Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Tumbo lisiloshiba “Mimi sitaki ‘naam’ zako nyingi .Wala sitaki msaada wako dhaifu….” a) Eleza muktadha wa dondoo hilo. (al.4) b) Taja na ueleze sifa tatu za...

      

Tumbo lisiloshiba
“Mimi sitaki ‘naam’ zako nyingi .Wala sitaki msaada wako dhaifu….”
a) Eleza muktadha wa dondoo hilo. (al.4)
b) Taja na ueleze sifa tatu za msemaji na tatu za msemewa. (al.6)
c) Linganisha matukio hadithini na hali halisi katika jamii ya kiafrika. (al.10)

  

Answers


ESTHER
a) Msemaji ni jitu, Msemewa ni Mzee Mago. Walikuwa mkahawani kwa Mzee Mago. Ni wakati Mzee Mago alisema atalisaidia Jitu, nalo Jitu likasema halikuhitaji usaidizi wowote kutoka kwa Mzee Mago na kusema kuwa lilikuwa na uwezo wa kumsaidia Mzee Mago kwa kukila chakula chote

b) Sifa tatu za msemaji na tatu za msemewa

Jitu (3*1)
1. Mlafi - Alikula vyakula vyote vya wateja waliokuwepo katika mkahawa wa Mzee Mago
2. Ni tajiri - Mavazi yake ya suti na tai yalidhihirisha kuwa ni tajiri. Aidha yeye aliendeshwa na dereva wake maalumu.
3. Mkubwa wa kimo - Alikuwa pandikizi la mtu . Alipoingia katika mkahawa mshenzi wateja wote walishtuka


Mzee Mago (3*1)

1. Mwenye bidi - Mzee Mago alijinyima , akatafuta wenzake wazungumze na kulijadili jambo ambalo lilikuwa nyeti sana kwao
2. Mpenda haki na mtetezi - Yeye hakupuuza ule uvumi bali alijaribu kuutafutia suluhisho
3. Ni mshawi - Aliwashawishi wanyonge wenzake watafute wanasheria waaminifu ili wasaidie kufafanua vipengele vigumu vya sheria kama njia ya kuwavukisha vikwazo ili wapate suluhisho
4. Ni mzindushi
C) Matukio hadithini na hali halisi Afrika

Unyakuzi wa ardhi
Dhuluma ya viongozi
Unyanyasaji
Ubinafsi
Matumizi ya polisi/sheria /kunyanyasa raia
Matatizo ya wanyonge
( zozote 5*2)

ESTHER STEVE answered the question on May 27, 2018 at 18:06


Next: Give reasons why Jesus accepted to be baptized by John the Baptist
Previous: Describe the economic organization of the Buganda kingdom

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions