Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Kilio cha Lugha
Ni wimbo najiimbia, nijiliwaze
Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi
Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi
Lugha ya...(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Kilio cha Lugha
Ni wimbo najiimbia, nijiliwaze
Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi
Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi
Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia
Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa
Hamna nami imani, wala kupanga siasa,
Mwasema sayansini, siku ningalitosa,
Mwanambia nikotosa, kuiva sijafika.
Ela muelewe sana, Maamuma na Imamu,
Mulipokuwa vijana, kwenu nilikuwa timamu,
Sasa mumesoma sana, mwaniona ni haramu,
Mujue kuwa dawamu, utumwa mwauridhia.
Mzaliwapo mwalia, 'maa', maneno ya kwanza,
Lugha munayokulia, ya mama zetu ya kwanza,
Wa lugha muwedoria, muweze na kuikuza,
Sio kujipendekeza, uzungu kuigiza.
Majira ya ukoloni, ukombozi kusambaza,
Lugha mulithamini, Kiswahili kufukiza,
Hata kule risavuni, kizungu hanikuwaza,
Sasa mbona mwanibeza, mbali mwanitupilia?
Sayansi sio asili, msamiatiwe sinao,
Sayansi yataka mbali, msamiati ni wa hao
Nitakuwa Kiswahili, kiomba majina yao
Lugha kujikuza kwao, huomba linalofaa.
Enyi viongozi wetu ipangeni nadharia,
Kujenga siasa yetu, tuzidi kuwa huria
Lugha hata 'mbusha watu, tuche kuriaria,
Sifa ni kwa chake mtu, cha mwenzi hutoringia.
Utajiri wangu hasa, nikiwatajia wote,
Msamiati huwa, ni wa Afrika yote,
Na methali za kuasa, nahau na ngeli zote,
Na nisemwapo popote, ujumbe hukamilika.
Afrika ndipo petu, pa wabantu halisi,
Baba na mama ni Bantu, shina la wangu ukwasi,
Warabu na wengi wetu, sio wangu Adinasi
Kwao 'meomba kiasi, ili kujizidisha.
Mfumo mpya hongera, wa elimu humu Kenya,
Lugha takuwa imara, ukabila tutafinya,
Kiswahili ni ibara, kila mtu kiimanya,
Methali imetuonya, mtumwa si mwasilia
Tamati lugha yalia, yabaguliwa bayana,
Kukua imeridhia, msamiati kufana,
Wengine wataijulia, kwa marefu na mapana,
Lugha yenu ya maana, mwaipuuza yalia.
(a) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu.
(b) Kwa kutoa hoja ime, eleza kwa nini shairi hili likaitwa kilio cha lugha.
(c) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari.
(d) Eleza toni ya shairi hili.
(e) Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano milatu.
F)Bainisha nafsineni katika shairi.
G)Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa shairi.
(i) nasongwa
(ii) kuriaria
(iii) adinasi
Date posted: February 6, 2018. Answers (1)
Jadili dhima ya fasihi katika jamii(Solved)
Jadili dhima ya fasihi katika jamii
Date posted: February 6, 2018. Answers (1)
Soma kifungu kifuatacho halafu ujibu maswali yanayoifuatia.
Watu wengi hawawezi kunywa chai au uji bila kutia sukari. Wanatumia sukari kwa hamu na ghamu bila kutambua kuwa...(Solved)
Soma kifungu kifuatacho halafu ujibu maswali yanayoifuatia.
Watu wengi hawawezi kunywa chai au uji bila kutia sukari. Wanatumia sukari kwa hamu na ghamu bila kutambua kuwa hiyo ni sumu wanayojiongezea mwilini.
Ni ukweli usiopingika kuwa wazee wetu wa jadi waliishi muda mrefu wakiwa na siha njema kuliko sisi. Hii ni kwa sababu waliishi katika kipindi ambacho sukari inayotengenezwa viwandani haikuweko. Iwapo ilikuweko, ilikuwa bidhaa ya wateule wa ungwana kutengenezea vitu kama keki, mahamri na vitumbua. Akina yahe hawangeweza kuigharamia.
Watafiti wa masuala ya afya wamegundua kuwa sukari inayotayarishwa viwandani sasa hivi haina virutubishi vyovyote. Hali kadhalika, utaratibu wa viwandani wa kutayarisha sukari ili iwe nyeupe na kuichuja huharibu virutubishi vinavyoweza kuwa muhimu mwilini. Umuhimu wa sukari wakausaza kuwa kutia ladha tamu tu. Umuhimu huu hauwezi kulinganishwa na madhara yanayoletwa na sukari hii. Baada ya kusagika mwilini, sukari hii huacha masalio ya sidi mwilini yenye sumu inayoathiri siha.
Matumizi ya sukari kwa wingi husababisha madhara mbalimbali mwilini. Huchangia kuoza na kuharibika kwa meno. Sukari nyeupe imehusishwa na ongezeko la maradhi ya kisukari, moyo na hipoglisimoia au upungufu wa sukari mwilini. Matumizi holela ya sukari huleta kipandauso au ugonjwa wa ghafla wa kuumwa na upande mmoja wa kichwa unaoambatana na kichefuchefu, kutapika na matatizo ya kuona. Sukari pia huleta maradhi ya ngozi na figo, pamoja na ongezeko la kemikali iitwayo kolestroli, ambayo ni ufuta unaonata na hutokana na kutoyeyuka kwa mafuta yote mwilini. Kemikali hii inaporundikana moyoni, hufanya mishipa inayotoa damu moyoni na kuisambaza mwilini kuwa myembamba na sugu. Moyo hulazimika kusukuma damu kwa nguvu na huenda ukachoka na kukoma kufanya kazi.
Wataalamu wa lishe bora wamependekeza ulaji wa vyakula kama nafaka, matunda, mboga na miwa ambavyo vimejaa sukari asilia. Fauka ya hayo, sukari inayotokana katika asali ni bora zaidi kwa mwili wa mwanadamu. Asali huwa na sukari asilia, vitamini, madini na amino asidi. Hivi vyote huwa na manufaa mbalimbali mwilini. Asali huupa mwili nishati inayohitajika kuendesha shughuli za viungo.Licha ya hayo, asali huchangamsha mwili. Asali huwa na kemikali ambazo huwasaidia watoto kukua vizuri. Huweza kuzidisha kiwango cha himoglobini, hivyo kupunguza uwezekano wa watoto kuwa na anemia (upungufu wa damu). Asali husaidi katika usagaji wa chakula iwapo itatumiwa kabla ya mlo. Matumizi ya kijiko kimoja cha asali kila siku husaidia mwili kujikinga dhidi ya magonjwa ya kukohoa. Asali husaidia pia kuondoa harufu mbaya kinywani.
Asali inaweza kutumiwa kujipaka. Inapotumika kwa njia hii, hutunza ngozi na kuifanya ing'are, huondoa vipele na ugumu wa ngozi, pamoja na kutibu kule ngozi ilikokatikakatika. Hali kadhalika asali hutibu vidonda. Viwanda vingi vya vipodozi vilevile hutumia asali kama malighafi muhimu katika utengenezaji wa bidhaa hizo.
(a) Pendekeza anwani kwa taarifa uliyosoma.
(b) Taja matumizi mawili ya sukari nyeupe
(c) Eleza madhara matatu ya sukari nyeupe mwilini.
(d) Bainisha aina ya sukari iliyo na manufaa mwilini mwa binadamu na ueleze ni yapi.
(e) Eleza manufaa mawili ya asali:
(i) Ndani ya mwili
(ii)Nje ya mwili
(f)Eleza maana ya msamiati huu kama uliyotumika katika kifungu.
(i) Akina yahe
(ii) Sugu
(iii)Vipodozi
Date posted: January 23, 2018. Answers (1)
Huku ukitolea mifano ya kipera husika, fafanua dhima za maghani.(Solved)
Huku ukitolea mifano ya kipera husika, fafanua dhima za maghani.
Date posted: January 19, 2018. Answers (1)
Je, miviga ina upungufu gani?(Solved)
Je, miviga ina upungufu gani
Date posted: January 17, 2018. Answers (1)
Andika katika usemi wa taarifa
“Karibu Bakari, tafadhali kaa”, Maimuna alisema. “Asante, je, habari za nyumbani?” Bakari aliuliza(Solved)
Andika katika usemi wa taarifa
“Karibu Bakari, tafadhali kaa”, Maimuna alisema. “Asante, je, habari za nyumbani?” Bakari aliuliza
Date posted: January 17, 2018. Answers (1)