"... dawa ya adui ni kummegea unachokula." (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Jadili jinsi dawa inayorejelewa inavyozorotesha hali katika mji wa Cheneo.

      

"... dawa ya adui ni kummegea unachokula."
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Jadili jinsi dawa inayorejelewa inavyozorotesha hali katika mji wa
Cheneo.

  

Answers


gregory
Eleza muktadha wa dondoo hili.
? Anayesema maneno haya ni Bili akimwambia Mstahiki Meya. Wamo ofistni
mwake Mstahki Meya. Walikuwa wakizugumza kuhusu mwanakandarasi
aliyekuwa ameshtaki Baraza akidai pesa zake.
(b) Jadili jinsi dawa inayorejelewa inavyozorotesha hali katika mji wa
Cheneo.
? Dawa inayorejelewa ni ufisadi. Ufisadi umezorotesha hali katika Cheneo
kwa njia mbalimbali kama:
? Meya anaidhinisha kuongezewa mishahara kwa madiwani ili wamuunge
mkono. Hazina ya baraza inamomonyoka zaidi. Madiwani hawampi
ushauri wa kweli na uongozi unaanguka.
? Meya anamgawia Bili viwanja vinne. Bili anaishia kumpa ushauri wa
kuporosha. Meya anaifisidi hazina ya baraza kwa kumpeleka Bili na familia
yake kwa burudani.
? Meya anaunda kamati nyingi ili kuwahonga madiwani wanaomuunga
mkono. Anaishia kushauriwa kufanya maamuzi yasiyo ya busara,
anakataa kuwasikiliza wafanya kazi, mji umejaa urundo, wageni wanakosa
kufika na uongozi wa Meya unaanguka.
? Meya anamlipa Bili kwa huduma ambayo kwa ukweli hajatoa. Huu
unakuwa mzigo kwa hazina ya baraza.
? Meya anaidhinisha Diwani I na Diwani II kulipwa 'overtime' na hali
hawajafanya lolote. Anaishia kumpa Bili upenyu wa kushauri wauze fimbo
ya Meya.
? Meya anaidhinisha kutotozwa kodi kwa madiwani kwa kutaka wamuunge
mkono. Hili linalinyima baraza pato na kuzidisha nakisi ya fedha.
? Meya anamhonga mhubiri kwa sadaka ili aendelee kumwombea. Mhubiri
anashindwa kumkosoa Meya, uongozi unaanguka.
? Bili anamshauri Meya amwambie mwanakandarasi alishtaki baraza ili
apewe fidia kwa kukatizwa kwa kandarasi. Meya anapata fungu lake pia.
? Raia wanachukua hongo kutoka kwa viongozi. Wanawachagua na
kuendeleza uongozi mbaya. Meya anamwambia Siki kuwa hata akitaka
uongozi mara nne, tano na sita atapewa kwani ana akili na uwezo wa
ushawishi.
? Ufisadi unamfanya Meya kumshirikisha Bili katika maamuzi muhimu ya
Baraza, na hali Bili si mfanya kazi wa Baraza. Bili anaishia kumporosha
Meya.
? Ufisadi unamfanya Diwani I (Bwana Usalama) kufanikisha wizi wa fimbo ya
Meya. Anatoka nayo kasha anatangaza kwamba kulitokea rabsha ikaibwa.
? Ufisadi unamfanya Meya, Diwani 1, Diwani II na Bili kutotoa siri kuhusu
nyama ya kuiba fimbo ya Meya linapata hasara.
gregorymasila answered the question on February 6, 2018 at 07:05


Next: "Anwani Mstahiki Meya ni kinaya." Jadili ukweli wa kauli hii kwa kurejelea tamthilia.
Previous: Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Kilio cha Lugha Ni wimbo najiimbia, nijiliwaze Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi Lugha ya...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions