Upepo unapovuma, kaskazi kwenda kusi , Kwa ngurumu kututuma, ukivisomba vifusi, Ukasukua milima, nakuyang' oa manyasi, IIi kukwepa mikosi, miti mikuu hwinama. Miti mile...

      

Upepo unapovuma, kaskazi kwenda kusi ,
Kwa ngurumu kututuma, ukivisomba vifusi,
Ukasukua milima, nakuyang' oa manyasi,
IIi kukwepa mikosi, miti mikuu hwinama.

Miti mile iloimia , ikaijaza nafasi,
Kwa matawi yake mema, kusheheneza utosi,
Haiwi iko salama, upepo ukenda kasi,
IIi kukwepa mikosi , miti mikuu hwinama.

Upepo ukiivuma , miti haitaanasi,
Huchezeshwa lelemama, ikachezeshwa na dansi,
Matawi yake hunema , yakakatika rahisi,
IIi kukwepa mikosi, miti mikuu hwinama.

Upepo ukitetema, hukata kama makasi,
Miti hwingia ulema, uzima ukawa basi,
Hilivunja tawi zima, kama eawi halinesi,
IIi kukwepa mikosi, miti mikuu hwinama.

Upepo una zahama , hasa ule wa chunusi,
Hata misitu hwandama, ikabaki mufilisi,
Matawi mani huhama, ikapoteza nemsi,
IIi kukwepa mikosi, miti mikuu hwinama.

Upepo unasukuma, miti hula sarakasi,
Matawi yakachutama, mengi chini hujilisi,
Watu ukiwatazama, wanavuja makamasi,
IIi kukwepa mikosi, miti mikuu hwinama.

Ndege wachimachima, viota wameviasi,
Wakajiweka wanyama, kwenye vichaka yabisi,
Majahazi yaparama, yakenda mwemdo wa ngisi,
IIi kukwepa mikosi, miti mikuu hwinama .

.
Miti mile yenye kima , yenye tambo mahsusi,
Mtawi kakikingama, ili upepo kuuasi,
Billahi yaja nakama, kubwa tena kwa wepesi,
IIi kuwepa mikosi, miti mikuu hwinama.

Miti mile hungama, na kujidhili nafusi,
Upepo ukishavuma, ndipo inatanafusi,
Vinginevyo ni kiyama, hapana wa kuramisi,
Ili Kukwepa mikosi, miti mikuu hwinama.

Maswali

(h) Andika kichwa mwafaka cha shairi hili. (alama 2)
(i) Eleza ujumbe uliomo katika shairi hili. (alama 3)
(j) Taja na utoe mifano ya tamathali za usemi zilizotumiwa katika shairi. (alama 4)
(k) Eleza muundo wa shairi hili. (alama 4)
(l) Andika ubeti wa sita kwa lugha nathari. (alama 4)
(m) Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama ilivyotumiwa katika shairi.(alama 3)
(i) Kututuma
(ii) Haitaanasi
(iii) Zahama

  

Answers


ESTHER
(a) Upepo (1 x 2 = alama 2)
(b) Viongozi huhitajika wawe wanyenyekevu na kuadilika ili kujiepusha na matatizo mengi ya watetesi au maadui.

(c) (i) Jazanda – ili kukwepa mikosi miti mikuu hwinama.
(ii) Tashishi – Miti hula sarakasi.
(iii) Taswira – kusukua milima majahazi yakaparama.
(iv) Tashbihi – hukata kama makasi. (zozote 2x2 = alama 4)

(d) (i) Beti tisa.
(ii) Mishororo minne katika ubeti – Tarbia.
(iii) Vipande viwili – mathnawi.
(iv) Kibwagizo – ili kukuwepa mikosi, miti mikuu hwinama.
(v) Vina – vina vya ukwapi ni ma katika mishororo mitatu ya kwanza kwa kila ubeti na si katika kibwagizo.
- Vina vya utao ni si katika mishororo mitatu ya kwanza kwa kila ubeti na ma katika kibwagizo kibwagizo.
(vi) Mizani – Kumi na sita kwa kila mshororo. (zozote 4 x 1 = alama 4)

(e) - Upepo unapovuma miti huyumbayumba kiajabu na matawi mengi huanguka.
- Watu wanalia kwa huzuni. Ili kukwepa matatizo, viongozi lazima wawe
wanyenyekevu.

(f) (i) Kututuma – Kupiga.
(ii) Haitaanasi – Haifurahii.
(iii) Zahama – Fujo, Ghasia.


ESTHER STEVE answered the question on April 30, 2018 at 20:05


Next: Na ujenge nyumba yako, jingi jasho likuoshe,Ufyeke, upime na uweke nguzo,Kisha paa uweke na ukandike,Siku nyingi bila kuingiliwa na mgeni hutakaa.Wataanza kutalii mpaka mende usiku,Nje...
Previous: Jadili aina tatu za ‘maana’ huku ukizitolea mifano kutoka Kiswahili.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions