Jadili juhudi za TUKI katika kuendeleza na kustawisha Kiswahili katika ukanda wa Afrika Mashariki.

      

Jadili juhudi za TUKI katika kuendeleza na kustawisha Kiswahili katika ukanda wa Afrika Mashariki.

  

Answers


ESTHER
TUKI- Taasisi ya uchunguzi wa Kiswahili iko katika chuo kikuu cha dar-es-salaam na ndiyo taasisi pekee ambayo shughuli yake kuu ni utafiti na usambazaji wa Kiswahili. Juhudi zake ni kama ifuatavyo:
1. Kuendeleza utungaji wa kamusi zinazohusiana na Kiswahili sanifu. Kamusi hizi ni kama vile: kamusi ya Kiswahili sanifu, Kamusi ya Isimu jamii, kamusi ya Kiswahili-Kingereza, kamusi ya sayansi na teknolojia na kadhalika
TUKI pia hupitia na hurekebisha kamusi za Kiswahili panapotokea haja. Kamusi hizi zimesaidia pakubwa katika kuendeleza na kueneza Kiswahili.
2. Kutafiti na kuchapisha matokeo ya utafiti katika nyaja mbalimbali za lugha, isimu na fasihi ya Kiswahili. Utafiti huu umesaidia katika kukuza na kueneza Kiswahili.

3. Kulinda usanifu wa Lugha ya Kiswahili. TUKI imejitwika mzigo wa kulinda usanifu wa lugha ya Kiswahili. Inashughulika na usanifishaji wa misamiati mipya inayoundwa au kubuniwa kutumika katika Kiswahili.
4. TUKI husimamia tafsiri na ukalimani. Taasisi hii hutoa ushauri kwa serikali, mashirika ya kitaifa nay a kibinafsi kuhusu mambo ya tafsiri hasa ya hati za kiserikali, katiba n.k. Hili husaidia katika kuendeleza Kiswahili sanifu.
5. Kufundisha Kiswahili kama lugha ya pili hasa kwa wageni kutoka nje ya ulimwengu wa waswahili. TUKI hushiriki katika kufundisha katika idara ya Kiswahili, fasihi, lugha za kigeni na isimu nah ii ni njia mwafaka ya kuendeleza Kiswahili
Hoja 5*3 = 15

ESTHER STEVE answered the question on April 30, 2018 at 20:22


Next: Eleza nafasi ya makundi yafuatayo katika ama kukua au kudhoofika kwa Kiswahili nchini Kenya kabla ya uhuru. (a) Watawala (b) Wamisheni (c) Walowezi
Previous: Jadili kwa kina sifa zozote tano zinazokitambulisha Kiswahili kama lugha ya kibantu

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions