“Hatimaye Tarishi alikuja na barua moja ya Mtemi na nakala ya siku hiyo ya gazeti la Tomoko Leo: Mtemi Nasaba Bora akapokea barua hiyo na...

      

“Hatimaye Tarishi alikuja na barua moja ya Mtemi na nakala ya siku hiyo ya gazeti la Tomoko Leo: Mtemi Nasaba Bora akapokea barua hiyo na gazeti toka kwa tarishi aliyekuwa kanywea si haba.”
(a) Jadili mambo yaliyomshtua Mtemi Nasaba Bora kuhusiana na barua na gazeti alizopokea siku hiyo.
(b) Onyesha jinsi madhubuti alivyoendeleza uasi dhidi ya babake.

  

Answers


ESTHER
(a) Jadili mambo yaliyomshitua Mtemi Nasaba Bora kuhusiana na barua na gazeti alizozipokea siku hiyo.
? Hakuona picha yake katika gazeti la Tomoko Leo kama ilivyokuwa wakati nduguye Mwalimu Majisifu alikuwa mhariri wa gazeti hilo licha ya kutoelewana kwao.
? Katika barua aliyopokea mtoto wake madhubuti aliyekuwa masomoni. Urusi alimwarifu juu ya kurejea kwake nyumbani na angetaka mpango wa kumtafutia ajira jeshini au popote uisitishwe, kwa sababu hataki ajira inayotokana na mlungula.
? Madhubuti pia alisema kuwa alitaka kusimama kwa miguu yake mwenyewe apate au akose kwa kustahiki au kushtahili kwa sababu ya jadi yake.
? Madhubuti alimwambia babake alikuwa amechoka na ingawa alimpenda kulikuwa na vitendo vyake ambavyo hakuwa akivipenda.
? Mtemi Nasaba Bora alipomaliza kusoma barua alikasirika na kugonga meza kwa kuona kuwa madhubuti hajui dunia inavyozanguka.
? Pia alikasirika kwa kuona Madhubuti alivyokuwa amejitambulisha na mamake(Madhubuti Zuhura) badala ya kujitambulisha naye kama baba yake.
(b) Onyesha jinsi Madhubuti alivyoendeleza uasi dhidi ya babake.
? Katika barua aliyomwandikia babake alipokaribia kurudi nyumbani alitaka mipango ya kutafutiwa kazi jeshini au popote isitishwe kwa sababu hukutaka kazi iliyotokana na mlungula.
? Madhubuti alimwambia babake kuwa ingawa alimpenda kulikuwa na vitendo vyake ambavyo hakupenda.
? Madhubuti alimaliza barua yake kwa kujiita Madhubuti Zuhura badala ya kujitambulisha na babake.
? Alipendana na kushirikana na mfanyikazi wao Amani kwa sababu mitazamo yao ilishabihiana. Hatimaye alihamia kibandani alimokaa Amani.
? Madhubuti alichukia vitendo vya babake vya kupoka, kupiga pute, kulimbikiza mali haramu na kuhalalisha haramu kwa sababu vilifanya bara la Afrika kuchekwa katika kila pembe ya dunia.
? Alimwomba Amani ashirikiane naye katika kuwazidua watu kwa lengo la kukomesha udhalimu kuanzia pale kwao wanapofanyiwa udhalimu na baba yake.
? Madhubuti alifuata kwa kukubali babake ampeleke masomoni ng’ambo kwa pesa alizowaitisha watu kwa nguvu ingawa alikuwa amefaulu kuingia katika Chuo Kikuu pale nyumbani kwao.
? Anahiari kujiua kinasaba ili azaliwe upya na asiwe na uhusiano wowote na Nasaba ya Mtemi Nasaba Bora.
? Madhubuti alikubaliana na Amani waongoze mapinduzi kwa tahadhari wasije wakatoa viongozi dhalimu na kuingiza mwingine dhalimu zaidi.
? Madhubuti alipopata ajira mjini Songoa alianza kuchunguza jinsi babake alivyopata kumiliki mashamba mengi makubwa.
ESTHER STEVE answered the question on April 30, 2018 at 20:49


Next: Explain the problems faced by Africans farmers during colonial period
Previous: Explain the advantages of induction motors over synchronous motors

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions