Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Kilio cha Lugha Ni wimbo najiimbia, nijiliwaze Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi Lugha ya...

      

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Kilio cha Lugha
Ni wimbo najiimbia, nijiliwaze
Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi
Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi
Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia
Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa
Hamna nami imani, wala kupanga siasa,
Mwasema sayansini, siku ningalitosa,
Mwanambia nikotosa, kuiva sijafika.
Ela muelewe sana, Maamuma na Imamu,
Mulipokuwa vijana, kwenu nilikuwa timamu,
Sasa mumesoma sana, mwaniona ni haramu,
Mujue kuwa dawamu, utumwa mwauridhia.
Mzaliwapo mwalia, 'maa', maneno ya kwanza,
Lugha munayokulia, ya mama zetu ya kwanza,
Wa lugha muwedoria, muweze na kuikuza,
Sio kujipendekeza, uzungu kuigiza.
Majira ya ukoloni, ukombozi kusambaza,
Lugha mulithamini, Kiswahili kufukiza,
Hata kule risavuni, kizungu hanikuwaza,
Sasa mbona mwanibeza, mbali mwanitupilia?
Sayansi sio asili, msamiatiwe sinao,
Sayansi yataka mbali, msamiati ni wa hao
Nitakuwa Kiswahili, kiomba majina yao
Lugha kujikuza kwao, huomba linalofaa.
Enyi viongozi wetu ipangeni nadharia,
Kujenga siasa yetu, tuzidi kuwa huria
Lugha hata 'mbusha watu, tuche kuriaria,
Sifa ni kwa chake mtu, cha mwenzi hutoringia.
Utajiri wangu hasa, nikiwatajia wote,
Msamiati huwa, ni wa Afrika yote,
Na methali za kuasa, nahau na ngeli zote,
Na nisemwapo popote, ujumbe hukamilika.
Afrika ndipo petu, pa wabantu halisi,
Baba na mama ni Bantu, shina la wangu ukwasi,
Warabu na wengi wetu, sio wangu Adinasi
Kwao 'meomba kiasi, ili kujizidisha.
Mfumo mpya hongera, wa elimu humu Kenya,
Lugha takuwa imara, ukabila tutafinya,
Kiswahili ni ibara, kila mtu kiimanya,
Methali imetuonya, mtumwa si mwasilia
Tamati lugha yalia, yabaguliwa bayana,
Kukua imeridhia, msamiati kufana,
Wengine wataijulia, kwa marefu na mapana,
Lugha yenu ya maana, mwaipuuza yalia.
(a) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu.
(b) Kwa kutoa hoja ime, eleza kwa nini shairi hili likaitwa kilio cha lugha.
(c) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari.
(d) Eleza toni ya shairi hili.
(e) Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano milatu.
F)Bainisha nafsineni katika shairi.
G)Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa shairi.
(i) nasongwa
(ii) kuriaria
(iii) adinasi

  

Answers


gregory
(a) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu.
? Tarbia - mishororo mine katika kila mshororo.
(b) Kwa kutoa hoja ime, eleza kwa nini shairi hili likaitwa kilio cha lugha.
? Kiswahili chapuuzwa kuwa hakijakomma
? Waliosoma hawakienzi Kiswahili wakifikiria hawana haja na lugha hii.
? Viongozi hawakienzi Kiswahili katika kujenga siasa.
? Kiswahili hakipewi nafasi.
? Waafrika hawaoni utajiri wa Kiswahili kuwa na msamiati kutoka aarika
nzima.
(c) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari.
? Kila mmoja aelewe
? Mlipokuwa vijana mlikitumia Kiswahili.
? Baada ya kusoma mmeanza kukidharau
? Kwa kufanya hivi mjue mwafurahia utumwa.
(d) Eleza toni ya shairi hili.
? Toni ya huzuni - lugha ya mtu mweusi chalia.
(e) Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano milatu.
? Inkisari - kiwa - nikiwa
? Mazida - muelewe - mwelewe
? Tabdila - mulithamini - mlithamini.
? Kuboronga lugha - hamna name imani - hamna imani name.
? Utuhozi - risaruni.
(f) Bainisha nafsineni katika shairi.
Hafsheni
? Mtetezi wa lugha ya Kiswahili anayelalamikia kupuuzwa kwa Kiswahili.
? Aliyezinduka na kutambua umuhimu wa Kiswahili barni Afrika.
(g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa shairi.
(i) nasongwa
? Nasagwa – naumia
(ii) kuriaria
? kuzurura, kurandaranda
(iii) adinasi
? binadamu
gregorymasila answered the question on February 6, 2018 at 07:13


Next:  "... dawa ya adui ni kummegea unachokula." (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Jadili jinsi dawa inayorejelewa inavyozorotesha hali katika mji wa Cheneo.
Previous: Ili kuweza kufanikisha uwasilishaji wa utanzu wa nyimbo kwa hadhira eleza mambo anayohitaji mwimbaji.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions