Onyesha jinsi majazi yametumika katika tamthilia ya Kigogo.

      

Onyesha jinsi majazi yametumika katika tamthilia ya Kigogo.

  

Answers


ESTHER
Majazi ni mbinu ya kumpa mtu au mahali jina kulingana na hulka au sifa zake. Mwandishi ametumia majazi kama ifuatavyo.
Mhusika Jina na Sifa
Majoka Ni wingi wa joka: Nyoka mkubwa ajabu.
Majoka ana kampuni ya kutengeneza sumu ya nyoka. Ofisini mwake pia anafuga swila. Ngurumo aliuawa na chatu wa Majoka.
Nyoka huwa na sumu na Majoka ni sumu kwa maendeleo ya Sagamoyo. Anawaua wapinzani na vibaraka wake kama vile Jabali na Ngurumo.
Majoka pia ni msiri ajabu! Mambo yake huyatenda kichinichini kama anyemeleavyo nyoka.
Tunu
Kitu anachopewa mtu na mwingine kama zawadi. Kitu ambacho ni adimu kupatikana na chenye kutumika kwa nadra.
Tunu ni zawadi kwa wanasagamoyo. Amekuja kuwakomboa kutoka uongozi wa kidhalimu wa Majoka. Tunu ni mwanamke jasiri, aliyesoma na mwenye busara. Ni miongoni mwa wanawake nadra sana Sagamoyo
Sudi Sudi ni bahati njema. Kama Tunu, kuwa na Sudi Sagamoyo ni bahati njema. Anaipigania hadi kupata ukombozi.
Kenga Kenga ni kufanya mtu aamini jambo lisilo la kweli; danganya au laghai
Kenga ni mshauri wa karibu wa Majoka. Tunaona akiwa mshauri wa uongo. Kwa mfano, anamshauri kumtia ndani Ashua kutamfanya Sudi amchongee kinyago. Badala ya kumshauri Majoka kusikiliza vilio vya wanasagamoyo, anamshauri kuwamaliza vijana wanaotetea haki pamoja na wafadhili wao. Anamdanganya Majoka kuwa Tunu hawezi kupigiwa kura ilhali watu wengi wako nyuma ya Tunu.

Husda Linatokana na neno Husuda .
Husuda ni mtazamo wa ubaya juu ya mtu na mali yake; tabia ya mtu kutopendezwa au kutofurahia mafanikio ya mwingine; jicho baya.
Husda amejaa husuda. Anamuonea wivu Ashua na kumsingizia kuwa na uhusiano na bwanake mzee Majoka. Majoka pia hampendi Husda kwa kuwa alijua Husda anaongozwa na tama ya mali yake wala si mapenzi ya dhati.
Boza Ina maana ya mtu mpubavu.
Boza ni pumbavu, anamfuata Majoka kijinga hata haoni anapodhulumiwa. Kwa mfano, haoni kuwa serikali ina ufisadi kwa kuwatoza kodi ya juu na hata soko halisafishwi. Anafurahia kipande kidogo cha keki anachopewa na Kenga ilhali mkewe ndiye aliyeoka.
Kombe Kombe ni mmea unaotambaa ambao utomvu wake ni sumu inayopakwa katika kigumba cha mshale. Kombe ni sumu katika harakati za ukombozi. Ni kigeugeu anayejifanya kibaraka mbele ya viongozi na kuwasema wasipokuwepo. Watu wa aina hii hulemaza shughuli za ukombozi.
Ngurumo Ina maana ya Sauti ya mvumo inayosikika angani, hasa wakati wa mvua kubwa au mlio wa mnyama kama simba.
Ngurumo ni mkali. Yeye ndiye alimvamia Tunu na kumuumiza. Sauti yake husikilizwa na walevi anapofanyia Majoka kampeni.
Mamapima Hili linatokana na hali ya kuwapimia watu vileo kule Mangweni
Hashima Kutokana na neno heshima. Hashima ni mwanamke mwenye heshima na mtulivu. Alimlea mwanawe kwa maadili hata baada ya mumewe kuaga
Chapakazi Ni hali ya kufanya kazi. Soko la chapakazi ndiko watu wanapofanyia kazi ili kujipatia riziki
Sagamoyo Saga ni kupondaponda kitu.
Moyo ni kiungo muhimu cha kusukuma damu mwilini. Kikiwa na hitilafu, mtu hufariki.
Sagamoyo linaashiria Utawala dhalimu wa Majoka unawaumiza nyoyo wananchi kama vile: kutozwa kodi ya juu, kunyimwa haki ya kuandamana, watu kuuawa kiholela na wengine kufungwa bila makosa n.k

ESTHER STEVE answered the question on May 14, 2018 at 20:43


Next: Kiswahili ni lugha ya kibantu kulingana na ushahidi wa ki-isimu. Thibitisha kauli hii.
Previous: Discuss five trends in forms of business units.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions