Tom: Vipi Tracey? Naona leo unalinga sana. Umenivaria miwani, mbona hivi? Is it because you are very smart today? Tracey: Niko poa! Hata hivyo naona una yako mengine wewe!...

      

Tom: Vipi Tracey? Naona leo unalinga sana.
Umenivaria miwani, mbona hivi? Is it because you are very smart today?
Tracey: Niko poa! Hata hivyo naona una yako mengine wewe! Siringi! Nikobusy tu sana. Plus company yako inatisha, hujui siku hizi nimechill.Tena umenubore.
Tom: Kumbe wewe ni……………………………

(a) Taja sajili inayojitokeza katika dondoo hii. (alama 1)
(b) Taja mifano inayojitokeza katika dondoo ya
(i) Kubadili msimbo (alama 1)
(ii) Kuchanganya msimbo. (alama 1)
(c) Ni kwa nini wazungumzaji hubadili na kuchanganya msimbo. (alama 2)
(d) Ni mzungumzaji yupi ana lafudhi? Ni nini maana ya lafudhi? (alama 3)
(e) Taja sababu mbili za kuwa na lafudhi. (alama 2)

  

Answers


ESTHER
(a) Mazungumzo ya vijana. alama 1
(b) Kubadili msimbo
(i) Is it because you are very smart today? Plus your company
1X1
(ii) Kuchanganya msimbo
- Niko busy
- Nimechill
- Umenibore
1X1

(c) Kwa sababu ya kuwa na ufanisi wa lugha mbili au zaidi.
- Kwa kukosa msamiati mwafaka wa kutumia lugha moja ili kuonyesha kuwa unaifahamu
lugha iliyo na hadhi Fulani katika jamii. Ili kuficha maana kutoka kundi moja la watu.
(d) Mzungumzaji mwenye lafudhi.
Tom 1
Maana ya lafudhi –
- Athari ya lugha ya kwanza.
(e) - Kwa sababu ya athari ya lugha ya mama
- Athari ya lugha zingine zinazozunguka mzungumzaji.
- Kwa sababu ya kasoro Fulani katika ala za matamshi za mzungumzaji.


ESTHER STEVE answered the question on April 30, 2018 at 19:57


Next: (a) Katika jamii huwa wakati mwingine kuna matumizi ya lugha isiyo ya kistaarabu.taja mifano mitano ya lugha ya sampuli hiyo. ( alama 5) (b) Taja mambo matano...
Previous: Na ujenge nyumba yako, jingi jasho likuoshe,Ufyeke, upime na uweke nguzo,Kisha paa uweke na ukandike,Siku nyingi bila kuingiliwa na mgeni hutakaa.Wataanza kutalii mpaka mende usiku,Nje...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions