Jadili maudhui ya tamaa katika tamthilia ya Kigogo

      

Jadili maudhui ya tamaa katika tamthilia ya Kigogo.

  

Answers


ESTHER
Tamaa imejitokeza Kwa njia tofauti tofauti katika Tamthilia ya Kigogo
Majoka ana tamaa ya uongozi, hataki kuondoka mamlakani. Anafanya kila awezalo kuondoa wapinzani wake kama Jabali. Anapigana na akina Tunu na Sudi ili asalie uongozini.

Anataka kumtambulisha Ngao Junior rasmi kuwa mrithi wake kwenye siasa.
Majoka anadai kuwa hata asipopigigwa kura moja atashinda. Ana tamaa ya uongozi.

Majoka ana tamaa ya mali, ananyakua uwanja wa soko ili kujenga hoteli ya kifahari ilhali tayari ana nyingine.

Majoka anawafisidi wananchi ili kujilimbikizia mali kwa sababu ya tamaa

Mamapima ana tamaa ya mali, anawapunja walevi na kuwauzia pombe haramu inayowadhuru. Hajali maana anaongozwa na tamaa ya mali.

Husda ana tamaa ya mali, anaolewa na Majoka kwa sababu ya mali yake.

Tamaa inamtawala Ashua hadi anaomba talaka. Anadai amachoka kupendwa kimaskini kwa kuongozwa na tamaa ya mali.

Akina Boza, Kombe na Ngurumo ni wenye tamaa. Wanajipendekeza Kwa viongozi ili wanufaike Kwa miradi na kandarasi.

ESTHER STEVE answered the question on April 13, 2018 at 18:56


Next: Who was the longest serving cabinet secretary in Kenya?
Previous: Define microbial generation time

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions