"Anwani Mstahiki Meya ni kinaya." Jadili ukweli wa kauli hii kwa kurejelea tamthilia.

      

"Anwani Mstahiki Meya ni kinaya." Jadili ukweli wa kauli hii
kwa kurejelea tamthilia.

  

Answers


gregory
Anwani Mstahiki Meya ni kinaya kw vile
anayeitwa Mstahiki anatakiwa kuwa mtu wa kuheshimiwa. Kama kiongozi
heshima hutokana na uongozi bora unaowafanya raia kuonea fahari uongozi wa
kiongizi wao. Hata hivyo, Mstahiki Meya hakustahiki kuitwa kiongozi kwa sababu
zifuatazo:
? Wafanyakazi wa mji wanaendelea kufanya kazi kwa muda mrefu bila
mshahara.Hospitali hazina dawa na wagonjwa wanakufa kutokana na
magonjwa yanayoweza kutibiwa kwa urahisi,
? Kuna njaa kiasi kwamba wafanya kazi wake wanakula mabaki ya chakula
kutoka nyumbani mwake na kuugua.
? Anapanga na Bili jinsi wataipunja baraza kupitia kesi ya mwenye kandarasi
anayedai haki yake.
? Anadanganya kuwa ameagiza dawa kutoka ng'ambo huku akijua fika kuwa
hajaagiza.
? Anawatenga wanaodhamiria kumsaidia kuongoza vizuri kama vile Siki na
Diwani III.
? Anaharibu aasasi za serikali kama vile hospitali huku mkewe akienda
ng'ambo kujifungua.
? Anawaita viongozi wa wafanya kazi ofisini mwake akijua kuwa hakuwa na
mpango wa kushughulikia malalamiko yao.
? Badala ya kusuluhisha matatizo yanayokumba mji wa Cheneo kwa
majadiliano, anaamua kutumia vyombo vya utawala kunyamazisha
upinzani.
? Ananyakua ardhi ya umma na kujigawia pamoja na marafiki zake hasa Bili.
? Anaidhinisha kutotozwa kodi kwa madiwani huku wafanya kazi wa
kawaida wakilazimishwa kufanya kazi kwa miezi mingi bila mshahara
kutokanan na nakisi ya kifedha.
? Anashiriki katika wizi wa fimbo ya Meya ishara ya mamlaka ya cheo chake.
? Anaingilia mambo yasiyo na maana yoyote kama vile ukubwa wa mayai
aliyopikiwa badala ya kushughulikia matatizo katika Cheneo kwa busara
ifaayo.
? Anakiri kudanganywa na Bili na kuwategemea madiwani ambao hawakuwa
na ujuzi wa kutosha.
? Anawahonga madiwani ili wamuunge mkono badala ya kuwatambua kama
wawakilishi wa wananchi watakaompa ukweli wa mambo ili kuongoza
anavyostahili.
? Anamhonga mhubiri ili aendelee kumwombea yeye badala ya kubadili
uongozi wake unaoendelea kuzorotesha hali mjini Cheneo.
? Anaendelea kumlipa Bili kwa huduma isiyo na manufaa yoyote. Bili alijua
kuwa alikuwa akimdanganya Meya na mambo yanapoharibika anatoroka
pasipo kwaheri.
? Anapogundua alidanganywa mambo yalikuwa yameharibika kiasi cha
kutobadilika.
? Anahakikisha kuwa masiahi ya kiafya ya wenye mamlaka
yameshughulikiwa huku raia wake wakugua na kufa kwa ukosefu wa
huduma hospitalini.
? Anautambua urafiki wa kusifiwa zaidi ya utaaiamu. Diwani III na Siki
hawakutambuliwa kwa vile katika kumwmbia Meya ukweli walionekanan
kama maadui wake,
? Anakosa kufikiria na kufanya maamuzi huru na kutokana na haya
anadanganywa na waliojali masilahi yao kama Bili na Diwani ! na Diwani II.
gregorymasila answered the question on February 6, 2018 at 07:03


Next: Jadili umuhimu wa kinachotafutwa katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
Previous:  "... dawa ya adui ni kummegea unachokula." (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Jadili jinsi dawa inayorejelewa inavyozorotesha hali katika mji wa Cheneo.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions