Kwa kutoa mifano yoyote Kumi, fafanua matumizi ya nyimbo katika Tamthilia ya Kigogo

      

Kwa kutoa mifano yoyote Kumi, fafanua matumizi ya nyimbo katika Tamthilia ya Kigogo.

  

Answers


ESTHER
WIMBO WA UZALENDO.
Wimbo huu unaimbwa katika kituo cha habari cha wazalendo, ni wimbo unaosifu Sagamoyo na kiongozi wake kuwa;

Sagamoyo ni jimbo tukufu, wanamtukuza Ngao kuwa kiongozi shupavu.
Maudhui katika wimbo huu ni kinaya kwa vile Majoka sio kiongozi shupavu, uongozi wake una dosari. (uk5)

WIMBO WA HASHIMA.
Anaimba wimbo huu akiwa nyumbani kwake. Wimbo huu unaashiria kuwa mambo hubadilika, kila siku wasema heri yalipita jana. (uk51)

WIMBO WA MAMAPIMA.
Ni wimbo wa kishairi unaorejela Sudi na Tunu. Mamapima anawashauri wajipe raha kwa kujiunga nao katika ulevi. (uk60)

WIMBO WA NGURUMO.
Ngurumo anaimba wimbo kwa mamapima akimrejelea Tunu. Ni wimbo wa kumsuta Tunu kwa kuwa yeye ni mwanamke anapaswa kuolewa.

WIMBO WA UMATI.
Umati unaimba wimbo katika lango la soko la chapakazi. Watu wanaimba kuwa yote yanawezekana bila Majoka. Wimbo huu unasifia juhudi za Tunu kuikomboa Sagamoyo na kuleta uhuru halisi.

WIMBO WA ASHUA.
Ashua anaimba kuwa soko lafunguliwa bila chopi kumaanishwa vikaragosi hawana nguvu dhidhi ya wanamapinduzi. (uk92)
ESTHER STEVE answered the question on April 13, 2018 at 19:18


Next: Explain the maslow’s hierarchy of needs theory.
Previous: Give three forces that give the earth it's oblate shape

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions