Utengano wa kitabaka umechangia kuwepo Kwa dhuluma barani Afrika. Ukirejelea hadithi zifuatazo katika diwani ya Tumbo lisiloshiba, Dhibitisha. 1.Tumbo lisiloshiba 2.shibe inatumaliza 3....

      

Utengano wa kitabaka umechangia kuwepo Kwa dhuluma barani Afrika. Ukirejelea hadithi zifuatazo katika diwani ya Tumbo lisiloshiba, Dhibitisha. 1.Tumbo lisiloshiba 2.shibe inatumaliza...

  

Answers


ESTHER
Kudhulumu ni kunyanyasa au kumnyima mtu Haki. Hadithi nyingi katika diwani ya Tumbo lisiloshiba zimeangazia aina tofauti za dhuluma. Msingi wa dhuluma hizi ni tofauti za kitabaka.
Katika hadithi ya Tumbo lisiloshiba, tabaka la juu(viongozi) linalowakilishwa na jitu lenye tumbo lisiloshiba linadhulumu watu wa tabaka la chini. ( Wanamadongoporomoka) hawa hawahusishwi katika shughuli za kubomomoa vibanda vyao. Vinabomolewa pasipo hata na mpango wa njihia kuwahamishia mahala kwingineko. Kuwanyima haki ya kumiliki ardhi na kuwabomolea vibanda ni dhuluma.

Katika hadithi ya Shibe inatumaliza, viongozi wanawadhulumu wanananchi. Dawa zinazostahili kuwa za bure Kwa raia zinalipiwa Kwa kuwa zimeuziwa marafiki wa viongozi. Viongozi wanakula na kunywa watakavyo huku raia wakiangamizwa na njaa na umaskini.

Katika hadithi ya Kidege Midege mikubwa inayoashiria tabaka la juu (viongozi) inaidhulumu videge vidogo na visamaki ( tabaka la chini) Midege hii inakula visamaki kidibwini na kuharibu mazingira bila kujali wanaoathiriwa na tabia hii. Hii ni dhuluma.

Hadithi ya Tulipokutana tena inaonyesha dhuluma wanazopitia watoto wa kimaskini. Hawa wamenyimwa takriban haki zote za watoto. Bogoa anadhulumiwa na mlezi wake WA tabaka la juu. Hapati lishe bora, elimu, mavazi, makazi mema, muda wa kucheza na anafanyishwa Kazi za sulubu. Hii ni dhuluma

Katika hadithi ya ndoto ya Mashaka, dhuluma imejitokeza. Watu wa Tandale wameachwa kuishi maisha duni katika mitaa ya mabadani. Viongozi wamewatelekeza, hawana huduma za kimsingi kama maji Safi.
ESTHER STEVE answered the question on April 21, 2018 at 17:55


Next: What are the problems facing the Kenya’s economy?
Previous: What are the major steps in designing a customer/market driven marketing strategy?

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions