Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Je, ni sababu zipi zilizopelekea kusanifishwa kwa kiswahili?

      

Je, ni sababu zipi zilizopelekea kusanifishwa kwa kiswahili?

  

Answers


mary
Kuna sababu nyingi ambazo zinapelekea kusanifishwa kwa Kiswahili.Tutazitazama tatu kati ya hizo na mbazo zina mashiko zaidi.
a) Wingi wa lahaja uswahilini.
Lugha ya Kiswahili ina zaidi ya lahaja kumi na nane na ambazo ni za pwani, visiwani na bara. Kutokana na wingi huu wa lahaja, mawasiliano katika kiswahili yalikumbwa na matatizo na yakatatanisha hivi kwamba akiwa watu wawili wanatumia lahaja mbili tofauti, ni nani kati yao atasema anakitumia Kiswahili hasa na mazungumzo yao ni tofauti? Ili kuondoa tatizo hili la kimawasiliano, ilibidi Kiswahili kisanifishe kwa kutafuta lahaja moja ambayo ingetumiwa kama ya wasastani na kipimo cah ubora wa Kiswahili kote duniani.
b) Tume ya Elimu ya Phelps-Stokes
Tume hii iliyojumulisha wanaelimu ilikuja Afrika kutoka Uimgereza ikiwa na jukumu la kutathmini elimu ya mwafrika. Walipendekeza kuwa elimu ingemfaa Mwafrika ikiwa atafunzwa kwa lugha yake asilia. Lakini ikawa vigumu kwa serikali ya Uingereza kutekeleza pendekezo hili kutokana na wingi wa lugha Afrika. Hata hivyo walipofika Afrika Mashariki walipata Kiswahili kikiwa kimeenea sana kiwango cha kuwa lingua-franka, hivyo wangeweza kukitumia Kiswahili kama lugha ya kufunzia. Hata hivyo Kiswahili kilikuwa na lahaja nyingi na ili kitumike vyema katika elimu ilifaa kisanifishwe . mapendekezo ya tume hii yalipelekea kusanifishwa kwa lugha ya Kiswahili.
c) Mapinduzi ya viwandani.
Hili ni tukio la kihistoria lililozipitikia nchi za Bara Uropa. Tukio hili lilizalisha viwanada ambapo kazi nyingi zilizokuwa zikifanya na binabamu zilianza kufanywa kwa matumizi ya mashine. Kupitia hali hii bidhaa zilizalishwa kwa wingi sana. Kwa sababu ya bidhaa nyingi zilizozalishwa kulihitajika soko na pia malighafi ya kutumika kwa ajili ya viwanda hivyo, Afrika ilitokea kuwa sehemu moja ya kutekeleza haya. Wageni hao walipotua pwani ya Afrika mashariki walijifunza Kiswahili kwani ndicho kilichokuwa kama ufunguo. Hata hivyo lahaja walizojifunza zilikua tofauti kulingana na pale ambapo mtu alitua. Wageni hao walipopatana wlizungumza Kiswahili cha mgongano na hili likapelekea kuanzishwa kwa mchakato mzima wa kusanifisha Kiswahili.
Hizi si sababu pekee zilizopelekea kusanifishwa kwa Kiswahili lakini hoja hizi zina mashiko zaidi.

maryann1 answered the question on March 23, 2018 at 12:06


Next: (a) What is trade liberalization? (b) Highlight the merits and demerits of liberalization?
Previous: What is the essence of philosophy to Kenya?

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions