(a) Katika jamii huwa wakati mwingine kuna matumizi ya lugha isiyo ya kistaarabu.taja mifano mitano ya lugha ya sampuli hiyo. ( alama 5) (b) Taja mambo matano...

      

(a) Katika jamii huwa wakati mwingine kuna matumizi ya lugha isiyo ya kistaarabu.taja mifano mitano ya lugha ya sampuli hiyo. ( alama 5)

(b) Taja mambo matano yanayoathiri jinsi tunavyoweza kutumia lugha katika jamii(mtindo nafsi na mtu)
MAJIBU

  

Answers


ESTHER
1. (a) - Hutaja sehemu nyeti za mwili wa binadamu k.v za uzazi.
- Hutaja mada pale isisyofaa mf. Kutaja vifo,magonjwa , upimaji wa kinyesi , makamasin.k wakati wa kula.
- Wanataja vilema au walio na udhaifu mbalimbali wakiwepo. Mf. Zeruzeru , kipofu , kiziwi
- Hutumia maneno ya kimatusi k.v mjinga , pumbavu, mshezi. n.k.
- Hutumia lugha ya kulaani . KN Ninakuombea kifo cha haraka au ufutwe kazi. (5 x 1 = 5)
(b) - Hadhira mf. Wale anaowazugumzia kama ni watoto atatumia lugha yenye ucheshi.
- Utungo / matini - kama ni mashairi utatumia lugha yenye ukiushi.
- Tabaka mf. Tabaka la juu wamezoea kingereza hawapendi kwa mfano Kiswahili.
- Hali mf. Chokora wanatumia lugha ya kutisha, mtu akiwa mgonjwa ua mlevi lugha yake huwa tofauti.
- Mada - zile ngumu lugha huwa nyepesi.
- Matilaba - mf Mtu anapotaka wenzake wamuunge mkono atatumia lugha kwa namna ambayo itawavuta kwake.
- Umri - Kundi la kiumri husababisha vilugha mf. Vijana watakuwa na mtindo wao. (5 x 5 = 10)


ESTHER STEVE answered the question on April 30, 2018 at 19:53


Next: (a) Eleza maana ya istilahi zifuatazo za isimu jamii. i) Lafudhi ii) Lahaja iii) Rejesta Taja sifa nne za sajili ya wanasiasa (alama 4)
Previous: Tom: Vipi Tracey? Naona leo unalinga sana. Umenivaria miwani, mbona hivi? Is it because you are very smart today? Tracey: Niko poa! Hata hivyo naona una yako mengine wewe!...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions