Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

“We bwana unafikiri natumia petroli nini?” (a) Uweke usemi huu katika muktadha wake. (al 4) (b) Huku ukitoa mifano, eleza mbinu mbili za lugha zilizotumiwa na mwandishi...

      

“We bwana unafikiri natumia petroli nini?”
(a) Uweke usemi huu katika muktadha wake. (al 4)
(b) Huku ukitoa mifano, eleza mbinu mbili za lugha zilizotumiwa na mwandishi katika dondoo hili. (al 4)
(c) Eleza migogoro yoyote sita inayojitokeza katika riwaya ya Kidagaa Kimemwozea. (al 12)

  

Answers


ESTHER
Msemaji – Dora
Msemewa – mwalimu majisafu Mahali – nyumbani kwao Sababu – Kutelekeswa kwa kazi zote za kuwalinda wanao walemuvu bila usaidizi wa mumewe majisifu. (1 x 4) (b) Utohozi – Petroli Swali balagha : “wewe unafikiri ninatumia petrol nini? (2 x2) (c) Migogoro
(i) Migogoro ya kindugu
Bwana mtemi na familia yake wanakinzana. Madhubuti amekuwa mwasi kwa babake. Mtemi na mkewe wanasomeana kila mara. Mtemi pia anashiriki mapenzi nje ya ndoa. Bwana majisifu na mkewe dora vile vile wana migogoro kuhusu ulezi wa wanao vilema.
(ii) Migogoro kati ya watawal na watawaliwa
Mtemi na nduguye hawapikiki chungu kimoja. Wao wanazomeana kila mara. Hali inayowafanya wasiwasiliane ufanisi au matatizo yao.
(iii)Migogoro kati ya watawala na wataliwa
Mzee matuko weye anatiwa nguvuni kwasababu ya kumwambia mtemi wazi wazi kuwa utawala wake ni mbaya na anafua kuondoka uongozini. Mtemi anawadhuklumu wanasokomoko kwa kunyakua shamba zao kama ule la chichiri Hamadi.
(iv)Migogoro ya waajiri na waajiriwa
Mtemi Nasaba bora anawaajhiri na kufata kazi wafanya kazi wakati wowote. Akiona wanafanya kazi vyema anawapiga kalamu. Wafanyakazi wengi sokomoko wanafanya kazi za sulubu zilizo na mishahara ya kijungu jiko.
(v) Migogoro ya mashamba
Wanasokomoko na Tomoko kwa ujumla wanamlaumu mtemi kwa kuwapokonya mashamba yao. Amani hana furaha kwa sababu ya shamba lao kuchukuliwa na Bwana Mtemi.
(vi)Migogoro ya kimapenzi
Majununi na mitchelle wamekuwa na huba. Hata hivyo Mitchelle anamkataa majununi kwa kusingizia nyumba. Mashaka anaamua kutotoka shuleni kwa sababu ya mapenzi yake kuvunjika. Mengine
(vii) Migogoro ya kinasaba
(viii) Migogoro ya kijinsia
(ix) Migogoro ya askari na wanachi
(x) migogoro ya setka katika uandishi
(xi)migogoro ya elimu
ESTHER STEVE answered the question on May 14, 2018 at 19:56


Next: Kidagaa Kimemwozea “....usiniweke pembeni kama tanbihi, mimi na wanawake wenzangu kama wanaume wengine wafanyavyo waandikapo...” a) Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama 4)
Previous: Maenezi ya Kiswahili Afrika Mashariki punde baada ya uhuru yalikuwa na chagamoto tele. Fafanua zozote tano.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions