Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
2. Riwaya ya kidagaa imeangazia maudhui ya utengano. Thibitisha.
a) Fao anatengana na mwanafunzi wake baada ya kumpachika mimba.
b) Uhuru anatengana na wazazi wake yaani Lowela na M.N Bora wanapompoza Amani ulezi wake.
c) M. N. Bora anatengana na Amani baada ya kumshuku kwamba ana uhusiano na mkewe Bi.Zuhura.
d) Aidha kuna utengano kati ya M.M. Majisifu na mkewe Dora kutokana na falsafa yake.
e) Chichiri Hamadi anatengana na familia yake baada ya kuuliwa na M.N.Bora.
f) M. N. Bora anatengana na mkewe Bi Zuhura baada ya kumpata Amani katika chumba chake.
g) M.N. Bora anafanya Lowela kutengana na wazazi wake.
h) M.N. Bora ikizidi anasababisha utengano kati ya Mashaka na Ben Bella.
i) Mashaka anabadilika na kuwa mwendawazimu baada ya kutengana na Ben Bella anatengana na afya yeke nzuri.
j) M.N. Bora anafanya watu kutengana na mashamba yaoakina Imani na Chirchir Hamadi.
k) Michelle anatengana na Majununi.
l) Amani anatengana na mswada wake baada ya kuibiwa na M.M. Majisifu.
m) M.M. Majisifu anatengana na kazi zake na kuingilia ulevi.
n) M.M. Majisifu anatengana na wanawe walemavu na hata kuwaita mashata na masimbi.
o) Amani anatengana na masomo yake baada ya kusingiziwa uchochezi.
p) Amani na Imani wanatengana na shughuli zao za kila siku kufungwa jela kwa kusingiziwa kukiua kitoto Uhuru.
q) Uhuru anatengana na uhai wake – anaaga dunia.
r) Chwehwe Makweche (Horse power) anatengana /talanta yake baada ya kujeruhiwa.
s) Mamake Imani anatengana na uhai wake baaada ya kupigwa na askari na kuuwawa.
t) Oscar Kambona anatengana na boma lao baada ya mamake kuuwawa.
u) Serekali haidhamini masomo ya umma hivyo kuwafanya wanafunzi wengi kama vile Imani, Amani, DJ, na kutengana na masomo yao.
v) M.N. Bora anaitisha hongo ili awahurumie raia katika ofisiyake hivyo kuwafanya watengane na hela zao.
w) Majibwa ya M.N. Bora yanatengana na afya bora kwa sababu hayachanjwi wala kulishwa vizuri.
x) M.N. Bora anawafuta wafanyakazi kiholela hata wanaponadhifisha maskani yake – utengano na gazi.
y) Madhubuti anatengana na wazazi wake (baba yake)
z) M.N. Bora anatengana na cheo chake (utemi)
M.N. Bora anatengana na uhai wake kwa kujitia kitanzi.
M.M. Majisifu anatengana na wanafunzi wa chuo kikuu cha mukokotoni.
Musyoxx answered the question on February 22, 2018 at 18:29
- Lugha huchangia vipi kuleta;
i) Utengano
ii) Utangamano katika jamii
(Solved)
Lugha huchangia vipi kuleta;
i) Utengano
ii) Utangamano katika jamii
Date posted: February 22, 2018. Answers (1)
- Eleza majukumu manne yanayotekelezwa na lugha katika jamii(Solved)
Eleza majukumu manne yanayotekelezwa na lugha katika jamii
Date posted: February 22, 2018. Answers (1)
- Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Ni dhahiri shahiri kwamba uharamia umechipuka kama desturi na mfumo wa maisha katika siku za hivi karibuni. Janga hili limeshamiri...(Solved)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Ni dhahiri shahiri kwamba uharamia umechipuka kama desturi na mfumo wa maisha katika siku za hivi karibuni. Janga hili limeshamiri hususan pembeni mwa bara la Afrika na kanda ya Afrika Mashariki.Taarifa za uharamia zimetawala vyombo vya habari, kiasi cha kwamba haipiti siku bila kuripotiwa visa vipya vya matendo haya mabovu ambayo yanaweza tu kumithilishwa na uhayawani.Matukio haya yamewalimbikizia mabaharia na nchi husika, simanzi na masaibu yasiyoweza kutiwa kwenye mizani.
Yumkini tatizo hili halitokei pasi na kumotishwa na kitita kikubwa cha fidia kinachodaiwa na maharamia hawa. Aghalabu, suala hili lahusishwa pakubwa na azma na ari ya kuendeleza ujambazi wa kimataifa sawia na ulipuaji wa bomu mijini Nairobi na Dar es Salaam mnamo Agosti 7,1998, na tukio la Septemba 11, mwaka wa 2001 kule Marekani.Maafa na uharibifu wa mali si hoja, la mno kwa maharamia ni kutosheleza matakwa yao. Kwa upande mwingine, ukosefu wa tawala-wajibika katika maeneo kunakotokea unyama huu ni thibitisho tosha la mazingara yanayowezesha na kuruhusu kuchipuka kwa janga hili.
Mchipuko wa baa la uharamia umelengwa jamii ya kimataifa ambayo ni mhudumu mkuu wa harakati za kusitisha majanga makubwa kama vile njaa, umaskini na magonjwa yaliyosheheni pakubwa barani. Bila shaka, hili ni suala linalosawisishwa na ‘kinyume mbele’. Maharamia wanatishia utangamano wa kimataifa wanapotibua usafiri wa abiria na shehena zinazoelekezwa sehemu tofauti ulimwenguni.
Matumizi ya kidiplomasia na mashauriano hayaelekei kuzalisha matunda katika juhudi za kudhibiti uharamia. Zaidi ya hayo, matumizi ya nguvu yahusishayo mashambulizi pamoja na maharamia kufunguliwa mashtaka nchini Kenya na Ufaransa kunaelekea kuzipiga jeki juhudi za uharamia ulimwenguni.Aidha, utawala wa nchi kunakochipuka uharamia haujajizatiti kuharamisha doa hili linalotisha ustawi wa kimataifa.
Mathalan, ni jambo lisilopingika inapobainika kuwa uharamia umedumaza biashara ya kimataifa, hali inayochangia upungufu na ucheleweshaji wa bidhaa muhimu zinazoendeleza ustawi wa uchumi. Dosari hii inaelekea kukwamiza mojawapo wa malengo ya maendeleo ya milenia yanayosisitiza uimarishaji na ushirikiano wa maendeleo na upanuzi wa masoko ulimwenguni. Harakati za kitalii katika kanda ya mashariki ya bara la Afrika zimehujumiwa. Ni muhali kwa utalii kustawi kwenye maeneo yaliyo na tishio la usalama. ltakumbukwa bayana kwamba watalii hawasafiri tu kwa ndege bali hata kwa meli.
Jitihada za kuweka laini za mawasiliano chini ya bahari ili kurahisisha na kupunguza gharama za mtandao ulimwenguni ni ndoto ambayo haijatimia hadi hivi sasa, kufuatia juhudi za maharamia katika bahari ya Hindi. Kwa mujibu wa hali hii, mawasiliano mepesi na nafuu yasitarajiwe hivi karibuni. Licha ya hayo, shughuli za uvuvi na biashara nyenginezo kwenye kanda ya mwambao zimetiliwa shaka si haba.
Itabidi mikakati na suluhisho la kudumu liweze kupatikana ili vitendo vya uharamia viweze
kusitishwa.
MASWALI
(a) Kwa nini uharamia umetamalaki ulimwenguni?
(b) Fafanua dhana ya ‘kinyume-mbele’ kwa mujibu wa taarifa hii.
(c) Uharamia unaelekea kumtia hofu mwandishi. Fafanua.
(d) Thibitisha kuwa Kenya imeathirika pakubwa kutokana na vitendo vya uharamia
(e) Ukirejelea kifungu, eleza maana ya:
(i) uharamia ………………………………………………………………………………….
(ii) mtandao …………………………………………………………………………………
(iii) mwambao ………………………………………………………………………………
Date posted: February 22, 2018. Answers (1)
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
T. Arege: Barabara
Barabara bado ni ndefu
Nami tayari nimechoka tiki
Natamani kuketi
Ninyooshe misuli
Nituliza akili.
Lakini
Azma yanisukuma
Mbele ikinihimiza kuendelea
Baada ya miinuko...(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
T. Arege: Barabara
Barabara bado ni ndefu
Nami tayari nimechoka tiki
Natamani kuketi
Ninyooshe misuli
Nituliza akili.
Lakini
Azma yanisukuma
Mbele ikinihimiza kuendelea
Baada ya miinuko na kuruha
Sasa naona unyoofu wake
Unyoofu ambao unatisha zaidi.
Punde natumbukia katika shimo
Nahitaji siha zaidi ili kupanda tena
Ghafla nakumbuka ilivyosema
lie sauti zamani kidogo
"Kuwa tayari kupanda na kushuka
Ingawa nimechoka
Jambo moja li dhahiri
Lazima nifuate barabara
Ingawa machweo yaingia
Nizame na kuibuka
Nipande na kushuka.
Jambo moja nakukumbukia:
Mungu Je, nimwombe tena?
Hadi lini? Labda amechoshwa na ombaomba zangu
Nashangaa tena!
Kitu kimoja nakiamini
Lazima niendelee kijitahidi kwa kila hatua mpya
Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu
Nikinaswa na kujinasua
Yumkini nitafika mwisho wake
Ingawa wangu mwisho haitauwahi kabla.
(a) Eleza toni ya shairi hili.
B)Mshairi ana maana gani anaposema "Kuwa tayari kupanda na kushuka"
katika ubeti wa tatu?
(c) Fafanua tamathali tano za usemi zilizotumiwa katika shairi hili
ukizitolea mifano mwafaka.
(d) Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano wa shairi hili.
(e) Eleza maana ya:
(i) kuruba
(ii) barabara yenye ukungu
Date posted: February 7, 2018. Answers (1)
- Jadili maudhui ya elimu kwa mujibu wa "Kanda la Usufi", "Shaka ya Mambo" na "Tazama na Mauti(Solved)
Jadili maudhui ya elimu kwa mujibu wa "Kanda la Usufi", "Shaka ya Mambo" na "Tazama na Mauti
Date posted: February 7, 2018. Answers (1)
- Kwa kutumia mifano mwafaka eleza majukumu matano ya nyimbo katika jamii(Solved)
Kwa kutumia mifano mwafaka eleza majukumu matano ya nyimbo katika jamii
Date posted: February 6, 2018. Answers (1)
- Ili kuweza kufanikisha uwasilishaji wa utanzu wa nyimbo kwa hadhira eleza mambo anayohitaji mwimbaji.(Solved)
Ili kuweza kufanikisha uwasilishaji wa utanzu wa nyimbo kwa hadhira eleza mambo anayohitaji mwimbaji.
Date posted: February 6, 2018. Answers (1)
- Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Kilio cha Lugha
Ni wimbo najiimbia, nijiliwaze
Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi
Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi
Lugha ya...(Solved)
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Kilio cha Lugha
Ni wimbo najiimbia, nijiliwaze
Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi
Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi
Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia
Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa
Hamna nami imani, wala kupanga siasa,
Mwasema sayansini, siku ningalitosa,
Mwanambia nikotosa, kuiva sijafika.
Ela muelewe sana, Maamuma na Imamu,
Mulipokuwa vijana, kwenu nilikuwa timamu,
Sasa mumesoma sana, mwaniona ni haramu,
Mujue kuwa dawamu, utumwa mwauridhia.
Mzaliwapo mwalia, 'maa', maneno ya kwanza,
Lugha munayokulia, ya mama zetu ya kwanza,
Wa lugha muwedoria, muweze na kuikuza,
Sio kujipendekeza, uzungu kuigiza.
Majira ya ukoloni, ukombozi kusambaza,
Lugha mulithamini, Kiswahili kufukiza,
Hata kule risavuni, kizungu hanikuwaza,
Sasa mbona mwanibeza, mbali mwanitupilia?
Sayansi sio asili, msamiatiwe sinao,
Sayansi yataka mbali, msamiati ni wa hao
Nitakuwa Kiswahili, kiomba majina yao
Lugha kujikuza kwao, huomba linalofaa.
Enyi viongozi wetu ipangeni nadharia,
Kujenga siasa yetu, tuzidi kuwa huria
Lugha hata 'mbusha watu, tuche kuriaria,
Sifa ni kwa chake mtu, cha mwenzi hutoringia.
Utajiri wangu hasa, nikiwatajia wote,
Msamiati huwa, ni wa Afrika yote,
Na methali za kuasa, nahau na ngeli zote,
Na nisemwapo popote, ujumbe hukamilika.
Afrika ndipo petu, pa wabantu halisi,
Baba na mama ni Bantu, shina la wangu ukwasi,
Warabu na wengi wetu, sio wangu Adinasi
Kwao 'meomba kiasi, ili kujizidisha.
Mfumo mpya hongera, wa elimu humu Kenya,
Lugha takuwa imara, ukabila tutafinya,
Kiswahili ni ibara, kila mtu kiimanya,
Methali imetuonya, mtumwa si mwasilia
Tamati lugha yalia, yabaguliwa bayana,
Kukua imeridhia, msamiati kufana,
Wengine wataijulia, kwa marefu na mapana,
Lugha yenu ya maana, mwaipuuza yalia.
(a) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu.
(b) Kwa kutoa hoja ime, eleza kwa nini shairi hili likaitwa kilio cha lugha.
(c) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari.
(d) Eleza toni ya shairi hili.
(e) Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano milatu.
F)Bainisha nafsineni katika shairi.
G)Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa shairi.
(i) nasongwa
(ii) kuriaria
(iii) adinasi
Date posted: February 6, 2018. Answers (1)
- "... dawa ya adui ni kummegea unachokula."
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Jadili jinsi dawa inayorejelewa inavyozorotesha hali katika mji wa
Cheneo.(Solved)
"... dawa ya adui ni kummegea unachokula."
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
(b) Jadili jinsi dawa inayorejelewa inavyozorotesha hali katika mji wa
Cheneo.
Date posted: February 6, 2018. Answers (1)
- "Anwani Mstahiki Meya ni kinaya." Jadili ukweli wa kauli hii
kwa kurejelea tamthilia.(Solved)
"Anwani Mstahiki Meya ni kinaya." Jadili ukweli wa kauli hii
kwa kurejelea tamthilia.
Date posted: February 6, 2018. Answers (1)
- Jadili umuhimu wa kinachotafutwa katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. (Solved)
Jadili umuhimu wa kinachotafutwa katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.
Date posted: February 6, 2018. Answers (1)
- Fafanua mjukumu ya elimu na dini katika jamii kwa mujibu wa riwaya:
Kidagaa Kimemwozea.(Solved)
Fafanua mjukumu ya elimu na dini katika jamii kwa mujibu wa riwaya:
Kidagaa Kimemwozea.
Date posted: February 6, 2018. Answers (1)
- Jadili dhima ya fasihi katika jamii(Solved)
Jadili dhima ya fasihi katika jamii
Date posted: February 6, 2018. Answers (1)
- Fafanua sifa za Kenga kama zinavyojitokeza wazi katika tamthilia ya kigogo.(Solved)
Fafanua sifa za Kenga kama zinavyojitokeza wazi katika tamthilia ya kigogo.
Date posted: January 31, 2018. Answers (1)
- Eleza changamoto zilizoukabili usanifishaji wa kiswahili.(Solved)
Eleza changamoto zilizoukabili usanifishaji wa kiswahili.
Date posted: January 30, 2018. Answers (1)
- Soma kifungu kifuatacho halafu ujibu maswali yanayoifuatia.
Watu wengi hawawezi kunywa chai au uji bila kutia sukari. Wanatumia sukari kwa hamu na ghamu bila kutambua kuwa...(Solved)
Soma kifungu kifuatacho halafu ujibu maswali yanayoifuatia.
Watu wengi hawawezi kunywa chai au uji bila kutia sukari. Wanatumia sukari kwa hamu na ghamu bila kutambua kuwa hiyo ni sumu wanayojiongezea mwilini.
Ni ukweli usiopingika kuwa wazee wetu wa jadi waliishi muda mrefu wakiwa na siha njema kuliko sisi. Hii ni kwa sababu waliishi katika kipindi ambacho sukari inayotengenezwa viwandani haikuweko. Iwapo ilikuweko, ilikuwa bidhaa ya wateule wa ungwana kutengenezea vitu kama keki, mahamri na vitumbua. Akina yahe hawangeweza kuigharamia.
Watafiti wa masuala ya afya wamegundua kuwa sukari inayotayarishwa viwandani sasa hivi haina virutubishi vyovyote. Hali kadhalika, utaratibu wa viwandani wa kutayarisha sukari ili iwe nyeupe na kuichuja huharibu virutubishi vinavyoweza kuwa muhimu mwilini. Umuhimu wa sukari wakausaza kuwa kutia ladha tamu tu. Umuhimu huu hauwezi kulinganishwa na madhara yanayoletwa na sukari hii. Baada ya kusagika mwilini, sukari hii huacha masalio ya sidi mwilini yenye sumu inayoathiri siha.
Matumizi ya sukari kwa wingi husababisha madhara mbalimbali mwilini. Huchangia kuoza na kuharibika kwa meno. Sukari nyeupe imehusishwa na ongezeko la maradhi ya kisukari, moyo na hipoglisimoia au upungufu wa sukari mwilini. Matumizi holela ya sukari huleta kipandauso au ugonjwa wa ghafla wa kuumwa na upande mmoja wa kichwa unaoambatana na kichefuchefu, kutapika na matatizo ya kuona. Sukari pia huleta maradhi ya ngozi na figo, pamoja na ongezeko la kemikali iitwayo kolestroli, ambayo ni ufuta unaonata na hutokana na kutoyeyuka kwa mafuta yote mwilini. Kemikali hii inaporundikana moyoni, hufanya mishipa inayotoa damu moyoni na kuisambaza mwilini kuwa myembamba na sugu. Moyo hulazimika kusukuma damu kwa nguvu na huenda ukachoka na kukoma kufanya kazi.
Wataalamu wa lishe bora wamependekeza ulaji wa vyakula kama nafaka, matunda, mboga na miwa ambavyo vimejaa sukari asilia. Fauka ya hayo, sukari inayotokana katika asali ni bora zaidi kwa mwili wa mwanadamu. Asali huwa na sukari asilia, vitamini, madini na amino asidi. Hivi vyote huwa na manufaa mbalimbali mwilini. Asali huupa mwili nishati inayohitajika kuendesha shughuli za viungo.Licha ya hayo, asali huchangamsha mwili. Asali huwa na kemikali ambazo huwasaidia watoto kukua vizuri. Huweza kuzidisha kiwango cha himoglobini, hivyo kupunguza uwezekano wa watoto kuwa na anemia (upungufu wa damu). Asali husaidi katika usagaji wa chakula iwapo itatumiwa kabla ya mlo. Matumizi ya kijiko kimoja cha asali kila siku husaidia mwili kujikinga dhidi ya magonjwa ya kukohoa. Asali husaidia pia kuondoa harufu mbaya kinywani.
Asali inaweza kutumiwa kujipaka. Inapotumika kwa njia hii, hutunza ngozi na kuifanya ing'are, huondoa vipele na ugumu wa ngozi, pamoja na kutibu kule ngozi ilikokatikakatika. Hali kadhalika asali hutibu vidonda. Viwanda vingi vya vipodozi vilevile hutumia asali kama malighafi muhimu katika utengenezaji wa bidhaa hizo.
(a) Pendekeza anwani kwa taarifa uliyosoma.
(b) Taja matumizi mawili ya sukari nyeupe
(c) Eleza madhara matatu ya sukari nyeupe mwilini.
(d) Bainisha aina ya sukari iliyo na manufaa mwilini mwa binadamu na ueleze ni yapi.
(e) Eleza manufaa mawili ya asali:
(i) Ndani ya mwili
(ii)Nje ya mwili
(f)Eleza maana ya msamiati huu kama uliyotumika katika kifungu.
(i) Akina yahe
(ii) Sugu
(iii)Vipodozi
Date posted: January 23, 2018. Answers (1)
- Ukifuata utratibu unaokubalika, onyesha hatua sita za uwasilishaji wa vitendawili. (Solved)
Ukifuata utratibu unaokubalika, onyesha hatua sita za uwasilishaji wa vitendawili.
Date posted: January 19, 2018. Answers (1)
- Huku ukitolea mifano ya kipera husika, fafanua dhima za maghani.(Solved)
Huku ukitolea mifano ya kipera husika, fafanua dhima za maghani.
Date posted: January 19, 2018. Answers (1)
- Je, miviga ina upungufu gani?(Solved)
Je, miviga ina upungufu gani
Date posted: January 17, 2018. Answers (1)
- Orodhesha sherehe nne za jamii yako zinazohusishwa na miviga (Solved)
Orodhesha sherehe nne za jamii yako zinazohusishwa na miviga
Date posted: January 17, 2018. Answers (1)