Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Utawala mbaya ni tatizo kuu linalozikumba nchi nyingi za kiafrika. Jadili kwa kurejelea matukio mbalimbali katika tamthilia ya kigogo

      

Utawala mbaya ni tatizo kuu linalozikumba nchi nyingi za kiafrika. Jadili kwa kurejelea matukio mbalimbali katika tamthilia ya kigogo.

  

Answers


ESTHER
Maudhui ya uongozi mbaya yameshamiri katika tamthilia hii.

Viongozi wa Sagamoyo hawajali umma wanaoutumikia. Wamekosa kuwajibika kazini na wanaongozwa na tamaa ya mali na ubinafsi. Majoka: Kigogo wa Sagamoyo, anaishi maisha ya kifahari. Ana kampuni kubwa Sagamoyo ya kutengeneza sumu ya nyoka, ana hoteli kubwa ya kifahari na shule ya kibinafsi. Ana hela za kutosha kuenda kubarizi pamoja na mkewe katika hoteli yake ya kifahari.

Kwa upande mwingine, wananchi wanateseka. Hali Sagamoyo ni ya kusikitisha na kuvunja moyo. Jazanda ya keki ya taifa inaakisi hali halisi Sagamoyo. Sio kila mtu huipata.

Huduma muhimu hazipo Sagamoyo. Baadhi ya mambo anayoyatetea Tunu ni kuwepo kwa barabara, elimu, hospitali, vyoo, nguvu za umeme na ajira kwa vijana. Ukosefu wa huduma hizi unadhihirisha uongozi mbaya.
Soko la Chapakazi wanakofanyia kazi wachochole ni chafu. Hili halikutarajiwa ikizingatiwa kuwa wanatozwa kodi ya juu, na si kodi tu bali hata hongo. Kodi inatumiwa kuwafaidi viongozi na ndio maana hakuna hela za kusafisha soko. Soko limegeuzwa jaa la taka na kemikali na watu wanaugua magonjwa anuwai kutokana na hili.

Majoka analifunga soko la Sagamoyo. Wananchi hupata riziki yao hapa na hivyo kulifunga kunawalemaza. Sudi kwa mfano ameshindwa kuikimu familia kwa kuwa hana mahali pa kuuzia vinyago. Tunaona mwanawe akilia njaa. Hawakula chochote usiku na hawakupata kiamsha kinywa. Majoka amehodhi soko hili ili ajenge hoteli ya kifahari na sehemu nyingine akammegea mshauri wake wa karibu: Kenga

Vijana waliosoma hawapati kazi ya maana. Sudi kwa mfano anachonga vinyago japo amesoma hadi chuo kikuu. Tunu ana hata shahada ya uzamili na hana kazi. Kazi Sagamoyo zinatolewa kwa njia ya ufisadi. Majoka amewahi kuwaahidi Tunu na Ashua kazi katika shule na kampuni yake mtawalia wakaikataa kwa kuwa ni wazalendo halisi.

Waliopata kazi wanalipwa mishahara duni. Walimu na wauguzi kwa mfano wamekuwa kwenye migomo ya kutaka nyongeza ya ajira. Wanaongezewa hela chache na kisha kodi inapandishwa.
Haki haipo Sagamoyo, Ashua anamlaumu Majoka kuwa anawafanya wanafunzi makabeji kwa kudungwa sumu ya nyoka lakini Majoka anajitapa kuwa hakuna ushahidi. Japo uko, kwa vile yeye ni kiongozi hawezi akachukuliwa hatua. Kama anavyosema Ashua, ushahidi hauwezi ukapatikana katika kesi ya kuku iwapo kipanga ndiye hakimu.

katiba na sheria za jimbo la Sagamoyo hazifuatwi. Katiba imepiga marufuku uuzaji wa pombe haramu kwa mfano, lakini Mamapima anaiuza na mwenyewe anasema ana kibali kutoka kwa Majoka mwenyewe.
Viongozi wanachukua mikopo kutoka nchi za magharibi itakayolipwa kwa muda mrefu. Wananchi wanaofanya kazi za sulubu na hata vizazi vya kesho ndio wanatwikwa mzigo wa kulipa madeni ambayo hata hawakuona manufaa yake.

Majoka hawajali wananchi hata kidogo. Tayari nchi ina njaa na mazao yamepungua kama anavyoeleza Hashima uk 51. Kinaya ni kuwa Majoka anafungulia biashara ya ukataji miti tena. Hili litazidisha ukame na hivyo njaa itaongezeka.

Uongozi wa Majoka ni wa kidikteta na kimabavu. Majoka hakubali upinzani wowote ule. Tunaona anavyowahangaisha Sudi na Tunu. Sudi amewahi kufungwa gerezani uk 46. Tunu naye alivamiwa na Ngurumo uk 63. Bila shaka Ngurumo alitumwa na Majoka kumuua lakini akabahatika katika kile Majoka anadhani ni mapuuza ya Chopi. Ngurumo anauawa baadaye kwa amri ya Majoka pia ili kuficha ushahidi wa uozo wake. Majoka pia alimuua mpinzani wake wa awali: Jabali wa chama cha mwenge uk 34. Vyombo vya habari vinavyotangaza mambo yalivyo vinatishiwa kufungwa kama vile sauti ya mzalendo. Anataka matangazo na habari zimfae yeye.

Majoka anatumia mbinu anuwai kuendeleza uongozi mbaya. Vibaraka na washauri wabaya wanammiminia sifa za uongo badala ya kumkosoa. Boza kwa mfano anatetea uamuzi wa kusherehekea uhuru kwa mwezi mzima kwa kusema Majoka atawalisha wasiojiweza. Huu ni uongo na Boza alifaa kutambua kuwa kutofanya kazi mwezi mzima kutafanya uchumi kuzorota na njaa kuongezeka. Hatambui kuwa Majoka anaijali nasfi yake tu.
Majoka anatumia hongo ili wananchi wazidi kumtumikia. Mfano anammegea Kenga kipande cha ardhi sokoni. Vibaraka wake pia wanapata kandarasi kama vile Ngurumo na mkewe Boza.
Majoka pia anaeneza propaganda au uvumi wa uongo ili kujifaa yeye. Kwa mfano kusema Sudi ndiye anamvamia Tunu ili kuwatawanya. Vitisho na kuwatia wananchi woga ni njia nyingine anayotumia Majoka kuendeleza uongozi mbaya. Uk51.

Kuna ukabila katika Jimbo la Sagamoyo. Akina Kombe wanapokezwa vijibarua vya kulihama Jimbo la Sagamoyo.
Majoka anajua jinsi ya kucheza siasa ili kudumisha uongozi wake mbaya. Kwa mfano, makaburi yamejaa na Ngurumo hana pa kuzikwa. Majoka anapendekeza azikwe juu ya mwingine(ukatili ulioje!) anaelewa hili litampaka tope na hivyo anaamuru chatu auwawe maana anajua wakereketwa wa mazingira wataandamana na hivyo vyombo vya habari vitaelekezwa huko.

Maandamano ni ishara ya uongozi mbaya. Wanasagamoyo wanaandamana kutetea haki zao. Hata hivyo, hakuna haki ya kujieleza Sagamoyo. Askari badala ya kuwalinda raia wanatumiwa na Majoka kuwatawanya wanaoandamana. Hawafanyi hivi kwa amani na wengi wanaumia na hata kufa kwa kupigwa risasi. Vitoa machozi vinatumika. Wapinzani wa Majoka pia wanatiwa ndani na kuteswa. Vyombo vya dola hivyo vinatumiwa kuendeleza uongozi mbaya.

ESTHER STEVE answered the question on April 28, 2018 at 16:02


Next: Under what circumstance is a person considered a pro non grata?
Previous: Describe the procedure of carrying out a field study

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions