Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Eleza mambo yanayochangia katika kuenea kwa lugha ya kiswahili

      

Ekeza mambo yanayochangia katika kuenea kwa lugha ya kiswahili

  

Answers


Arnold
1. Lugha ya Kiswahili kufundishwa katika taasisi za elimu.

Kiswahili kinafundishwa katika shule za msingi na upili kama somo la lazima. Kiswahili kinafundishwa pia katika vyuo vikuu na hivyo basi kinaenea kupitia kwa elimu.

2. Kubuniwa kwa taasisi za uchunguzi za Kiswahili.

Taasisi za kufanya utafiti katika lugha ya Kiswahili zimebuniwa kwa mfano TUKI. Taasisi hizi zinawezesha katika usanifishaji na uboreshaji wa misamiati na maneno ya Kiswahili.

3. Kiswahili kinatumika katika uchapishaji wa magazeti na majarida.

Lugha ya Kiswahili kinatumiwa kuchapisha magazeti kama vile taifa leo na kwa njia hii kiswahili kinazidi kuenziwa na kuenezwa.

4. Kiswahili kimefanywa kuwa lugha ya taifa.

Nchini Kenya Kiswahili kimefanywa kuwa lugha ya taifa na hivyo basi kinazungumzwa na rais wa humu nchini kwa sababu lugha ya taifa ni kitambulisho cha taifa.

5. Kiswahili kutumika katika vyombo vya habari.

Lugha ya kiswahili kinatumiwa katika vyombo vya habari kama vile redio na runinga kutoa taarifa kwa raia.

6. Kiswahili kutumika katika utunzi wa nyimbo na sanaa nyinginezo.

Wasanii wanakitumia Kiswahili kutunga nyimbo na mashairi pamoja na tungo nyingine hivyo kudumisha uenezi wa lugha ya kiswahili. Tungo hizi zinaposomwa na kusikilizwa kinaboresha lugha ya kiswahili miongoni mwa jamii.

Arnold Diru answered the question on June 23, 2018 at 03:48


Next: Knowledge based systems (KBSs) are developed to deal with particular application domain in which alternative techniques are unable to produce reliable and manageable solutions....
Previous: What was the name given to the supreme being among the Ameru community?

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions