1. Eleza maana ya istilahi hii: Usanifishaji 2. Eleza mambo manne yaliyochangia maenezi ya kiswahili kabla ya uhuru.

      

1. Eleza maana ya istilahi hii: Usanifishaji
2. Eleza mambo manne yaliyochangia maenezi ya kiswahili kabla ya uhuru.

  

Answers


ESTHER
1) Usanifishaji ni uamuzi wa kuchagua lugha moja au mojawapo ya lahaja za lugha na kuifanyia marekebisho ya kimatamshi, kisarufi kimaana na kimaandishi ili iweze kutumika kirasmi.
- Kusanifisha lugha ni kuifanya ikubalike na kutumiwa kwa njia iliyosawa na kila mtu.

2) a) Misafara ya wafanyibiashara baina ya pwani na bara.
b) Utawala wa wakoloni hasa wajerumani waliotumia kiswahili kuwasiliana na watawaliwa.
c) Juhudi za usambazaji wa dini ya Kiislamu na kikristo.
d) Juhudi za serikali za kikoloni kutoa sera zilizokinufaisha kiswahili mfano kamati y a usanifishaji - 1930
e) Matumizi ya lugha ya kiswahili katika vyombo vya habari.
f) Kuibuka kwa waandishi wa kisanii kwa lugha ya kiswahili Sheraban Bin Roberts. (4 x 2 = 8

ESTHER STEVE answered the question on April 28, 2018 at 15:47


Next: “Starehe za nyani kuchezea tagaa mbovu nazo ni starehe?” (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Tambua mbinu ya lugha katika dondoo na ueleze maana....
Previous: (a) Vijana huchangia pakubwa katika kuhujumu maendeleo ya lugha ya kiswahili. Jadili ukweli wa kauli hii ukitoa mifano miwili. (Alama 4) (b) Pendekeza njia tatu ambazo kwazo vijana...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions