Tamaa inatawala katika Tamthilia ya Kigogo. Dhibitisha

      

Tamaa inatawala katika Tamthilia ya Kigogo. Dhibitisha

  

Answers


ESTHER
Ubinafsi na Tamaa
Ubinafsi ni ile hali ya mtu kutaka kujinufaisha yeye mwenyewe bila kuwajali wengine.Ubinafsi katika tamthilia hii umedhihirika vizuri kupitia kwa viongozi na baadhi ya wananchi ambao ni vibaraka
Viongozi wanahodhi mali ya umma kwa manufaa yao wenyewe na kuwagawia marafiki zao. Majoka amehodhi soko la Chapakazi ili ajenge hoteli ya kifahari na kummegea Kenga sehemu fulani. Majoka tayari ana hoteli nyingine na hivyo hii ni tamaa na ubinafsi. Wanajilimbikizia mali ya umma huku wakiwaacha wananchi kuteseka.
Keki inapookwa, inaliwa na viongozi huku wananchi wakipata makombo kama anavyoyaita Sudi. Huu ni ubinafsi. Boza pia anaonekana mbinafsi, anapopewa kijikeki, anakila peke yake bila kumjali hata bibiye ambaye aliioka.
Ubinafsi unajitokeza pia tunapoona Boza akikosa kuwafahamisha Kombe na Sudi kuhusu mradi wa kuchonga vinyago uliofadhiliwa ili afaidike yeye tu. Kinaya ni kuwa hata hana talanta ya uchongaji.
Mamapima ni mbinafsi, hajali kuuza pombe haramu inayoua vijana na kuwafanya vipofu mradi tu apate pesa.
Ngurumo anadhihirisha ubinafsi. Anafurahia kufungwa kwa soko kwa kuwa vijana waliofanya kazi sokoni wanaenda kulewa kwa kuwa hawana pa kufanyia kazi na hivyo kuongeza faida kwao.
Wenye vioski katika kampuni anakofanya kazi Siti ni wabinafsi. Wana tamaa ya mali. Soko linapofungwa, wanaongeza bei ya chakula maradufu.
Kenga ni mbinafsi. Anajipendekeza kwa Majoka ili apate kufaidika
Tunaona viongozi wakikopa pesa kutoka nchi za nje ili wajifaidi. Hawajali kuwa vizazi vijavyo vitaachiwa mzigo mkubwa sana wa kulipa deni ambalo hata hawakufaidi.
Majoka anatawaliwa na tamaa ya uongozi na ubinafsi. Hakubali kuwepo kwa wapinzani. Aliwahi kumuua kiongozi wa chama cha Mwenge aliyejaribu kumpinga na tunaona akimdhulumu Tunu na hata kupanga njama ya kumuua.
ESTHER STEVE answered the question on April 28, 2018 at 15:26


Next: Jadili maudhui ya utabaka katika tamthilia ya Kigogo
Previous: “Starehe za nyani kuchezea tagaa mbovu nazo ni starehe?” (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Tambua mbinu ya lugha katika dondoo na ueleze maana....

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions