Jadili umuhimu wa kinachotafutwa katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

      

Jadili umuhimu wa kinachotafutwa katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

  

Answers


gregory
? Imani anatafuta haki ya kunyimwa malezi ya wazazi wake waliouliwa
kinyama. Imani anatafuta haki ya familia yake iliyonyanganywa shamba
lao.
? Amani anatafuta haki ya Ami yake Yusufu.
? DJ anatafuta haki baada ya kushambuliwa na jibwa lake Nasaba Bora.
? Amani anatafuta haki ya mswada uiiokataliwa na wachapishaji na baadaye
kuchapishwa kwa jina la mtu mwingine.
? Chwechwe Makweche anatafuta haki ya kuumia michezoni bila kufidiwa.
? Watoto wa Majisifu wanalilia haki ya kuishi kama binadamu wengine licha
ya ulemavu wao. Amani anatafuta haki ya kudhulumiwa na mtemi Nasaba
Bora kwa kizingizio kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mkewe Bi
Zuhura. Amani atafuta haki ya kujua waliokuwa wazazi wa kitoto Uhuru
baada ya yeye kulazimishwa kukilea licha ya kuwa hakuwa babake. Amani
na Imani wanatafuta haki ya kufungwa kwa kizingizio kuwa walimwuua
mtoto Uhuru. Wanafunzi wa mwalimu Majisifu wanatafuta haki ya kufunzwa
vyema baada ya Mwalimu wao kutohudhuria shule kwa muda mrefu. Yusufu
anatafuta haki baada ya kusingiziwa kumwuua Chichiri Hamadi.
? Raia wa Sokomoko wanatafuta haki dhidi ya Nasaba Bora anayewapokonya
ardhi, mali, mabiruti na wake wao.
? Wafungwa wanatafuta haki kwa kukosa kufikishwa mahakamani.
? Waandishi wengi chipukizi kama Amani wanatafuta haki ya kazi zao baada
ya kuibiwa miswada yao na akina Majisifu.
gregorymasila answered the question on February 6, 2018 at 07:01


Next: Fafanua mjukumu ya elimu na dini katika jamii kwa mujibu wa riwaya: Kidagaa Kimemwozea.
Previous: "Anwani Mstahiki Meya ni kinaya." Jadili ukweli wa kauli hii kwa kurejelea tamthilia.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions