikiano mkubwa. Mume anamthamini mke wake na hadiriki kufanya maamuzi muhimu yanayoweza kuathiri maendeleo ya familia bila kumhusisha mke. Mume kama huyo huketi na mkewe, wakishauriana na kufikia uamuzi bora.

Tukitoka katika muktadha wa kifamilia na kumulika ulimwengu wa kazi iwe ni katika afisi za kiserikali au kwenye makampuni binafsi, ukweli ni kwamba kiongozi yeyote yule aliyefaulu katika usimamizi wake mara nyingi huwa na mke nyumbani ambaye wanashauriana kila uchao kuhusu kazi anayofanya hata kama mke hafanyi kazi mahali pale. Hisia na mawaidha anayotoa mke kwa mume wake ni tunu na huenda asiyapate kwingineko kokote hata katika vitabu vya kupigiwa mifano. Hii ni mojawapo ya sababu ambayo huwafanya viongozi wa nchi mbalimbali kupenda sana kuwatambulisha wake na familia zao waziwazi kwa vile wanajua kuwa jamii inathamini sana msingi wa jamii. Kiongozi ambaye hana mke au familia au yule ambaye mke wake hatambuliki, hutiwa mashaka na jamii hata kama ni kiongozi aliye na azma ya kushikilia kazi ngumu ya kuongoza umma.

Tukirudi nyuma kidogo na kupiga darubini mataifa ya mbali, tunaweza kuwaona wanawake mashuhuri walio uongozini ambao hadi waleo unapigiwa mfano. Wanawake mashuhuri waliotoa uongozini ambao hadi waleo unapigiwa mfano. Wanawake hao walisimamia mojawapo ya mataifa yenye uwezo na ushawishi mkubwa zaidi duniani. Ingawa wengi wao sasa wameng’atuka, uongozi wao bado unakumbukwa hata baada ya miaka mingi ya wao kuamua kupumzika, Mifano ni kama: Bi Margaret Thatcher aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza, Bi Bandranaike wa Sri Lanka, Golda Meir wa Israel na wengine wengi katika mataifa kama Indonesia, Ufilipino, Bangladesh, Pakistani na kwingineko.

Katika kufikia tamati, tunapozungumza kuhusu jinsia, hatuna budi kugusia kitafsili masuala nyeti. Kwanza, imani ya kushikilia kikiki tamaduni zisizofaa, ni jambo linalofaa kuchunguzwa kw makini. Kwa mfano, kuna badhi ya jamii ambazo humlazimu mke kurithiwa baada ya kifo cha mumewe. Vile vile baadhi ya jamii za kiafrika zinashikilia kuwa mwanamke hana haki ya kurithi. Kutokana na imani hii, wanawake wengi huishi maisha ya taabu baada ya kutengana na waume zao kwa vile hawana haki ya kurithi chochote kutoka kwa wazazi wao hata kama wazazi hao wana mali nyingi kupindikukia. Mali ya wazazi ni haki ya watoto wa kiume wala si watoto wa kike! Hili ni jambo la kusikitisha mno.

Isitoshe, wanawake hukumbwa na kizingiti kingine wanapojaribu kumiliki mali ya waume zao baada ya waume hao kukata kamba. Sababu ni kuwa, baada ya hao wenda zao kuwekwa kaburini, vita vya umiliki wa mali huanza mara moja na mwishowe yule mke maskini hujikuta hana hata mahali pa kulala sembuse mali waliyochuma na mali yake yote kunyakuliwa na aila ya mumewe . Jambo hili linaonyesha namna tulivyoachwa nyuma na uhalisia wa mambo. Ni lazima jamii izinduke na itoke kwenye kiza hiki chenye maki nzito.

(a) Ina maana gani kusema kuwa wanaume hawana budi “kutembea na majira?”
(b) Kabla ya uzinduzi huu kuhusu usawa wa kijinsia, wanawake wamekuwa wakitendewa dhuluma za kila aina. Taja tatu
(c) Je, ni kwa nini viongozi wengi hupenda kujitambulisha na familia zao?
(d) Je, unaamini kuwa hisia na mawaidha anayotoa mke kwa mume wake ni tunu nahuenda yasipatikane kwingineko? Fafanua
(e) Je licha ya kunyimwa haki yake ya kujiamulia, ni matatizo yapi mengine
yanayoweza kumukumba mke anayelazimishwa kurithiwa

  

Answers


Davis
a)Lazima wakubali mabadiliko/suala kuhusu mabadiliko haliwezi puuziliwa mbali
b)-Kutukanwa
-Kudharauliwa
-Kunyimwa nafasi muhimu maishani kama vile masomo,uongozi.
c)Jamii inadhamini sana msingi wa familia
d)Kwa sababu yatalenga mafanikio ya familia na mume
e)-Kukosa urithi
-Maisha ya dhiki
-Kubaguliwa
-Magonjwa yanayoweza kuangamiza kwa mfano ukimwi.
Githiari answered the question on January 16, 2018 at 12:53


Next: Why must user needs be considered when acquiring new software?
Previous: Taja tofauti iliyopo kati ya sauti /f/ na /v/

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions