Fafanua mjukumu ya elimu na dini katika jamii kwa mujibu wa riwaya: Kidagaa Kimemwozea.

      

Fafanua mjukumu ya elimu na dini katika jamii kwa mujibu wa riwaya:
Kidagaa Kimemwozea.

  

Answers


gregory
? Elimu inasaidia kuelezea hisia za mtu kupitia maandishi. Mfano - Amani
ameandika mswada kuonyesha msimamo wake katika masuala tofautiElimu
iliyosisitizwa ni elimu ya kujielewa. Elimu ya kujua mtu atoka wapi na
anaelekea wapi kwa mujibu wa Amani. Elimu imesawiriwa kuwa muhimu
licha ya utajiri na kutosheka maishani. Baada ya muda mrefu, Amani
anarudi chuoni na kupata shahada ya kwanza katika Fasihi na Falsafa.
Elimu ni njia ya kujipatia heshima na umaarufu. Nasaba Bora alimheshimu
ndugu yake kwa uwezo wake katika lugha. Hakupenda wakati ambapo
inamlazimu kusoma hotuba kwa kiingereza asichokielewa
? Wasio na elimu wanabaki kutaabika. Mfano Chwechwe Makweche baada
ya kuacha masomo katika darasa la saba na kuwa mchezaji shupavu,
analemewa na maisha baada ya kuvunjika pfupaja la mguu.
? Elimu imetumiwa kama chombo cha kuwakweza baadhi ya raia katika
madaraka - kama Majisifu anapata kazi kutokana na elimu yake.
? Elimu pia imetumiwa kama chombo cha mapinduzi kwa kutetea haki za
wanyonge. Mfano - Madhubuti anapomaliza masomo yak Urusi anaungana
na Amani kuleta mabadiliko Sokomoko.
? Imani katika dini inajitokeza ambapo kila linapojitokeza jambo mbaya watu
hukimbilia dini.
? Kwa upande mwingine dini imebainishwa kama chombo cha kuadilisha.
Mfano: babake Nasaba Bora na Majisifu aliwalea kwa mwongozo wa bibilia
huku akiwasihi waishi kwa umoja na upendo.
? Dini pia huweza kutumiwa kama hifadhi ya maovu. Kwa mujibu wa
Majisifu maovu mengi kama vile mauaji hufanywa katika jina la Mungu
kutokana na unafiki. Dini ina jukumu la kuwapoza wanaomboleza. - Dini
imetekeleza jukumu la kuunganisha familia pamoja mfano: Babake Nasaba
Bora alihakikisha familia yake imeunganishwa na dini.
gregorymasila answered the question on February 6, 2018 at 07:00


Next: Outline the steps to follow when mending a gaping seam on an apron.
Previous: Jadili umuhimu wa kinachotafutwa katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions