Na ujenge nyumba yako, jingi jasho likuoshe,Ufyeke, upime na uweke nguzo,Kisha paa uweke na ukandike,Siku nyingi bila kuingiliwa na mgeni hutakaa.Wataanza kutalii mpaka mende usiku,Nje...

      

1. Na ujenge nyumba yako, jingi jasho likuoshe,
Ufyeke, upime na uweke nguzo,
Kisha paa uweke na ukandike,
Siku nyingi bila kuingiliwa na mgeni hutakaa.

Wataanza kutalii mpaka mende usiku,
Nje na ndani ya nyumba watazunguka,
Bila woga, bila ruhusa ulichonacho watakula,
Masalia yatakuwa yako, ijara ya kaziyo.

Na nyingi dawa uweke, nyumba nzima uihame,
Ukae nje nzima siku usubiri,
Wazima wamelala ukirudi usiku,
Vichwa vigumu hawafi mende rahisi.

Kifo cha mende sharti miguu juu
Kichwa ukikanyage kipasuke usikie,
Na kisha wengine usiku mchana uwasake.
Mpaka watakapokwisha. Usiseme nao.

Maswali

(a) (i) Hili ni shairi la aina gani? (alama 1)
(ii) Tetea jibu lako. (alama 3)
(b) Eleza jinsi mshairi alivyoutumia uhuru wake katika utunzi wa shairi hili. (alama 4)
(c) Taja mbinu mbili za lugha alizotumia mshairi na uzitolee mifano. (alama 4)
(d) Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (alama 4)
(e) Eleza ujumbe wa mshairi. (alama 2)
(f) Toa mfano mmoja wa mshata. (alama 1)
(g) Kichwa gani kinaliafiki shairi hili? (alama 1)

  

Answers


ESTHER
(a) (i) Shairi huru (1 x 1 = alama 1)
(ii) - Vina vinabadilikabadilka.
- Idadi ya mizani katika kila mishororo ni tofauti.
- Idadi ya vipande si sawa katika kila msororo.
- Shairi halina kibwagizo. (zozote 3x1 = alama 3)

(b) Uhuru / idhini ya mshairi
• Kuboronga sarufi mf. Nje na ndani ya nyumba watazunguka – watazunguka nje na ndani ya nyumba n.k.
• Inkisari mf. Kaziyo – kazi yako. (2 x 2 = alama 4)

(c) Uhaishaji – Jingi jasho likuoshe.
Tanakuzi – Nje na ndani ya nyumba usiku mchana uwasake.
Taswira – Kifo cha mende … sharti miguu juu.
Ufyeke, upime na uweke nguzo, kisha paa uweke na ukandike. (zozote 2x2 = alama 4)

(d) - Na uweke dawa nyingi hata nyumba.
- Uihame na ukae nje siku nzima ukisubiri.
- Ukirudi usiku, bado utakuta ni wazima.
- Wamelala kwani mende ni vichwa vigumu.
- Hawafi kwa urahisi. (zozote 4x1 = alama 4)

(e) - Ukijenga nyumba yako, hutakaa sana bila kuingiliwa na wageni.
- Hata mende wataanza kutalii bila ruhusa na bila woga wakila ulicho nacho wakuachie masalio.
- Hata ukiweka dawa hawafi.
- Mende wakifa ni sharti miguu iwe juu.
- Haiwezekani mtu kuishi pweke kwenya nyumba. (zozote 2x1 = alama 2)

(f) - Kisha paa uweke na ukaandike
- Siku nyingi bila kuingiliwa na mgeni hutakaa (1 x 1 = alama 1)

(g) - Mende
- Kifo cha mende
- Mende nyumbani (1 x 1 = alama 1)

ESTHER STEVE answered the question on April 30, 2018 at 20:04


Next: Tom: Vipi Tracey? Naona leo unalinga sana. Umenivaria miwani, mbona hivi? Is it because you are very smart today? Tracey: Niko poa! Hata hivyo naona una yako mengine wewe!...
Previous: Upepo unapovuma, kaskazi kwenda kusi , Kwa ngurumu kututuma, ukivisomba vifusi, Ukasukua milima, nakuyang' oa manyasi, IIi kukwepa mikosi, miti mikuu hwinama. Miti mile...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions