“Starehe za nyani kuchezea tagaa mbovu nazo ni starehe?” (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Tambua mbinu ya lugha katika dondoo na ueleze maana....

      

"Starehe za nyani kuchezea tagaa mbovu nazo ni starehe?"
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Tambua mbinu ya lugha katika dondoo na ueleze maana.
c) Eleza sifa sita za:
i. Msemaji
ii. Msemewa

  

Answers


ESTHER
a. Maneno haya yalisemwa na Tunu. Alikuwa akimsemeza Ngurumo. Ilikuwa kule Mangweni kwa mamapima wanakokutana akina Ngurumo kupiga mtindi. Tunu alikuwa anajaribu kumuonyesha Ngurumo madhara ya pombe haramu ndipo akamwambia aachane na starehe za watu wengine.
b. Kuna jazanda.
Nyani akichezea tagaa mbovu bila shaka huanguka na kuumia. Akina Ngurumo kushiriki unywaji wa pombe haramu ni kama nyani anayechezea tagaa mbovu. Watapata madhara mengi kama vile upofu na vifo.
c. Msemaji ni Tunu. Ana sifa zifuatazo
1. Tunu ni jasiri tena ana msimamo dhabiti. Anasema kuwa hawataulegeza msimamo wao hadi soko lifunguliwe vilevile japo ameumia, anataka kukutana na anaokisia walimuumiza. Anamkabili Majoka kwa ujasiri na kumuita muuaji
2. Tunu ni rafiki wa dhati wa Sudi na mwenye utu. Nia ya kuikomboa Sagamoyo inawaweka pamoja. Tunu anamsaidia Sudi kuwatunza watoto.
3. Mwadilifu. Anahusiana na Sudi kwa heshima kama wakombozi wa Sagamoyo
4. Amezinduka. Anaelewa Sagamoyo haiongozwi ipasavyo na hakubali kuingia katika mitego ya Majoka ya kusitisha juhudi zake za ukombozi
5. Mtetezi wa haki. Anatetea haki za wanasagamoyo kama vile kufunguliwa kwa soko la chapakazi
6. Kiongozi bora. Tunu alikuwa kiongozi tangu akiwa chuoni na baadaye alichaguliwa kuwa Kigogo wa Sagamoyo
Msemewa ni ngurumo. Ana sifa zifuatazo:
1. Ni mlevi: Huenda kwa mamapima kupiga mtindi
2. Ni mkware: anahusiana kimapenzi na Asiya; bibiye Boza
3. Ni katili: anatumiwa na Majoka kumuumiza Tunu
4. Ni kibaraka: Haoni maovu yoyote ya Majoka. Anakubali kutekeleza njama za kihuni za Majoka
5. Ni pumbavu: anaona kunywa pombe haramu kama starehe.
6. Mwenye taasubi ya kiume. Anasema heri ampe paka kura kuliko kumpa Tunu.
ESTHER STEVE answered the question on April 28, 2018 at 15:30


Next: Tamaa inatawala katika Tamthilia ya Kigogo. Dhibitisha
Previous: 1. Eleza maana ya istilahi hii: Usanifishaji 2. Eleza mambo manne yaliyochangia maenezi ya kiswahili kabla ya uhuru.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions