Eleza shinda zinazokumba lugha ya kiswahili katika jamii

      

Eleza shinda zinazokumba lugha ya kiswahili katika jamii.

  

Answers


Mageto
1.Kiswahili kimepewa vipindi vichache ikilinganishwa na kiingereza-hivi imeathiri matumizi ya lugja ya kiswahili.
2.Athari ya lugha asili/lugha ya mama-katika mazungumzo watu hupenda kutumia lugha ya kwanza ambayo si kiswahili kwa ajili ya kuelewana.hivi basi lugha ya kiswahili haisambai katika maeneo mengi.
3.Chimbuko la sheng'-kuibuka kwa sheng' kama lugha ya mazungumzo imeathiri maendelezo ya kiswahili,hivi kwamba msamiati wa kiswahili unaotumiwa ni finyu mno.
4.Ukosefu wa utafiti katika lugha ya kiswahili-wasomi wachache sana wanafanya utafiti katika sarufi ya lugha ya kiswahili kwa ujumla.Kutokana na tatizo hili kiswahili hakijaweza kusambaa katika maeneo mengi.
5.Dhana potovu kwamba kiswahili ni cha adhi ya chini ikilinganishwa na kiingereza-watu wana dhana kuwa kiingereza kina ustaarabu ikilinganishwa na kiswahili. Kwa hivyo hupenda kukitumia kiingereza Mara kwa Mara katika mazungumzo rasmi kama vile kuwasilisha miswada bungeni.Hiyo basi tatizo hili limeathiri maenezo ya kiswahili
Real Educator answered the question on April 20, 2018 at 08:51


Next: Explain ways in which the Kenyan government promotes culture today
Previous: 

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions