Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali. Ni dhahiri shahiri kwamba uharamia umechipuka kama desturi na mfumo wa maisha katika siku za hivi karibuni. Janga hili limeshamiri...

      

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Ni dhahiri shahiri kwamba uharamia umechipuka kama desturi na mfumo wa maisha katika siku za hivi karibuni. Janga hili limeshamiri hususan pembeni mwa bara la Afrika na kanda ya Afrika Mashariki.Taarifa za uharamia zimetawala vyombo vya habari, kiasi cha kwamba haipiti siku bila kuripotiwa visa vipya vya matendo haya mabovu ambayo yanaweza tu kumithilishwa na uhayawani.Matukio haya yamewalimbikizia mabaharia na nchi husika, simanzi na masaibu yasiyoweza kutiwa kwenye mizani.
Yumkini tatizo hili halitokei pasi na kumotishwa na kitita kikubwa cha fidia kinachodaiwa na maharamia hawa. Aghalabu, suala hili lahusishwa pakubwa na azma na ari ya kuendeleza ujambazi wa kimataifa sawia na ulipuaji wa bomu mijini Nairobi na Dar es Salaam mnamo Agosti 7,1998, na tukio la Septemba 11, mwaka wa 2001 kule Marekani.Maafa na uharibifu wa mali si hoja, la mno kwa maharamia ni kutosheleza matakwa yao. Kwa upande mwingine, ukosefu wa tawala-wajibika katika maeneo kunakotokea unyama huu ni thibitisho tosha la mazingara yanayowezesha na kuruhusu kuchipuka kwa janga hili.
Mchipuko wa baa la uharamia umelengwa jamii ya kimataifa ambayo ni mhudumu mkuu wa harakati za kusitisha majanga makubwa kama vile njaa, umaskini na magonjwa yaliyosheheni pakubwa barani. Bila shaka, hili ni suala linalosawisishwa na ‘kinyume mbele’. Maharamia wanatishia utangamano wa kimataifa wanapotibua usafiri wa abiria na shehena zinazoelekezwa sehemu tofauti ulimwenguni.
Matumizi ya kidiplomasia na mashauriano hayaelekei kuzalisha matunda katika juhudi za kudhibiti uharamia. Zaidi ya hayo, matumizi ya nguvu yahusishayo mashambulizi pamoja na maharamia kufunguliwa mashtaka nchini Kenya na Ufaransa kunaelekea kuzipiga jeki juhudi za uharamia ulimwenguni.Aidha, utawala wa nchi kunakochipuka uharamia haujajizatiti kuharamisha doa hili linalotisha ustawi wa kimataifa.
Mathalan, ni jambo lisilopingika inapobainika kuwa uharamia umedumaza biashara ya kimataifa, hali inayochangia upungufu na ucheleweshaji wa bidhaa muhimu zinazoendeleza ustawi wa uchumi. Dosari hii inaelekea kukwamiza mojawapo wa malengo ya maendeleo ya milenia yanayosisitiza uimarishaji na ushirikiano wa maendeleo na upanuzi wa masoko ulimwenguni. Harakati za kitalii katika kanda ya mashariki ya bara la Afrika zimehujumiwa. Ni muhali kwa utalii kustawi kwenye maeneo yaliyo na tishio la usalama. ltakumbukwa bayana kwamba watalii hawasafiri tu kwa ndege bali hata kwa meli.
Jitihada za kuweka laini za mawasiliano chini ya bahari ili kurahisisha na kupunguza gharama za mtandao ulimwenguni ni ndoto ambayo haijatimia hadi hivi sasa, kufuatia juhudi za maharamia katika bahari ya Hindi. Kwa mujibu wa hali hii, mawasiliano mepesi na nafuu yasitarajiwe hivi karibuni. Licha ya hayo, shughuli za uvuvi na biashara nyenginezo kwenye kanda ya mwambao zimetiliwa shaka si haba.
Itabidi mikakati na suluhisho la kudumu liweze kupatikana ili vitendo vya uharamia viweze
kusitishwa.

MASWALI

(a) Kwa nini uharamia umetamalaki ulimwenguni?

(b) Fafanua dhana ya ‘kinyume-mbele’ kwa mujibu wa taarifa hii.


(c) Uharamia unaelekea kumtia hofu mwandishi. Fafanua.


(d) Thibitisha kuwa Kenya imeathirika pakubwa kutokana na vitendo vya uharamia




(e) Ukirejelea kifungu, eleza maana ya:
(i) uharamia ………………………………………………………………………………….
(ii) mtandao …………………………………………………………………………………
(iii) mwambao ………………………………………………………………………………

  

Answers


Peter
a)
(i) Pesa au fidia wanazolipwa maharamia.
(ii) Ari ya kuendeleza ujambazi wa kimataifa
(iii) Ukosefu wa utawala wa kuwajibika katika sehemu/nchi kunakotokea uharamia

b) Uharamia unaotokea barani Afrika umeelekezewa jamii ya kimataifa ambayo ni mhusika mkuu wa kuinusuru Afrika kutokana na njaa, magonjwa na umaskini.
(i) Matumizi ya diplomasia na mashauriano hayajafaulu katika kumaliza uharamia ulimwenguni
(ii) Matumizi ya nguvu (mashambulizi na mashtaka) yanaonekana kuendeleza uharamia.
(iii) Utawala/ uongozi wa mataifa husika haujajizatiti kuuharamisha uharamia.
d)
(i) Uharamia umedumaza biashara kutokana na upungufu na ucheleweshaji wa bidhaa muhimu zinazohitajika nchini.
(ii) Shughuli za kitalii zinahujumiwa
(iii) Kucheleweshwa kwa uwekaji wa nyaya/ laini za kuwezesha urahisi na wepesi wa
mawasiliano ulimwenguni.
(iv) Uvuvi pamoja na shughuli nyingine zinazotendeka mwambao haziendelezwi ipasavyo.
e)
(i) Wizi, ujambazi au unyang’anyi wa baharini kwa kutumia nguvu.
(ii) Mfumo wa mawasiliano yaunganishayo ulimwengu kwa matumizi ya tarakilishi au simu
za rununu.
(iii) Sehemu ya nchi iliyo karibu na bahari; pwani.



Musyoxx answered the question on February 22, 2018 at 16:23


Next: Describe a typical coreless type of induction furnace and its special features
Previous: Eleza majukumu manne yanayotekelezwa na lugha katika jamii

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. T. Arege: Barabara Barabara bado ni ndefu Nami tayari nimechoka tiki Natamani kuketi Ninyooshe misuli Nituliza akili. Lakini Azma yanisukuma Mbele ikinihimiza kuendelea Baada ya miinuko...(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
    T. Arege: Barabara
    Barabara bado ni ndefu
    Nami tayari nimechoka tiki
    Natamani kuketi
    Ninyooshe misuli
    Nituliza akili.
    Lakini
    Azma yanisukuma
    Mbele ikinihimiza kuendelea
    Baada ya miinuko na kuruha
    Sasa naona unyoofu wake
    Unyoofu ambao unatisha zaidi.
    Punde natumbukia katika shimo
    Nahitaji siha zaidi ili kupanda tena
    Ghafla nakumbuka ilivyosema
    lie sauti zamani kidogo
    "Kuwa tayari kupanda na kushuka
    Ingawa nimechoka
    Jambo moja li dhahiri
    Lazima nifuate barabara
    Ingawa machweo yaingia
    Nizame na kuibuka
    Nipande na kushuka.
    Jambo moja nakukumbukia:
    Mungu Je, nimwombe tena?
    Hadi lini? Labda amechoshwa na ombaomba zangu
    Nashangaa tena!
    Kitu kimoja nakiamini
    Lazima niendelee kijitahidi kwa kila hatua mpya
    Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu
    Nikinaswa na kujinasua
    Yumkini nitafika mwisho wake
    Ingawa wangu mwisho haitauwahi kabla.
    (a) Eleza toni ya shairi hili.
    B)Mshairi ana maana gani anaposema "Kuwa tayari kupanda na kushuka"
    katika ubeti wa tatu?
    (c) Fafanua tamathali tano za usemi zilizotumiwa katika shairi hili
    ukizitolea mifano mwafaka.
    (d) Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano wa shairi hili.
    (e) Eleza maana ya:
    (i) kuruba
    (ii) barabara yenye ukungu

    Date posted: February 7, 2018.  Answers (1)

  • Jadili maudhui ya elimu kwa mujibu wa "Kanda la Usufi", "Shaka ya Mambo" na "Tazama na Mauti(Solved)

    Jadili maudhui ya elimu kwa mujibu wa "Kanda la Usufi", "Shaka ya Mambo" na "Tazama na Mauti

    Date posted: February 7, 2018.  Answers (1)

  • Kwa kutumia mifano mwafaka eleza majukumu matano ya nyimbo katika jamii(Solved)

    Kwa kutumia mifano mwafaka eleza majukumu matano ya nyimbo katika jamii

    Date posted: February 6, 2018.  Answers (1)

  • Ili kuweza kufanikisha uwasilishaji wa utanzu wa nyimbo kwa hadhira eleza mambo anayohitaji mwimbaji.(Solved)

    Ili kuweza kufanikisha uwasilishaji wa utanzu wa nyimbo kwa hadhira eleza mambo anayohitaji mwimbaji.

    Date posted: February 6, 2018.  Answers (1)

  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Kilio cha Lugha Ni wimbo najiimbia, nijiliwaze Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi Lugha ya...(Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
    Kilio cha Lugha
    Ni wimbo najiimbia, nijiliwaze
    Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi
    Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi
    Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia
    Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa
    Hamna nami imani, wala kupanga siasa,
    Mwasema sayansini, siku ningalitosa,
    Mwanambia nikotosa, kuiva sijafika.
    Ela muelewe sana, Maamuma na Imamu,
    Mulipokuwa vijana, kwenu nilikuwa timamu,
    Sasa mumesoma sana, mwaniona ni haramu,
    Mujue kuwa dawamu, utumwa mwauridhia.
    Mzaliwapo mwalia, 'maa', maneno ya kwanza,
    Lugha munayokulia, ya mama zetu ya kwanza,
    Wa lugha muwedoria, muweze na kuikuza,
    Sio kujipendekeza, uzungu kuigiza.
    Majira ya ukoloni, ukombozi kusambaza,
    Lugha mulithamini, Kiswahili kufukiza,
    Hata kule risavuni, kizungu hanikuwaza,
    Sasa mbona mwanibeza, mbali mwanitupilia?
    Sayansi sio asili, msamiatiwe sinao,
    Sayansi yataka mbali, msamiati ni wa hao
    Nitakuwa Kiswahili, kiomba majina yao
    Lugha kujikuza kwao, huomba linalofaa.
    Enyi viongozi wetu ipangeni nadharia,
    Kujenga siasa yetu, tuzidi kuwa huria
    Lugha hata 'mbusha watu, tuche kuriaria,
    Sifa ni kwa chake mtu, cha mwenzi hutoringia.
    Utajiri wangu hasa, nikiwatajia wote,
    Msamiati huwa, ni wa Afrika yote,
    Na methali za kuasa, nahau na ngeli zote,
    Na nisemwapo popote, ujumbe hukamilika.
    Afrika ndipo petu, pa wabantu halisi,
    Baba na mama ni Bantu, shina la wangu ukwasi,
    Warabu na wengi wetu, sio wangu Adinasi
    Kwao 'meomba kiasi, ili kujizidisha.
    Mfumo mpya hongera, wa elimu humu Kenya,
    Lugha takuwa imara, ukabila tutafinya,
    Kiswahili ni ibara, kila mtu kiimanya,
    Methali imetuonya, mtumwa si mwasilia
    Tamati lugha yalia, yabaguliwa bayana,
    Kukua imeridhia, msamiati kufana,
    Wengine wataijulia, kwa marefu na mapana,
    Lugha yenu ya maana, mwaipuuza yalia.
    (a) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu.
    (b) Kwa kutoa hoja ime, eleza kwa nini shairi hili likaitwa kilio cha lugha.
    (c) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari.
    (d) Eleza toni ya shairi hili.
    (e) Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano milatu.
    F)Bainisha nafsineni katika shairi.
    G)Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa shairi.
    (i) nasongwa
    (ii) kuriaria
    (iii) adinasi

    Date posted: February 6, 2018.  Answers (1)

  • "... dawa ya adui ni kummegea unachokula." (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Jadili jinsi dawa inayorejelewa inavyozorotesha hali katika mji wa Cheneo.(Solved)

    "... dawa ya adui ni kummegea unachokula."
    (a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
    (b) Jadili jinsi dawa inayorejelewa inavyozorotesha hali katika mji wa
    Cheneo.

    Date posted: February 6, 2018.  Answers (1)

  • "Anwani Mstahiki Meya ni kinaya." Jadili ukweli wa kauli hii kwa kurejelea tamthilia.(Solved)

    "Anwani Mstahiki Meya ni kinaya." Jadili ukweli wa kauli hii
    kwa kurejelea tamthilia.

    Date posted: February 6, 2018.  Answers (1)

  • Jadili umuhimu wa kinachotafutwa katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. (Solved)

    Jadili umuhimu wa kinachotafutwa katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

    Date posted: February 6, 2018.  Answers (1)

  • Fafanua mjukumu ya elimu na dini katika jamii kwa mujibu wa riwaya: Kidagaa Kimemwozea.(Solved)

    Fafanua mjukumu ya elimu na dini katika jamii kwa mujibu wa riwaya:
    Kidagaa Kimemwozea.

    Date posted: February 6, 2018.  Answers (1)

  • Jadili dhima ya fasihi katika jamii(Solved)

    Jadili dhima ya fasihi katika jamii

    Date posted: February 6, 2018.  Answers (1)

  • Fafanua sifa za Kenga kama zinavyojitokeza wazi katika tamthilia ya kigogo.(Solved)

    Fafanua sifa za Kenga kama zinavyojitokeza wazi katika tamthilia ya kigogo.

    Date posted: January 31, 2018.  Answers (1)

  • Eleza changamoto zilizoukabili usanifishaji wa kiswahili.(Solved)

    Eleza changamoto zilizoukabili usanifishaji wa kiswahili.

    Date posted: January 30, 2018.  Answers (1)

  • Soma kifungu kifuatacho halafu ujibu maswali yanayoifuatia. Watu wengi hawawezi kunywa chai au uji bila kutia sukari. Wanatumia sukari kwa hamu na ghamu bila kutambua kuwa...(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho halafu ujibu maswali yanayoifuatia.

    Watu wengi hawawezi kunywa chai au uji bila kutia sukari. Wanatumia sukari kwa hamu na ghamu bila kutambua kuwa hiyo ni sumu wanayojiongezea mwilini.


    Ni ukweli usiopingika kuwa wazee wetu wa jadi waliishi muda mrefu wakiwa na siha njema kuliko sisi. Hii ni kwa sababu waliishi katika kipindi ambacho sukari inayotengenezwa viwandani haikuweko. Iwapo ilikuweko, ilikuwa bidhaa ya wateule wa ungwana kutengenezea vitu kama keki, mahamri na vitumbua. Akina yahe hawangeweza kuigharamia.


    Watafiti wa masuala ya afya wamegundua kuwa sukari inayotayarishwa viwandani sasa hivi haina virutubishi vyovyote. Hali kadhalika, utaratibu wa viwandani wa kutayarisha sukari ili iwe nyeupe na kuichuja huharibu virutubishi vinavyoweza kuwa muhimu mwilini. Umuhimu wa sukari wakausaza kuwa kutia ladha tamu tu. Umuhimu huu hauwezi kulinganishwa na madhara yanayoletwa na sukari hii. Baada ya kusagika mwilini, sukari hii huacha masalio ya sidi mwilini yenye sumu inayoathiri siha.

    Matumizi ya sukari kwa wingi husababisha madhara mbalimbali mwilini. Huchangia kuoza na kuharibika kwa meno. Sukari nyeupe imehusishwa na ongezeko la maradhi ya kisukari, moyo na hipoglisimoia au upungufu wa sukari mwilini. Matumizi holela ya sukari huleta kipandauso au ugonjwa wa ghafla wa kuumwa na upande mmoja wa kichwa unaoambatana na kichefuchefu, kutapika na matatizo ya kuona. Sukari pia huleta maradhi ya ngozi na figo, pamoja na ongezeko la kemikali iitwayo kolestroli, ambayo ni ufuta unaonata na hutokana na kutoyeyuka kwa mafuta yote mwilini. Kemikali hii inaporundikana moyoni, hufanya mishipa inayotoa damu moyoni na kuisambaza mwilini kuwa myembamba na sugu. Moyo hulazimika kusukuma damu kwa nguvu na huenda ukachoka na kukoma kufanya kazi.


    Wataalamu wa lishe bora wamependekeza ulaji wa vyakula kama nafaka, matunda, mboga na miwa ambavyo vimejaa sukari asilia. Fauka ya hayo, sukari inayotokana katika asali ni bora zaidi kwa mwili wa mwanadamu. Asali huwa na sukari asilia, vitamini, madini na amino asidi. Hivi vyote huwa na manufaa mbalimbali mwilini. Asali huupa mwili nishati inayohitajika kuendesha shughuli za viungo.Licha ya hayo, asali huchangamsha mwili. Asali huwa na kemikali ambazo huwasaidia watoto kukua vizuri. Huweza kuzidisha kiwango cha himoglobini, hivyo kupunguza uwezekano wa watoto kuwa na anemia (upungufu wa damu). Asali husaidi katika usagaji wa chakula iwapo itatumiwa kabla ya mlo. Matumizi ya kijiko kimoja cha asali kila siku husaidia mwili kujikinga dhidi ya magonjwa ya kukohoa. Asali husaidia pia kuondoa harufu mbaya kinywani.


    Asali inaweza kutumiwa kujipaka. Inapotumika kwa njia hii, hutunza ngozi na kuifanya ing'are, huondoa vipele na ugumu wa ngozi, pamoja na kutibu kule ngozi ilikokatikakatika. Hali kadhalika asali hutibu vidonda. Viwanda vingi vya vipodozi vilevile hutumia asali kama malighafi muhimu katika utengenezaji wa bidhaa hizo.
    (a) Pendekeza anwani kwa taarifa uliyosoma.
    (b) Taja matumizi mawili ya sukari nyeupe
    (c) Eleza madhara matatu ya sukari nyeupe mwilini.
    (d) Bainisha aina ya sukari iliyo na manufaa mwilini mwa binadamu na ueleze ni yapi.
    (e) Eleza manufaa mawili ya asali:
    (i) Ndani ya mwili
    (ii)Nje ya mwili

    (f)Eleza maana ya msamiati huu kama uliyotumika katika kifungu.
    (i) Akina yahe
    (ii) Sugu
    (iii)Vipodozi

    Date posted: January 23, 2018.  Answers (1)

  • Ukifuata utratibu unaokubalika, onyesha hatua sita za uwasilishaji wa vitendawili. (Solved)

    Ukifuata utratibu unaokubalika, onyesha hatua sita za uwasilishaji wa vitendawili.

    Date posted: January 19, 2018.  Answers (1)

  • Huku ukitolea mifano ya kipera husika, fafanua dhima za maghani.(Solved)

    Huku ukitolea mifano ya kipera husika, fafanua dhima za maghani.

    Date posted: January 19, 2018.  Answers (1)

  • Je, miviga ina upungufu gani?(Solved)

    Je, miviga ina upungufu gani

    Date posted: January 17, 2018.  Answers (1)

  • Orodhesha sherehe nne za jamii yako zinazohusishwa na miviga (Solved)

    Orodhesha sherehe nne za jamii yako zinazohusishwa na miviga

    Date posted: January 17, 2018.  Answers (1)

  • Fafanua kikamilifu dhana zifuatazo za fasihi simulizi i) Nyiso ii) Mbolezi iii) Hodiya iv) Bembelezi v) Sifo(Solved)

    Fafanua kikamilifu dhana zifuatazo za fasihi simulizi
    i) Nyiso
    ii) Mbolezi
    iii) Hodiya
    iv) Bembelezi
    v) Sifo

    Date posted: January 17, 2018.  Answers (1)

  • Andika katika usemi wa taarifa “Karibu Bakari, tafadhali kaa”, Maimuna alisema. “Asante, je, habari za nyumbani?” Bakari aliuliza(Solved)

    Andika katika usemi wa taarifa
    “Karibu Bakari, tafadhali kaa”, Maimuna alisema. “Asante, je, habari za nyumbani?” Bakari aliuliza

    Date posted: January 17, 2018.  Answers (1)

  • Andika katika hali ya kutendewa: Kuku hawa wamemsumbua Sabina kwa muda mrefu.(Solved)

    Andika katika hali ya kutendewa:
    Kuku hawa wamemsumbua Sabina kwa muda mrefu.

    Date posted: January 17, 2018.  Answers (1)