Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Jadili aina tatu za ‘maana’ huku ukizitolea mifano kutoka Kiswahili.

      

Jadili aina tatu za ‘maana’ huku ukizitolea mifano kutoka Kiswahili.

  

Answers


ESTHER
1. Maana tambuzi. Hii ni ile maana inayofahamika na watu wanaotumia lugha fulani. Ni maana inayoelezewa na kamusi ya lugha fulani kama vile kamusi ya Kiswahili. Maana tambuzi ina sifa za kimmataifa. Kwa mfano, ukitaja kiti, mswahili yeyote yule ataelewa na kufahamu unachokizungumzia.
Kwa mfano, jina mwanamke lina maana ya +binadamu
+ kike
2. Maana kimatilaba. Hii ni maana inayotokana na jamii fulani. Kulingana na mtazamo wa jamii fulani, neno fulani huzua hisia tofauti katika jamii. Kwa mfano neno mbwa litazua hisia chanya kwa wazungu na hisia hasi kwa Waafrika.
3. Maana kimtindo. Hii ni maana inayotokana na mtindo wa kiwango cha mtu binafsi. Watu wa tabaka la juu watafasiri maana tofauti na watu la tabaka la chini. Kuna pia mtindo wa kikundi cha watu kama vile lahaja fulani. Maneno huenda yakawa na maana tofauti kulingana na mtindo wa kundi fulani la watu.

ESTHER STEVE answered the question on April 30, 2018 at 20:19


Next: Upepo unapovuma, kaskazi kwenda kusi , Kwa ngurumu kututuma, ukivisomba vifusi, Ukasukua milima, nakuyang' oa manyasi, IIi kukwepa mikosi, miti mikuu hwinama. Miti mile...
Previous: Eleza nafasi ya makundi yafuatayo katika ama kukua au kudhoofika kwa Kiswahili nchini Kenya kabla ya uhuru. (a) Watawala (b) Wamisheni (c) Walowezi

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions