Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Jadili jinsi maudhui ya usaliti yanavyofafanuliwa katika tamthilia ya mstahiki Meya.

Jadili jinsi maudhui ya usaliti yanavyofafanuliwa katika tamthilia ya mstahiki Meya.

Answers


Peter
MAUDHUI YA USALITI
-Wananchi wanasalitiwa na Meya
- Wananchi walimchagua Meya ili awaletee maendeleo badala yake anajiongeza posho na kuwasahau wale waliomchagua.
- Wananchi wanasalitiwa na Diwani I na II , wananchi waliwachagua kuwakilisha wananchi wa maeneo.
- Meya anasalitiwa na Bili
Baada ya kumshauri vibaya, Bili alimkimbia Meya na Kuzima simu.
- Meya anasalitiwa na mhazili
Mhazili hakuwa na sifa za kuajiriwa lakini Meya akampa kazi, mgomo ulipofanyika , mhazili aliungana nao.
- Meya anasalitiwa na askari – askari wakati wote walilinda utawala wake, walishiriki kumwondoa madarakani.
- Meya anasalitiwa na Gedi – Gedi alikuwa mpambe wa Meya, anamweleza Siki kuwa Meya hataki kumwona.
- Meya anasalitiwa na Siki, Siki anaungana na wafanyakazi kumpinga Meya ambaye ni binamu yake.
- Meya anasalitiwa na wafanyakazi.
Wafanyakazi walifaa kumtii Meya wanamgeuka na hivyo kumgomea Meya.
- Diwani III anawasaliti Diwani I na II.
Anajiunga na wananchi na kuleta upinzani.
- Mhubiri anawasaliti wananchi kwa kukubali ombi la Bili. Aidha anawasaliti kwa kumuombea Meya ambaye aliwanyanyasa wananchi.

Musyoxx answered the question on February 22, 2018 at 18:31

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions

  • Riwaya ya kidagaa imeangazia maudhui ya utengano. Thibitisha. (Solved)

    Riwaya ya kidagaa imeangazia maudhui ya utengano. Thibitisha.

    Date posted: February 22, 2018 .    Answers (1)

  • Lugha huchangia vipi kuleta; i) Utengano ii) Utangamano katika jamii (Solved)

    Lugha huchangia vipi kuleta;
    i) Utengano
    ii) Utangamano katika jamii

    Date posted: February 22, 2018 .    Answers (1)

  • Eleza majukumu manne yanayotekelezwa na lugha katika jamii (Solved)

    Eleza majukumu manne yanayotekelezwa na lugha katika jamii

    Date posted: February 22, 2018 .    Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali. Ni dhahiri shahiri kwamba uharamia umechipuka kama desturi na mfumo wa maisha katika siku za hivi karibuni. Janga hili limeshamiri... (Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
    Ni dhahiri shahiri kwamba uharamia umechipuka kama desturi na mfumo wa maisha katika siku za hivi karibuni. Janga hili limeshamiri hususan pembeni mwa bara la Afrika na kanda ya Afrika Mashariki.Taarifa za uharamia zimetawala vyombo vya habari, kiasi cha kwamba haipiti siku bila kuripotiwa visa vipya vya matendo haya mabovu ambayo yanaweza tu kumithilishwa na uhayawani.Matukio haya yamewalimbikizia mabaharia na nchi husika, simanzi na masaibu yasiyoweza kutiwa kwenye mizani.
    Yumkini tatizo hili halitokei pasi na kumotishwa na kitita kikubwa cha fidia kinachodaiwa na maharamia hawa. Aghalabu, suala hili lahusishwa pakubwa na azma na ari ya kuendeleza ujambazi wa kimataifa sawia na ulipuaji wa bomu mijini Nairobi na Dar es Salaam mnamo Agosti 7,1998, na tukio la Septemba 11, mwaka wa 2001 kule Marekani.Maafa na uharibifu wa mali si hoja, la mno kwa maharamia ni kutosheleza matakwa yao. Kwa upande mwingine, ukosefu wa tawala-wajibika katika maeneo kunakotokea unyama huu ni thibitisho tosha la mazingara yanayowezesha na kuruhusu kuchipuka kwa janga hili.
    Mchipuko wa baa la uharamia umelengwa jamii ya kimataifa ambayo ni mhudumu mkuu wa harakati za kusitisha majanga makubwa kama vile njaa, umaskini na magonjwa yaliyosheheni pakubwa barani. Bila shaka, hili ni suala linalosawisishwa na ‘kinyume mbele’. Maharamia wanatishia utangamano wa kimataifa wanapotibua usafiri wa abiria na shehena zinazoelekezwa sehemu tofauti ulimwenguni.
    Matumizi ya kidiplomasia na mashauriano hayaelekei kuzalisha matunda katika juhudi za kudhibiti uharamia. Zaidi ya hayo, matumizi ya nguvu yahusishayo mashambulizi pamoja na maharamia kufunguliwa mashtaka nchini Kenya na Ufaransa kunaelekea kuzipiga jeki juhudi za uharamia ulimwenguni.Aidha, utawala wa nchi kunakochipuka uharamia haujajizatiti kuharamisha doa hili linalotisha ustawi wa kimataifa.
    Mathalan, ni jambo lisilopingika inapobainika kuwa uharamia umedumaza biashara ya kimataifa, hali inayochangia upungufu na ucheleweshaji wa bidhaa muhimu zinazoendeleza ustawi wa uchumi. Dosari hii inaelekea kukwamiza mojawapo wa malengo ya maendeleo ya milenia yanayosisitiza uimarishaji na ushirikiano wa maendeleo na upanuzi wa masoko ulimwenguni. Harakati za kitalii katika kanda ya mashariki ya bara la Afrika zimehujumiwa. Ni muhali kwa utalii kustawi kwenye maeneo yaliyo na tishio la usalama. ltakumbukwa bayana kwamba watalii hawasafiri tu kwa ndege bali hata kwa meli.
    Jitihada za kuweka laini za mawasiliano chini ya bahari ili kurahisisha na kupunguza gharama za mtandao ulimwenguni ni ndoto ambayo haijatimia hadi hivi sasa, kufuatia juhudi za maharamia katika bahari ya Hindi. Kwa mujibu wa hali hii, mawasiliano mepesi na nafuu yasitarajiwe hivi karibuni. Licha ya hayo, shughuli za uvuvi na biashara nyenginezo kwenye kanda ya mwambao zimetiliwa shaka si haba.
    Itabidi mikakati na suluhisho la kudumu liweze kupatikana ili vitendo vya uharamia viweze
    kusitishwa.

    MASWALI

    (a) Kwa nini uharamia umetamalaki ulimwenguni?

    (b) Fafanua dhana ya ‘kinyume-mbele’ kwa mujibu wa taarifa hii.


    (c) Uharamia unaelekea kumtia hofu mwandishi. Fafanua.


    (d) Thibitisha kuwa Kenya imeathirika pakubwa kutokana na vitendo vya uharamia




    (e) Ukirejelea kifungu, eleza maana ya:
    (i) uharamia ………………………………………………………………………………….
    (ii) mtandao …………………………………………………………………………………
    (iii) mwambao ………………………………………………………………………………

    Date posted: February 22, 2018 .    Answers (1)

  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. T. Arege: Barabara Barabara bado ni ndefu Nami tayari nimechoka tiki Natamani kuketi Ninyooshe misuli Nituliza akili. Lakini Azma yanisukuma Mbele ikinihimiza kuendelea Baada ya miinuko... (Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
    T. Arege: Barabara
    Barabara bado ni ndefu
    Nami tayari nimechoka tiki
    Natamani kuketi
    Ninyooshe misuli
    Nituliza akili.
    Lakini
    Azma yanisukuma
    Mbele ikinihimiza kuendelea
    Baada ya miinuko na kuruha
    Sasa naona unyoofu wake
    Unyoofu ambao unatisha zaidi.
    Punde natumbukia katika shimo
    Nahitaji siha zaidi ili kupanda tena
    Ghafla nakumbuka ilivyosema
    lie sauti zamani kidogo
    "Kuwa tayari kupanda na kushuka
    Ingawa nimechoka
    Jambo moja li dhahiri
    Lazima nifuate barabara
    Ingawa machweo yaingia
    Nizame na kuibuka
    Nipande na kushuka.
    Jambo moja nakukumbukia:
    Mungu Je, nimwombe tena?
    Hadi lini? Labda amechoshwa na ombaomba zangu
    Nashangaa tena!
    Kitu kimoja nakiamini
    Lazima niendelee kijitahidi kwa kila hatua mpya
    Nijikokote kuiandama hii barabara yenye ukungu
    Nikinaswa na kujinasua
    Yumkini nitafika mwisho wake
    Ingawa wangu mwisho haitauwahi kabla.
    (a) Eleza toni ya shairi hili.
    B)Mshairi ana maana gani anaposema "Kuwa tayari kupanda na kushuka"
    katika ubeti wa tatu?
    (c) Fafanua tamathali tano za usemi zilizotumiwa katika shairi hili
    ukizitolea mifano mwafaka.
    (d) Eleza ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano wa shairi hili.
    (e) Eleza maana ya:
    (i) kuruba
    (ii) barabara yenye ukungu

    Date posted: February 7, 2018 .    Answers (1)

  • Kwa kutumia mifano mwafaka eleza majukumu matano ya nyimbo katika jamii (Solved)

    Kwa kutumia mifano mwafaka eleza majukumu matano ya nyimbo katika jamii

    Date posted: February 6, 2018 .    Answers (1)

  • Ili kuweza kufanikisha uwasilishaji wa utanzu wa nyimbo kwa hadhira eleza mambo anayohitaji mwimbaji. (Solved)

    Ili kuweza kufanikisha uwasilishaji wa utanzu wa nyimbo kwa hadhira eleza mambo anayohitaji mwimbaji.

    Date posted: February 6, 2018 .    Answers (1)

  • Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali. Kilio cha Lugha Ni wimbo najiimbia, nijiliwaze Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi Lugha ya... (Solved)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
    Kilio cha Lugha
    Ni wimbo najiimbia, nijiliwaze
    Sina wa kusaidia, nasongwa sina nafasi
    Kiwa kwetu naumia, kwengine si mahususi
    Lugha ya mtu mweusi, Kiswahili chalilia
    Wataalamu ni nani, mulipo mwaninyanyasa
    Hamna nami imani, wala kupanga siasa,
    Mwasema sayansini, siku ningalitosa,
    Mwanambia nikotosa, kuiva sijafika.
    Ela muelewe sana, Maamuma na Imamu,
    Mulipokuwa vijana, kwenu nilikuwa timamu,
    Sasa mumesoma sana, mwaniona ni haramu,
    Mujue kuwa dawamu, utumwa mwauridhia.
    Mzaliwapo mwalia, 'maa', maneno ya kwanza,
    Lugha munayokulia, ya mama zetu ya kwanza,
    Wa lugha muwedoria, muweze na kuikuza,
    Sio kujipendekeza, uzungu kuigiza.
    Majira ya ukoloni, ukombozi kusambaza,
    Lugha mulithamini, Kiswahili kufukiza,
    Hata kule risavuni, kizungu hanikuwaza,
    Sasa mbona mwanibeza, mbali mwanitupilia?
    Sayansi sio asili, msamiatiwe sinao,
    Sayansi yataka mbali, msamiati ni wa hao
    Nitakuwa Kiswahili, kiomba majina yao
    Lugha kujikuza kwao, huomba linalofaa.
    Enyi viongozi wetu ipangeni nadharia,
    Kujenga siasa yetu, tuzidi kuwa huria
    Lugha hata 'mbusha watu, tuche kuriaria,
    Sifa ni kwa chake mtu, cha mwenzi hutoringia.
    Utajiri wangu hasa, nikiwatajia wote,
    Msamiati huwa, ni wa Afrika yote,
    Na methali za kuasa, nahau na ngeli zote,
    Na nisemwapo popote, ujumbe hukamilika.
    Afrika ndipo petu, pa wabantu halisi,
    Baba na mama ni Bantu, shina la wangu ukwasi,
    Warabu na wengi wetu, sio wangu Adinasi
    Kwao 'meomba kiasi, ili kujizidisha.
    Mfumo mpya hongera, wa elimu humu Kenya,
    Lugha takuwa imara, ukabila tutafinya,
    Kiswahili ni ibara, kila mtu kiimanya,
    Methali imetuonya, mtumwa si mwasilia
    Tamati lugha yalia, yabaguliwa bayana,
    Kukua imeridhia, msamiati kufana,
    Wengine wataijulia, kwa marefu na mapana,
    Lugha yenu ya maana, mwaipuuza yalia.
    (a) Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu.
    (b) Kwa kutoa hoja ime, eleza kwa nini shairi hili likaitwa kilio cha lugha.
    (c) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari.
    (d) Eleza toni ya shairi hili.
    (e) Tambua uhuru wa kishairi uliotumiwa kwa kurejelea mifano milatu.
    F)Bainisha nafsineni katika shairi.
    G)Eleza maana ya maneno yafuatayo kwa mujibu wa shairi.
    (i) nasongwa
    (ii) kuriaria
    (iii) adinasi

    Date posted: February 6, 2018 .    Answers (1)

  • Fafanua mjukumu ya elimu na dini katika jamii kwa mujibu wa riwaya: Kidagaa Kimemwozea. (Solved)

    Fafanua mjukumu ya elimu na dini katika jamii kwa mujibu wa riwaya:
    Kidagaa Kimemwozea.

    Date posted: February 6, 2018 .    Answers (1)

  • Jadili dhima ya fasihi katika jamii (Solved)

    Jadili dhima ya fasihi katika jamii

    Date posted: February 6, 2018 .    Answers (1)

  • Fafanua sifa za Kenga kama zinavyojitokeza wazi katika tamthilia ya kigogo. (Solved)

    Fafanua sifa za Kenga kama zinavyojitokeza wazi katika tamthilia ya kigogo.

    Date posted: January 31, 2018 .    Answers (1)

  • Eleza changamoto zilizoukabili usanifishaji wa kiswahili. (Solved)

    Eleza changamoto zilizoukabili usanifishaji wa kiswahili.

    Date posted: January 30, 2018 .    Answers (1)

  • Je, miviga ina upungufu gani? (Solved)

    Je, miviga ina upungufu gani

    Date posted: January 17, 2018 .    Answers (1)

  • Fafanua kikamilifu dhana zifuatazo za fasihi simulizi i) Nyiso ii) Mbolezi iii) Hodiya iv) Bembelezi v) Sifo (Solved)

    Fafanua kikamilifu dhana zifuatazo za fasihi simulizi
    i) Nyiso
    ii) Mbolezi
    iii) Hodiya
    iv) Bembelezi
    v) Sifo

    Date posted: January 17, 2018 .    Answers (1)

  • Andika katika usemi wa taarifa “Karibu Bakari, tafadhali kaa”, Maimuna alisema. “Asante, je, habari za nyumbani?” Bakari aliuliza (Solved)

    Andika katika usemi wa taarifa
    “Karibu Bakari, tafadhali kaa”, Maimuna alisema. “Asante, je, habari za nyumbani?” Bakari aliuliza

    Date posted: January 17, 2018 .    Answers (1)

  • Andika kwa wingi Wimbi hilo la maji lilimhofisha mvuvi akashindwa kutupa wavu wake majini. (Solved)

    Andika kwa wingi
    Wimbi hilo la maji lilimhofisha mvuvi akashindwa kutupa wavu wake majini.

    Date posted: January 17, 2018 .    Answers (1)

  • Andika upya sentensi ifuatayo ukitumia virejeshi vya tamati: Mwanafunzi anayefanikiwa maishani ni yule anayesoma kwa bidii na pia anayewatii wazazi wake. (Solved)

    Andika upya sentensi ifuatayo ukitumia virejeshi vya tamati:
    Mwanafunzi anayefanikiwa maishani ni yule anayesoma kwa bidii na pia anayewatii wazazi wake.

    Date posted: January 16, 2018 .    Answers (1)

  • Onyesha chagizo katika sentensi ifuatayo Watu wanne walipeperushwa juu kwa juu na upepo mkali (Solved)

    Onyesha chagizo katika sentensi ifuatayo
    Watu wanne walipeperushwa juu kwa juu na upepo mkali

    Date posted: January 16, 2018 .    Answers (1)

  • Unda nomino kutokana na kivumishi:refu (Solved)

    Unda nomino kutokana na kivumishi:refu

    Date posted: January 16, 2018 .    Answers (1)

  • Akifisha Mtume asimame nusura aingie kwenye shimo la taka. (Solved)

    Akifisha
    Mtume asimame nusura aingie kwenye shimo la taka.

    Date posted: January 16, 2018 .    Answers (1)