(a) Eleza maana ya mivigo na inakotumika (b) Eleza sifa za miviga (c) Onyesha umuhimu wa miviga.

      

(a) Eleza maana ya mivigo na inakotumika
(b) Eleza sifa za miviga
(c) Onyesha umuhimu wa miviga.

  

Answers


Edith
a I.) Mivigo ni sherehe au bada zinazofuata utaratibu Fulani wa kisanaa za maonyesho ya fasihi simulizi.

II.) Inakotumiwa
- Katika matanga miviga hutumiwa kuliwaza waliofiwa.
- Katika jando na unyago, makunguni, maghariba na manyakanga hutumia miviga kufunza wavi, nasaha na mazingira yao.
- Katika mavuno miviga hutumiwa kutoa shukrani.
- Baada ya vita; hutumiwa kuongoa na kuwatolea shukrani mashujaa waliotoka vitani.
- Mtoto anapozaliwa au kupewa jina, miviga ya kumkaribisha ilifanywa.
- Wakati wa arusi.
- Matambiko ya kutakasa kama aliyemuua mtu.
- Kutawaza kwa viongozi.

b.) Sifa za miviga.
- Hulenga kundi maalum natoka jamii.
- Hutoa mawaidha.
- Hutokea kwa misimu.
- Hukusanya wanaotoa mawaidha na wanaotolewa hayo mawaidha.
- Kila tukio au jambo huwa na mivigo yake.

C.) Umuhimu wa miviga.
- Hudumisha mila na utamaduni wa jamii.
- Huwawezesha vijana kuwa na kumbukumbu za kila sherehe ilivyofanywa, wakati na maana take.
- Huelimisha vijana.
- Hutahadharisha kuhusu maovu.
- Huwezesha vijana kuelewa na kufahamu desturi zake.
- Huleta umoja na ushirikiano natoka jamii.
- Huburudisha.
- Hufundisha unyumba na malezi.
- Uhimiza bidii ya kufanya kazi na kujitegemea.
- Huleta maendeleo.
eddynightsy answered the question on April 27, 2018 at 08:24


Next: Citing decided cases, explain the doctrine of “Ultra vires.”
Previous: Eleza umuhimu wa ngomezi.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions