Jadili maudhui ya utabaka katika tamthilia ya Kigogo

      

Jadili maudhui ya utabaka katika tamthilia ya Kigogo.

  

Answers


ESTHER
UTABAKA/UBAGUZI
Utabaka katika jamii ni ile hali ya kugawa jamii kulingana na uwezo wa kiuchumi wa watu. Katika jamii ya Sagamoyo kuna matabaka mawili:
1. viongozi (matajiri)
2. Wananchi na wafanyakazi wa kawaida (maskini)
Ubaguzi ni hali ya kutoa huduma kwa mapendeleo. Tabaka la chini linabaguliwa.
Viongozi wa Sagamoyo ni matajiri. Wanaishi maisha mazuri tena ya hali ya juu. Watoto wao wanasomea shule za ng’ambo kwa mfano Ngao Junior. Viongozi wana hela nyingi na wanastarehe katika hoteli za kifahari.
Licha ya hali ngumu ya maisha, hawa wana pesa nyingi. Wana mashamba makubwa, makampuni, mahoteli na hata shule za kibinafsi. Kwa mfano, mzee Majoka ana kampuni ya Majoka and Majoka, Majoka and Majoka academy na Majoka and Majoka Resort.
Viongozi hawa wanalindwa na askari kila wakati kama vile Majoka analindwa na Chopi na Mwango. Wanaishi katika mazingira safi. Hawakosi maji na hata kunapokuwa na ukame, tayari wamejichimbia visima. Uk.53. Kwa kifupi, maisha yao ni ya raha na starehe za kila aina.
Kwa upande mwingine, tabaka la wachochole ni la raia ambao ndio wengi katika jamii. Maisha yao yamejaa mateso ya kila aina kutokana na tamaa na ubinafsi wa viongozi wao.
Hawa ni maskini hohe hahe.
Wanafanyia kazi katika mazingira chafu kama vile soko la Chapakazi lililogeuzwa jaa la takataka na kemikali. Wanaugua magonjwa ya kila aina kutokana na uchafu huu. Kidogo wanachokichuma kinatwaliwa na viongozi kama kodi na hongo. Soko lao linafungwa ili viongozi wajenge hoteli zaidi za kifahari. Hawana kazi za maana hata kama wengine wamesoma hadi vyuo vikuu kama vile Ashua, Sudi na Tunu. Wanatatizwa na njaa na umaskini. Watoto wa sudi kwa mfano walilala njaa. Hawana wa kuwalinda, askari wanalinda viongozi na kuwadhulumu wananchi.
Utawala umewakandamiza na wanaishi katika woga, njaa na umaskini. Wanabaguliwa katika utoaji wa huduma. Tunu anatetea kuwepo kwa huduma kama vile elimu, barabara, hospitali, maji safi na kadhalika.

ESTHER STEVE answered the question on April 28, 2018 at 15:22


Next: Ichambue jalada ya tamthilia ya Kigogo
Previous: Tamaa inatawala katika Tamthilia ya Kigogo. Dhibitisha

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions