Jadili kwa kina sifa zozote tano zinazokitambulisha Kiswahili kama lugha ya kibantu

      

Jadili kwa kina sifa zozote tano zinazokitambulisha Kiswahili kama lugha ya kibantu.

  

Answers


ESTHER
Wanaisimu maarufu kama vile Carl Meinhof na Malcom Guthrie wamedhihirisha kuwwa lguha ya Kiswahili ina sifa zinazofanana na zile za lugha nyingine za kibantu. Sifa hizi zimebainishwa kupitia vigezo fulani vya kiisimu. Vipengele hivi ni kama ifuatavyo:
a. Msamiati. Uchunguzi wa msamiati wa msingi wa lugha ya Kiswahili na ule wa lugha nyingine za kibantu umeonyesha kuwa kuna mfanano. Msamiati wa kimsingi na ule wa kawaida unalingana sana. Mfanao unadhihirika sana hasa katika msamiati ufuatao:
i. Msamiati wa viungo vya mwili. Kwa mfano
Kiswahili Kikuyu Lubukusu
ulimi lulimi

ii. Msamiati wa maumbile kama vile jua, maji, milima na kadhalika. Kwa mfano Jua katika Kiswahili na Sua katika lugha ya Kikamba.
iii. Msamiati wa hesabu hasa moja hadi tano.
b. Maumbo ya maneno.
Lugha ya Kiswahili ina maumbo ya maneno yanayofanana na lugha nyingine za kibantu. Maneno katika lugha hizi hujengwa na viambishi. Kwa mfano
m-tu - Kiswahili
Mu-ndu- Kikuyu
Lu-limi – Lubukusu

c. Mfumo wa sauti
Sauti za irabu na zile za konsonanti za lugha ya Kiswahili na lugha nyingine za kibantu hufanana kwa kiasi kikubwa katika mpangilio wake na muundo wake wa silabi. Mwanzo hakuna silabi funge katika lugha hizi isipokuwa katika maneno ya kukopwa. Silabi huundwa kwa konsonanti na irabu au silabi mwambatano zenye konsonanti zaidi ya moja. Mfano:
M-to-to
Ku-nywa
Mu-ndu
Lu-li-mi
d. Mfumo wa ngeli.
Sifa za lugha ya Kiswahili zinazojitokeza katika lugha nyingine za kibantu ni ile ya mpanngilio wa nomino kaatik makundi yanayoiywa ngeli. Vilevile kuna uwiano wa kimsamiati au upatanisho wa kisarufi kama vile: Mtoto Mzuri Ameanguka
Kiti kizuri kimeanguka
e. Mpangilio wa maneno
Mpangilio wa maneno katika sentensi, vishazi au virai katika lugha ya Kiswahili unafuata utaratibu fulani ambapo nomino ndio neno linalotawala na kuleta upatanisho wa kisarufi katika sentensi. Utaratibu huu hutumika katika lugha zote za Kibantu.

ESTHER STEVE answered the question on April 30, 2018 at 20:23


Next: Jadili juhudi za TUKI katika kuendeleza na kustawisha Kiswahili katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Previous:  Jadili maudhui ya siasa katika Tamthilia ya kigogo

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions