kiswahili ni lugha ya kibantu. Jadili.

      

Asili ya lugha ya Kiswahili

  

Answers


mary
UTANGULIZI
Kuna vyanzo vingi vinavyodhibitisha kuwa kiswahili ni lugha ya kibantu. vyanzo hivi ni pamoja na:
a) Umaeneo wa kiswahili
b) Unasaba
c) Umuundo wa kiswahili
d) Historia mapokeo na historia andishi ya kiswahili.
Kimaeneo kiswahili kinazungumzwa kusini mwa Ikweta kama lugha zingine za kibantu. Mtafiti wa lugha za kibantu Bleek (1862) alisema kwamba lugha za kibantu huzungumzwa kusini mwa Ikweta. Mtaalamu huyu aliziona lugha za kibantu kama zilizo na mzizi (ntu) katika kutajia binadamu. mfano:
lugha umoja wingi
Kikissi omunto avanto
Kikikuyu mundu andu
Kizulu munho wanhu
Kiswahili mtu watu
Kutokana na mifano hii inadhihirika wazi kwamba Kiswahili, Kikissi,Kikikuyu na Kizulu ni lugha za kibantu kwa kuwa lugha hizi zote zina mzizi (ntu) katika kumtajia binadamu.
Mtafiti mwingine kwa jina Malkon Guthrie (1948) katika tafiti zake ziitwazo "Comparative Bantu" anazidi kuonyesha jinsi kiswahili ni lugha ya kibantu kimuundo.. Mtafiti huyu anazilinganisha lugha mia mbili za kibantu kwenye swala la mashina ya maneno yapatayo 22,000. aligudua kwamba mashina 2300 yalifanana katika lugha tofauti tofauti za kibantu.Katika utafiti wake anagudua kuwa Kiswahili ni lugha ya kibantu kama kilivyo Kizulu.
Kulinganishwa kwa msamiati wa kimsingi ni kigezo kingine kinachoweza kutumika kudhibitisha kwamba Kiswahili ni lugha ya kibantu.Msamiati wa kimsingi ni ule msamiati ambao unatumiwa kutajia vitu vya kimsingi katika mazingira ya binadamu kama vile sehemu za mwili, maumbile ya kijeografia baadhi ya zinginezo.Msamiati wa kimsingi katika kiswahili unaingiliana na msamiati wa lugha zingine za kibantu. Kwa mfano:
lugha msamiati wa kisingi
Kikuria amache
Kimeru rujji
Kisawhili maji
Kikalejin pek
Kiluo pi
Kutokana na mfano huu ni wazi kwamba kisawhili, kimeru na kikuria vina mwingiliano wa karibu sana.Kikuria na Kimeru zinaorodheshwa kama lugha za kibantu vivyo hivyo ni wazi kuwa Kiswahili ni lugha ya kibantu pia.
Myambuliko wa vitenzi unaweza kutumika pia katika kuonyesha ubantu wa kiswahili kwa sababu mnyambuliko wa vitenzi katika lugha za kibantu kikiwemo kiswahili huchukua ruwaza maalam. Mfano
kiswahili fanya fanyana fanyia fanyika
kikikuyu ika ikana ikira ikika
kikissi kora korana korera koreka
kijaluo timo timo timne timore
Mfano huu unadhibitisha kwamba kisawhili kinanyambuliwa kufuatia ruwaza sawa na za lugha zingine za kibantu.
Hoja nyingine ni kwamba kiswahili kama lugha zingine za kibantu ni lugha ambishi bainishi. lugha ambazo ni ambishi bainishi ni lugha ambazo zinaruhusu kuongezwa viambishi mbali mbali katika maneno yake. Mfano
lugha neno viambishaji
Kikamba kaseo museo,tuseo,aseo,kiseo
Kikikuyu mwana ciana,twana, mana,kana
Kiswahili toto mtoto, watoto, kitoto, jitoto, vitoto
Lugha za kibantu huwa na tabia ya kuwa na upatanisho wa kisarufi kwa kufuata ngeli za maneno. hali kama hii hukikumba kiswahili na inaweza kutumiwa kudhibitisha kuwa kweli kiswahili ni lugha ya kibantu.Mfano
lugha mfano
Kikikuyu Ifuku riri ni rinene.
Kikissi Ikitabu iki ni kinene.
Kiswahili Kitabu hiki ni kikubwa.
Idadi ya vokali inaweza kutumika kuonyesha mahusiano baina ya kugha mbali mbali. kwa kutumia kigezo hiki, kiswahili kinajidhihirisha kama lugha yakibantu.Lugha za kibantu zina vokali za kimsingi kati ya tano na saba. Kiswahili kina vokali tano ambazo ni; a e i o u. Kikamba na kikuyu zina vokali saba. Kiarabu ambacho kinadaiwa kuwa ndicho msingi wa kiswahili kina vokali tatu pekee.
HITIMISHO
Kutokana na mifano migi ambayo tumeiona ni wazi kuwa kiswahili ni lugha ya kibantu hata ikiwa kuna baadhi ya watu ambao bado wanapinga wazo hili.

maryann1 answered the question on March 22, 2018 at 20:11


Next: Explain the process of fertilization in human beings
Previous: Why is the education system re-introducing technical and pre-vocational education that has been abandoned after independence?

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions