Jadili maudhui ya siasa katika Tamthilia ya kigogo

      

Jadili maudhui ya siasa katika Tamthilia ya kigogo

  

Answers


ESTHER
Siasa ni itikadi inayofuatwa na kundi fulani au jamii fulani ambayo ni msingi wa kuendesha uchumi, utamaduni na mwenendo mzima wa maisha ya jamii.
Siasa ni mfumo unaohusisha zaidi ya uongozi wa watu kwa kufuata kanuni, sheria sera, uwajibikaji, uwazi na ugawaji wa rasilimali sawa kwa wanachi wake katika kuwaletea maendeleo.
Wananchi huchagua kikundi cha watu ambao wanaamini na kuwapa uwezo wa kuunda serikali ili waongoze kwa niaba yao.
Mwandishi ameeleza siasa kama mchezo mchafu. Inageuka mchezo mchafu pale serikali inaanza kwenda kinyume na utaratibu na kanuni sahihi na kutofuata maadili ya uongozi. Viongozi wanageuka waongo, wakatili, wanafiki, wenye uchu wa mali, wanyonyaji na wauaji. Wanafanya lolote ili kujitajirisha. Wanaongoza nchi kwa manufaa yao binafsi na sio kuwaletea wananchi maendeleo. Wanawajengea hofu na kuwasababishia maisha magumu.
Majoka anajua vilivyo kuucheza huu mchezo. Atafanya lolote lile kujitajirisha na anaonekana kutotosheka. Ana washauri wabaya kama vile Kenga. Kenga anamfundisha ile siasa ya kuuma na kuvuvia.
Sudi amekuwa akipinga uongozi mbaya wa Majoka. vile vile Majoka alitaka kuchongewa kinyago na Sudi lakini Sudi anakataa. Ili kulipiza kisasi, Majoka analifunga soko na kumtia ndani Ashua ; mkewe Sudi. Anashauriwa kufanya hivi na Kenga ili pia aweze kumshawishi Sudi kumchongea kinyago ili mkewe aachiliwe.
Majoka anaapa kuifunga runinga ya mzalendo kwa kupeperusha habari za maandamano moja kwa moja. Anaipenda runinga ya mashujaa inayotangaza habari nzuri kumhusu pekee.
Majoka anawaua wapinzani wake au kuwatumia wahuni. Akitumia Kenga, alimuua Jabali ; mpinzani wake wa kipindi kilichotangulia wa chama cha mwenge. Anatumia Ngurumo kumvamia Tunu. Alikuwa amesema auawe lakini bahati nzuri akanusurika. Majoka anapotambua kuwa njama yake imejulikana, anamuua Ngurumo. Hata bibiye ; Asiya alikuwa pia auawe akanusurika.
Maziara ya Jimbo yamejaa na Ngurumo hana nafasi ya kuzikwa. Majoka anajua kuwa hili litamharibia sifa iwapo litaangaziwa na vyombo vya habari. Anaicheza karata yake vizuri. Anapanga chatu auwawe. Anajua kuwa wakereketwa wa mazingira wataandamana kutetea haki za wanyama na kwa hivyo vyombo vya habari vitawaangazia wao wala si mazishi ya Ngurumo atakayezikwa juu ya mfu mwingine.
Kenga alitarajia watu wengi wangehudhuria sherehe za uhuru. Haiwi hivyo. Anajuta heri wangelikodisha mabasi yawalete vijana na akina mama wajaze uwanja. Hii ni mbinu watumiayo wanasiasa kuonyesha walivyo na umaarufu kumbe sivyo.
Mwandishi wa tamthilia hii hata hivyo ametaka kuonyesha kuwa wananchi wanachangia pakubwa katika kuamua watatawaliwa vipi na viongozi. Iwapo watazinduka, waache usaliti, wasiongozwe na tamaa na waache ubaraka, kwa kutumia uwezo wao wa kura, wanaweza kuwachagua viongozi wazuri. Tunu anawahimiza wananchi kutowachagua tena viongozi wanaokiuka haki zao na wasiowajibika.

ESTHER STEVE answered the question on April 30, 2018 at 20:27


Next: Jadili kwa kina sifa zozote tano zinazokitambulisha Kiswahili kama lugha ya kibantu
Previous: Onyesha jinsi mbinu ya Taharuki imetumiwa katika Tamthilia ya kigogo

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions