Eleza mbinu zozote kumi za uandishi katika tamthilia ya kigogo

      

Eleza mbinu zozote kumi za uandishi katika tamthilia ya kigogo.

  

Answers


Raphael
1.USHAIRI.
Tunamwona babu anampa Majoka ushairi ndotoni ambapo anamshauri kusikia vilio vya wanasagamoyo. Anamwambia kuwa maisha ni njia mbili, wema na maovu na mwishowe maovu yana mwisho wake.
2.SADFA.
Pale ofisini mwa Majoka ambapo Ashua anaingia bila Majoka kumtarajia.
3.KISENGERE NYUMA.
Pale ambapo Ashua anakumbuka maneno matamu na mambo mengi aliyomwahidi mwanzoni mwa mapenzi yao.
4.METHALI.
Majoka anaposema kuwa heri kufuga mbuzi, binadamu wana maudhi ambapo ilikuwa ni baada ya Ashua kukataa ombi lake.
5.MASWALI YA BALAGHA.
Iyo rununu haitulii mfukoni, yakuuma?
6.KINAYA.
Pale ambapo Tunu anasema kuwa kwa mwezi huu mzima wa uhuru wale mali waliochuna kwa miaka sitini. Ni kinaya kwa sababu hakuna walichovuna bali viongozi wao ndio wanao jinufaisha na mali ya wanasagamoyo.
7.JAZANDA.
Pale ambapo husda anamwambia Ashua kuwa ameshindwa kufuga kuku na kanga hatamweza. Kuku akiwa ni mmewe Sudi na kanga akiwa ni Majoka ambapo Ashua alishindwa kumlinda Sudi Majoka hamwezi.
8.NDOTO.
Tunamwona Tunu anaota kuwa anafukuzwa na mzee Marara akiutaka mkufu wa dhahabu. Hii ina ishara ya kumkanya Tunu asiwe kiongozi wa Sagamoyo ambapo mkufu unaashiria uongozi.
9.KIANGAZAMBELE.
Majoka anapoanza kuogopa kuwa waandamanaji watafika kwenye ofisi yake na wammalize na mwishowe tunaona wanamtoa uongozini.
10.TAHARUKI.
Wageni walitarajiwa kule Sagamoyo kwenye sherehe za uhuru ambapo hatujaambiwa kama walikuja.


Earlen answered the question on June 24, 2018 at 14:30


Next: Explain six challenges that faced nationalists in Ghana
Previous: Describe how an image is formed on a CRO screen

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions