Soma kifungu kifuatacho halafu ujibu maswali yanayoifuatia. Watu wengi hawawezi kunywa chai au uji bila kutia sukari. Wanatumia sukari kwa hamu na ghamu bila kutambua kuwa...

      

Soma kifungu kifuatacho halafu ujibu maswali yanayoifuatia.

Watu wengi hawawezi kunywa chai au uji bila kutia sukari. Wanatumia sukari kwa hamu na ghamu bila kutambua kuwa hiyo ni sumu wanayojiongezea mwilini.


Ni ukweli usiopingika kuwa wazee wetu wa jadi waliishi muda mrefu wakiwa na siha njema kuliko sisi. Hii ni kwa sababu waliishi katika kipindi ambacho sukari inayotengenezwa viwandani haikuweko. Iwapo ilikuweko, ilikuwa bidhaa ya wateule wa ungwana kutengenezea vitu kama keki, mahamri na vitumbua. Akina yahe hawangeweza kuigharamia.


Watafiti wa masuala ya afya wamegundua kuwa sukari inayotayarishwa viwandani sasa hivi haina virutubishi vyovyote. Hali kadhalika, utaratibu wa viwandani wa kutayarisha sukari ili iwe nyeupe na kuichuja huharibu virutubishi vinavyoweza kuwa muhimu mwilini. Umuhimu wa sukari wakausaza kuwa kutia ladha tamu tu. Umuhimu huu hauwezi kulinganishwa na madhara yanayoletwa na sukari hii. Baada ya kusagika mwilini, sukari hii huacha masalio ya sidi mwilini yenye sumu inayoathiri siha.

Matumizi ya sukari kwa wingi husababisha madhara mbalimbali mwilini. Huchangia kuoza na kuharibika kwa meno. Sukari nyeupe imehusishwa na ongezeko la maradhi ya kisukari, moyo na hipoglisimoia au upungufu wa sukari mwilini. Matumizi holela ya sukari huleta kipandauso au ugonjwa wa ghafla wa kuumwa na upande mmoja wa kichwa unaoambatana na kichefuchefu, kutapika na matatizo ya kuona. Sukari pia huleta maradhi ya ngozi na figo, pamoja na ongezeko la kemikali iitwayo kolestroli, ambayo ni ufuta unaonata na hutokana na kutoyeyuka kwa mafuta yote mwilini. Kemikali hii inaporundikana moyoni, hufanya mishipa inayotoa damu moyoni na kuisambaza mwilini kuwa myembamba na sugu. Moyo hulazimika kusukuma damu kwa nguvu na huenda ukachoka na kukoma kufanya kazi.


Wataalamu wa lishe bora wamependekeza ulaji wa vyakula kama nafaka, matunda, mboga na miwa ambavyo vimejaa sukari asilia. Fauka ya hayo, sukari inayotokana katika asali ni bora zaidi kwa mwili wa mwanadamu. Asali huwa na sukari asilia, vitamini, madini na amino asidi. Hivi vyote huwa na manufaa mbalimbali mwilini. Asali huupa mwili nishati inayohitajika kuendesha shughuli za viungo.Licha ya hayo, asali huchangamsha mwili. Asali huwa na kemikali ambazo huwasaidia watoto kukua vizuri. Huweza kuzidisha kiwango cha himoglobini, hivyo kupunguza uwezekano wa watoto kuwa na anemia (upungufu wa damu). Asali husaidi katika usagaji wa chakula iwapo itatumiwa kabla ya mlo. Matumizi ya kijiko kimoja cha asali kila siku husaidia mwili kujikinga dhidi ya magonjwa ya kukohoa. Asali husaidia pia kuondoa harufu mbaya kinywani.


Asali inaweza kutumiwa kujipaka. Inapotumika kwa njia hii, hutunza ngozi na kuifanya ing'are, huondoa vipele na ugumu wa ngozi, pamoja na kutibu kule ngozi ilikokatikakatika. Hali kadhalika asali hutibu vidonda. Viwanda vingi vya vipodozi vilevile hutumia asali kama malighafi muhimu katika utengenezaji wa bidhaa hizo.
(a) Pendekeza anwani kwa taarifa uliyosoma.
(b) Taja matumizi mawili ya sukari nyeupe
(c) Eleza madhara matatu ya sukari nyeupe mwilini.
(d) Bainisha aina ya sukari iliyo na manufaa mwilini mwa binadamu na ueleze ni yapi.
(e) Eleza manufaa mawili ya asali:
(i) Ndani ya mwili
(ii)Nje ya mwili

(f)Eleza maana ya msamiati huu kama uliyotumika katika kifungu.
(i) Akina yahe
(ii) Sugu
(iii)Vipodozi

  

Answers


Davis
a)Sukari.
b)-Hutumiwa katika vinywaji k.v chai au uji
-Hutumika kupikia vyakula k.v keki,mahamri
c)-Husababisha maradhi ya kisukari,moyo na hipoglisimia.
-Huleta kipandauso,ugonjwa wa kuumwa na kichwa upande mmoja.
-Husababisha ongezeko la kolestroli,ambayo ni kemikali hatari inapoongezeka mwilini.
-Huleta maradhi ya ngozi na figo.
d)sukari asilia itokanayo na vyakula kama nafaka,matunda,mboga na miwa.
-Sukari itokanayo na asli.Huwa na virutubishi.
e)(i) -Huchangamsha mwili.
-Huupa mwili nishati.
-Husaidia usagaji wa chakula.
-Husaidia mwili kujikinga na maradhi kama homa.
-Huupa mwili madini,vitamini na amino aside. -Huzidisha kiwango cha homoglobini na kupunguza uwezo wa watoto wadogo kupata anemia.
(ii)-Hufanya ngozi kung’ara,huondoa vipele na ugumu wa ngozi.
-Hutibu kule ngozi imekatikakatika na vidonda vinavyotokana na kuchomeka.
f)(i) Watu maskini,wa tabaka la nchini.
(ii) Ngumu.
(iii) Bidhaa za kurembesha k.v poda,wanja,mafuta
Githiari answered the question on January 23, 2018 at 14:52


Next: A bubble of soap blown to the wider end of a funnel,When the top is left open the bubbles flatten to a film which rises...
Previous: Highlight the importance of wheat farming to the Kenyan economy

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Ukifuata utratibu unaokubalika, onyesha hatua sita za uwasilishaji wa vitendawili. (Solved)

    Ukifuata utratibu unaokubalika, onyesha hatua sita za uwasilishaji wa vitendawili.

    Date posted: January 19, 2018.  Answers (1)

  • Huku ukitolea mifano ya kipera husika, fafanua dhima za maghani.(Solved)

    Huku ukitolea mifano ya kipera husika, fafanua dhima za maghani.

    Date posted: January 19, 2018.  Answers (1)

  • Je, miviga ina upungufu gani?(Solved)

    Je, miviga ina upungufu gani

    Date posted: January 17, 2018.  Answers (1)

  • Orodhesha sherehe nne za jamii yako zinazohusishwa na miviga (Solved)

    Orodhesha sherehe nne za jamii yako zinazohusishwa na miviga

    Date posted: January 17, 2018.  Answers (1)

  • Fafanua kikamilifu dhana zifuatazo za fasihi simulizi i) Nyiso ii) Mbolezi iii) Hodiya iv) Bembelezi v) Sifo(Solved)

    Fafanua kikamilifu dhana zifuatazo za fasihi simulizi
    i) Nyiso
    ii) Mbolezi
    iii) Hodiya
    iv) Bembelezi
    v) Sifo

    Date posted: January 17, 2018.  Answers (1)

  • Andika katika usemi wa taarifa “Karibu Bakari, tafadhali kaa”, Maimuna alisema. “Asante, je, habari za nyumbani?” Bakari aliuliza(Solved)

    Andika katika usemi wa taarifa
    “Karibu Bakari, tafadhali kaa”, Maimuna alisema. “Asante, je, habari za nyumbani?” Bakari aliuliza

    Date posted: January 17, 2018.  Answers (1)

  • Andika katika hali ya kutendewa: Kuku hawa wamemsumbua Sabina kwa muda mrefu.(Solved)

    Andika katika hali ya kutendewa:
    Kuku hawa wamemsumbua Sabina kwa muda mrefu.

    Date posted: January 17, 2018.  Answers (1)

  • Andika kwa wingi Wimbi hilo la maji lilimhofisha mvuvi akashindwa kutupa wavu wake majini. (Solved)

    Andika kwa wingi
    Wimbi hilo la maji lilimhofisha mvuvi akashindwa kutupa wavu wake majini.

    Date posted: January 17, 2018.  Answers (1)

  • Andika upya sentensi ifuatayo ukitumia virejeshi vya tamati: Mwanafunzi anayefanikiwa maishani ni yule anayesoma kwa bidii na pia anayewatii wazazi wake. (Solved)

    Andika upya sentensi ifuatayo ukitumia virejeshi vya tamati:
    Mwanafunzi anayefanikiwa maishani ni yule anayesoma kwa bidii na pia anayewatii wazazi wake.

    Date posted: January 16, 2018.  Answers (1)

  • Onyesha chagizo katika sentensi ifuatayo Watu wanne walipeperushwa juu kwa juu na upepo mkali(Solved)

    Onyesha chagizo katika sentensi ifuatayo
    Watu wanne walipeperushwa juu kwa juu na upepo mkali

    Date posted: January 16, 2018.  Answers (1)

  • Unda nomino kutokana na kivumishi:refu(Solved)

    Unda nomino kutokana na kivumishi:refu

    Date posted: January 16, 2018.  Answers (1)

  • Akifisha Mtume asimame nusura aingie kwenye shimo la taka.(Solved)

    Akifisha
    Mtume asimame nusura aingie kwenye shimo la taka.

    Date posted: January 16, 2018.  Answers (1)

  • Sahihisha: Siku hizi mahitaji imezidi na pesa haitoshi.(Solved)

    Sahihisha
    Siku hizi mahitaji imezidi na pesa haitoshi.

    Date posted: January 16, 2018.  Answers (1)

  • Sahihisha Ndegwa alipeana kalamu yake kwa mwanafunzi.(Solved)

    Sahihisha
    Ndegwa alipeana kalamu yake kwa mwanafunzi.

    Date posted: January 16, 2018.  Answers (1)

  • Andika kwa usemi halisi: Yule mshukiwa aliyekamatwa na polisi alisema kuwa papo hapo ndipo alipoficha ule mkufu. (Solved)

    Andika kwa usemi halisi:
    Yule mshukiwa aliyekamatwa na polisi alisema kuwa papo hapo ndipo alipoficha ule mku

    Date posted: January 16, 2018.  Answers (1)

  • Taja tofauti iliyopo kati ya sauti /f/ na /v/(Solved)

    Taja tofauti iliyopo kati ya sauti /f/ na /v/

    Date posted: January 16, 2018.  Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali 1. Huku ulimwengu unapoingia katika teknologia ya tarakilishi na sera ya utandaridhi, ukweli wa mambo ni kuwa akina mama wamezinduka. Suala...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali
    1.
    Huku ulimwengu unapoingia katika teknologia ya tarakilishi na sera ya utandaridhi, ukweli wa mambo ni kuwa akina mama wamezinduka. Suala la usawa wa kijinsia limeanza kushamiri kote duniani na ole wake mwanamume yeyote ambaye hajawa tayari kutembea na majira. Lakini hebu tuchunguze jambo hili kwa makini zaidi. Usawa wa jinsia ni nini?

    Usawa wa kijinsia ni usawa wa binadamu wote; wawe wake au waume. Usawa huu unapaswa kudhihirika katika kugawa nafasi za kazi, utoaji wa elimu, nafasi za uongozi na nyanja nyinginezo zozote za maisha.

    Ubaguzi wa aina yoyote ile hasa dhidi ya mwanamke ni jambo linalokabiliwa na vita vikali sana ulimwenguni kote.

    Dahari na dahari, hasa katika jamii za kiafrika, kumekuwa na imani isiyotingisika kuwa mwanamke ni kiumbe duni akilinganishwa na mwanaume. Kwa hivyo mwanamke amekuwa akifanyiwa kila aina ya dhuluma ikiwepo kupigwa, kutukanwa, kudharauliwa, kunyimwa haki zake, kunyimwa heshima na mambo kama hayo. Lakini je, ni kweli kuwa mwanamke ni kiumbe duni asiyefaa kutendewa haki?

    Tukichunguza jamii kwa makini tunaweza kuona mara moja kuwa hivyo ni imani potofu isiyo na mashiko yoyote. Ukiimulika familia yoyote ile iliyopiga hatua kimaendeleo, uwezekano mkubwa ni kuwa mume na mke wa familia inayohusika wana ushirikiano mkubwa. Mume anamthamini mke wake na hadiriki kufanya maamuzi muhimu yanayoweza kuathiri maendeleo ya familia bila kumhusisha mke. Mume kama huyo huketi na mkewe, wakishauriana na kufikia uamuzi bora.

    Tukitoka katika muktadha wa kifamilia na kumulika ulimwengu wa kazi iwe ni katika afisi za kiserikali au kwenye makampuni binafsi, ukweli ni kwamba kiongozi yeyote yule aliyefaulu katika usimamizi wake mara nyingi huwa na mke nyumbani ambaye wanashauriana kila uchao kuhusu kazi anayofanya hata kama mke hafanyi kazi mahali pale. Hisia na mawaidha anayotoa mke kwa mume wake ni tunu na huenda asiyapate kwingineko kokote hata katika vitabu vya kupigiwa mifano. Hii ni mojawapo ya sababu ambayo huwafanya viongozi wa nchi mbalimbali kupenda sana kuwatambulisha wake na familia zao waziwazi kwa vile wanajua kuwa jamii inathamini sana msingi wa jamii. Kiongozi ambaye hana mke au familia au yule ambaye mke wake hatambuliki, hutiwa mashaka na jamii hata kama ni kiongozi aliye na azma ya kushikilia kazi ngumu ya kuongoza umma.

    Tukirudi nyuma kidogo na kupiga darubini mataifa ya mbali, tunaweza kuwaona wanawake mashuhuri walio uongozini ambao hadi waleo unapigiwa mfano. Wanawake mashuhuri waliotoa uongozini ambao hadi waleo unapigiwa mfano. Wanawake hao walisimamia mojawapo ya mataifa yenye uwezo na ushawishi mkubwa zaidi duniani. Ingawa wengi wao sasa wameng’atuka, uongozi wao bado unakumbukwa hata baada ya miaka mingi ya wao kuamua kupumzika, Mifano ni kama: Bi Margaret Thatcher aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza, Bi Bandranaike wa Sri Lanka, Golda Meir wa Israel na wengine wengi katika mataifa kama Indonesia, Ufilipino, Bangladesh, Pakistani na kwingineko.

    Katika kufikia tamati, tunapozungumza kuhusu jinsia, hatuna budi kugusia kitafsili masuala nyeti. Kwanza, imani ya kushikilia kikiki tamaduni zisizofaa, ni jambo linalofaa kuchunguzwa kw makini. Kwa mfano, kuna badhi ya jamii ambazo humlazimu mke kurithiwa baada ya kifo cha mumewe. Vile vile baadhi ya jamii za kiafrika zinashikilia kuwa mwanamke hana haki ya kurithi. Kutokana na imani hii, wanawake wengi huishi maisha ya taabu baada ya kutengana na waume zao kwa vile hawana haki ya kurithi chochote kutoka kwa wazazi wao hata kama wazazi hao wana mali nyingi kupindikukia. Mali ya wazazi ni haki ya watoto wa kiume wala si watoto wa kike! Hili ni jambo la kusikitisha mno.

    Isitoshe, wanawake hukumbwa na kizingiti kingine wanapojaribu kumiliki mali ya waume zao baada ya waume hao kukata kamba. Sababu ni kuwa, baada ya hao wenda zao kuwekwa kaburini, vita vya umiliki wa mali huanza mara moja na mwishowe yule mke maskini hujikuta hana hata mahali pa kulala sembuse mali waliyochuma na mali yake yote kunyakuliwa na aila ya mumewe . Jambo hili linaonyesha namna tulivyoachwa nyuma na uhalisia wa mambo. Ni lazima jamii izinduke na itoke kwenye kiza hiki chenye maki nzito.

    (a) Ina maana gani kusema kuwa wanaume hawana budi “kutembea na majira?”
    (b) Kabla ya uzinduzi huu kuhusu usawa wa kijinsia, wanawake wamekuwa wakitendewa dhuluma za kila aina. Taja tatu
    (c) Je, ni kwa nini viongozi wengi hupenda kujitambulisha na familia zao?
    (d) Je, unaamini kuwa hisia na mawaidha anayotoa mke kwa mume wake ni tunu nahuenda yasipatikane kwingineko? Fafanua
    (e) Je licha ya kunyimwa haki yake ya kujiamulia, ni matatizo yapi mengine
    yanayoweza kumukumba mke anayelazimishwa kurithiwa

    Date posted: January 16, 2018.  Answers (1)

  • Sababu za kubadilisha msimbo na athari zake(Solved)

    Sababu za kubadilisha msimbo na athari zake.

    Date posted: January 13, 2018.  Answers (1)

  • Eleza hatua ambazo mwanamke amechukua kujikomboa(Solved)

    Eleza hatua ambazo mwanamke amechukua kujikomboa

    Date posted: January 2, 2018.  Answers (1)

  • Taja aina mbili za mofimu na kwa kila toa mfano(Solved)

    Taja aina mbili za mofimu na kwa kila toa mfano

    Date posted: December 29, 2017.  Answers (1)