Onyesha jinsi mbinu ya Taharuki imetumiwa katika Tamthilia ya kigogo

      

Onyesha jinsi mbinu ya Taharuki imetumiwa katika Tamthilia ya kigogo

  

Answers


ESTHER
Taharuki ni hali ya kusubiri, kusisimka na kuwa na hamu kutaka kujua kitakachotokea baadaye na jinsi ya kutokea kwake katika kazi za fasihi. Baadhi ya mifano katika tamthilia ni kama:
? Boza anaangaliaangalia simu yake mara nyingi kama anayengojea jambo fulani uk. 1. Pia anaonekana kuchonga kinyago fulani na Kombe haelewi kuna nini. Linatuacha katika taharuki. Ni nini hicho anachokijua Boza ambacho Kombe hajui? Uk 3
? Sudi anachonga kinyago cha mwanamke. Je anamchonga nani? Uk. 10
? Mzee Kenga anapanga njama fulani, hatujui anapanga nini Uk. 15
? Kuna maandamano anakofanyia kazi Siti. Akina Tunu wanapoondoka kwenda huko, hatujui kunatokea nini. uk 18
? Ashua anapoenda ofisini mwa Majoka, Majoka anajaribu kumrai awe na uhusiano wa kimapenzi naye. Ashua anapokataa, Majoka anapigia Husda simu aje ofisni. Itakuwaje?
? Watoto wa Ashua wanapelekwa kwa akina Tunu, walipata chakula?
? Ndoto ya Tunu inatuwacha katika taharuki, mamake anasema sio ndoto ni tukio la kitotoni ila haelezi kisa hicho. Uk. 53
? Tunu anasema anataka kwenda kukutana na majangili waliomvamia. Anasema aliskikia sauti aijuayo. Hili linatuwacha katika taharuki. Nani huyo? Itakuwaje akienda? Uk. 55
? Hatujui iwapo akina Siti watahama Sagamoyo baada ya kupewa vijibarua Uk. 52
? Majoka anapozirai baada ya kupashwa habari za kufariki kwa Ngao Junior na kupelekwa hospitalini tunapata taharuki. Je, atapona? Atahudhuria mkutano?
? Ngurumo na Ngao Junior walizikwa? Lini? Wapi? Watu waliandamana kama alivyokisia Majoka?
? Husda hajui kwa nini Majoka akazirai. Nani atamwambia?
? Husda anapojulishwa kuwa Ngao Junior alifariki anazirai. Nini kiliendelea baadaye?
? Majoka alienda wapi baada ya kuachwa na wafuasi wake? Je alifunguliwa mashtaka?

ESTHER STEVE answered the question on April 30, 2018 at 20:34


Next:  Jadili maudhui ya siasa katika Tamthilia ya kigogo
Previous: Ujenzi wa jamii mpya ni wajibu wa vijana. Thibitisha ukweli wa kauli hii ukirejelea riwaya ya Kidagaa Kimemwozea.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions