Jadili mbinu anazotumia Majoka kudumu uongozini

      

Jadili mbinu anazotumia Majoka kudumu uongozini.

  

Answers


ESTHER
Mbinu anazotumia Majoka kungoza Sagamoyo

Uvumi. Watu wa Majoka wanaeneza uvumi kuwa Sudi na Ashua ndio wanawinda roho ya Tunu ili kuwatenganisha.

Ahadi za uongo. Madai ya Majoka kuwa atatoa chakula kwa wasiojiweza si ya kweli.
Kenga mshauri wa Majoka anawashawishi Sudi kuchonga kinyago cha Ngao ili apate malipo mazuri na maisha yake kubadilika. Kuwa jina lake litashamiri na apate tuzo nyingi zaidi ya hayo apate likizo ya mwezi mzima ughaibuni. Ahadi hizi zote ni za uongo.

Zawadi. Kenga anawaletea Sudi, Boza na Kombe zawadi ya keki kuwafumba ili wamuunge mkono Majoka.

Vitisho. Wanasagamoyo wanatishwa kwa kurushiwa vijikaratasi wahame.

Majoka anatumia polisi kuwatisha wanasagamoyo. Matokeo yake ni watu kuhofia usalama wao.

Majoka anamtishia Chopi kuwa atamwaga unga wake kwa kutowaamrisha polisi kutawanya waandamanaji.

Mapendeleo. Ashua baada ya kufuzu kutoka chuo kikuu alipewa kazi katika Majoka and Majoka academy akakataa, sasa angekuwa mwalimu mkuu katika mojawapo ya shule za kifahari, viongozi hupendelea wengine kutumia njia Zisizo halali.

Majoka alimpa Tunu kazi kiwandani akakataa.


Jela. Viongozi hufungia wanaowapinga jela. Ashua anatiwa ndani, kuna washukiwa wengi ndani.

Polisi. Majoka anatumia polisi kutawanya waandamanahi wanaodai haki zao.

Viongozi hutumia nguvu. Majoka anadai wafadhili wa wapinzani lazima wavunje kambi zao Sagamoyo, kuwa Sagamoyo yajiweza.
Anapanga kumkomesha Tunu dhidi ya kuongoza maandamano kutumia nguvu zake kiutawala.
Kenga anamshauri Majoka atangaze maandamano ni haramu kwa mutumia nguvu kisha maafisa wa polisi watumie nguvu zaidi.

Ulaghai. Majoka anapanga kuongeza mishahara ya waalimu na wauguzi kwa asilimia kidogo kisha apandishe kodi.

Kudhibiti vyombo vya habari . Majoka anapanga kufunga vituo vya runinga sagamoyo ili abakie na vichache anavyotaka vya kutangaza habari anazotaka.

Wavamizi. Majoka anatumia wavamizi, Tunu anaumizwa mfupa wa muundi, ana majeraha kutokana na uvamizi.

Ulinzi mkali. Majoka na watu wake wana ulinzi mkali. Kenga ana walinzi, Majoka analindwa na maafisa wa polisi.

Tunu na watu wake wanafurushwa wanapojaribu kukaribia soko la Chapakazi.

Kufuta kazi wasiomuunga. Majoka anamfuta kazi kingi kwa kutomtii kupiga watu risasi sokoni Chapakazi.

ESTHER STEVE answered the question on April 20, 2018 at 05:24


Next: State uses of radio isotopes in the following: 1. Medicine 2. Agriculture 3. Industries
Previous: Give and illustrate character traits of Taiyo and Joseph Parmuat in the story Blossoms of the Savannah

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions